Fathima Godabar; Mwanamke anayeongoza kwa uzuri duniani

Fathima Godabar; Mwanamke anayeongoza kwa uzuri duniani

Mkuu...naamini uzuri ni ujumla wa mtu..sio sura tu! Anaweza akawa na sura nzuri zaidi ya malaika..cheki shepu sasa, Michelini imesingiziwa! She is 'cute'...but to say she is beautiful, I need to see more!
Hata wewe Doctor unataka kumuona zaidi ili uweze kuthibisha uzuri wake ahhhh?
 
kiukweli kwa kigezo hicho cha sura dada huyo ni mzuri sana, ila dhana ya kusema kuliko wote duniani hapa natatanika kwani aliyetoa hilo jumuisho ameshatembea duniani kote? naamini wapo wazuri pengine kumpita ambao hawajapata fursa ya kuonekana na wengi.

..kweli mkuu tena wapo wengine vijijini wakipata exposure,wakapakwa poda lazima wamfunike. alafu huyo ni muarabu sijui atakuwaje mzuri kulikowanawake wote wakati wengine ni wabongo(weusi) vigezo vyetu vya urembo ni tofauti na vyao...
 
mke wangu ndiyo mwanamke mzuri kuliko wanawake wote duniani
 
Huyu dada ni wa kawaida..apo amepakwa make up matata..akiosha uso unga utakaotoka tunapikia chapati kabsa..wangeweka picha hana ata make up ndo tujue uzuri wake..
 
Hakuna mwanamke mzuri ka mke wangu, KWISHAAA!!

hizo nyingine stori tu msifie sura na hadi dada zetu wanatumia carolite kisa wanaamini uso ndio icon/signature ya uzuri.

Zile hijabu za kininja nazipenda sana Washawasha
Zile ndio mpango mzima.
Nalog off
 
Kama umetuletea mwanamke mzuri kuliko wote, tuletee pia mbaya kuliko wote ili tupate vigezo vya uzuri ipasavyo.
 
Kwanza anaweza akawa jini huyo, uzuri gani hamna kitu blod keleb
 
Haaaa! Alaf n'likuwa sjamuangalia vizurii... Kumbe naye ana kidoti... Kama yule miss nanihii yule demu yule hata daimondi alimwimba kwenye nyimbo yake...
 
She looks like those Indian demi gods....
 
Fathima+Kulsum+Saudi+Arabia+queen+3.jpg



Fathima+Kulsum+Saudi+Arabia+queen+1.jpg




wanja umewachanganya nyie
 
Fathima+Kulsum+Saudi+Arabia+queen+3.jpg



Fathima+Kulsum+Saudi+Arabia+queen+1.jpg



KWA UFUPI

Licha ya kujifunika mwili wake wote kwa mavazi yenye stara, hiyo haijawa sababu ya kuficha uzuri

wa asili mwanadada huyu, ambaye kwa sasa anaonekana kuwa mzuri zaidi akilinganishwa na

wanawake wote duniani.



Licha ya usemi unaosema uzuri upo machoni kwa mtu, lakini ukweli utabaki palepale kwamba kitu au mtu hadi kuonekana mzuri, lazima kiwe kimekubalika na watu wengi.

Wengi tumekuwa na fikra kuwa pengine Angelina Jolie na Aishwarya Rai, ndiyo wanawake wazuri duniani. Hiyo imesababishwa na umaarufu walionao walimbwende hao.

Lakini, umaarufu siyo kigezo cha kuwa mzuri kwani wapo watu wazuri mno na hawatambuliki, kwa sababu tu hawana umaarufu kama ilivyo kwa Angelina Joliea au Aishwarya Rai.

Miongoni mwa watu hao ni Fathima Zohar Godabari, raia wa Saudia Arabia, anayesadikiwa kuwa mwanamke mrembo kuliko wote walio duniani kwa sasa.

Licha ya kujifunika mwili wake wote kwa mavazi yenye stara, hiyo haijawa sababu ya kuficha uzuri wa asili mwanadada huyu, ambaye kwa sasa anaonekana kuwa mzuri zaidi akilinganishwa na wanawake wote duniani.

Mwonekano wa sura yake, urefu na wembamba wa wastani unatosha kudhihirisha mvuto wa hali ya juu alionao Fathima. Rangi ya ngozi, uzuri wa nywele na midomo yake inatosha kueleza na kukubali kuwa ndiye mrembo zaidi duniani kwa sasa.

Mrembo huyu anatoka katika familia ya kifalme ya nchini Saudi Arabia akitajwa pia kuwa mstari wa mbele kushiriki katika masuala yenye manufaa kwa wanawake.

Godabari pia ni mwanaharakati anayejihusisha na utetezi wa haki za wanawake na mshauri anayewakusanya wanawake katika makundi madogo madogo kwa lengo la kujisimamia na kupingana na aina yoyote ya ukatili dhidi yao.

Licha ya urembo na moyo wa kujitolea alionao, Godabari anatajwa pia kuwa ni miongoni mwa wanawake wachache kutoka nchi za kiarabu waliofanikiwa kupata kiwango cha juu cha elimu.

Kwa hivi sasa yuko nchini Uingereza ambapo anachukua shahada ya uzamili katika masomo ya uongozi wa biashara.Fathima Zohar Godabari alizaliwa Oktoba 22,1986 nchini India. Kwa sasa amefunga ndoa na Sheikh Awadi Al Muhammad wa ukoo wa kifalme nchini Saudia Arabia.


Imeandaliwa na Elizabeth Edward.chanzo. Fathima Godabar; Mwanamke anayeongoza kwa uzuri duniani - Makala - mwananchi.co.tz



[/QUOTEm

Mbona wakawaida tu? Mbona kuna weusi wengi wazuri kuliko huyo? Au kwasababu ni mweupe? Msiwebrainwashed kwamba uzuri lazima ujumuishe weupe...huyo? Mi ata ajanshtua kabisaa
 
Back
Top Bottom