Fathima Godabar; Mwanamke anayeongoza kwa uzuri duniani

Fathima Godabar; Mwanamke anayeongoza kwa uzuri duniani

Mpwa wangu, habari ya asubuhi, ukisema "uone kwa ndani" ni wapi huko? kwenye Moyo au wapi? hahahahaaaaaaaa najaribu ku-imagine huko ndani unakosema wewe
Kwani uzuri wa mwanamke ni kitu gani? kam sio uso? unataka mpaka uone kwa ndani?ili iweje Mkuu?
 
Tulopokuwa chuoni, bafuni tulikuwa tunaoga weeengi kwa wakati mmoja tena uchi kabisa, mwanzoni ilikuwa inanipa shida sana maana sikuzoea, na ilinichukua muda sana kucoop yale mazingira, nilijifunza kuwa, si vile watu wanavyoonekana wakiwa wamependeza wanapovaa nguo nzuri, ndivyo wanavyokuwa wakivua nguo, huo ni ukweli ambao nimeprove mimi mwenyewe, kwa hiyo huyu anayeitwa mzuri kuliko wote duniani, inaweza kuwa hivyo hivyo, akivua nguo unaweza ukashangaa sana, uzuri wa mtu si sura tu jamani kuna vitu vingi, kama siku hizi ambapo uzuri ni pesa yako!! zipo cosmatic nyingi tunazopaka wanawake siku hizi, ndio maana ukienda kwenye shughuli yoyote kila mtu anaonekana ni mzuri sana kwa ajili ya kupaka decoration, so uzuri si usoni tu kwa kweli
 
Angesema mzuri bt sio dunia nzima hapo amekosea.
Kuna wazuri aise tena wakiwa hawajajiremba
Sembuse huyo full makep
 
Hayo ma make ups ndiyo uzuri??? Wa kawaida sanaaaa. Chukua wadada wa kondoa ..... utasikitika na uzuriiii tena hawajui makeups!!!
 
Jamani mchawi tumseme ila sifa yake ya kupaa na ungo tumpe.
Ni mzuri ila sio dunia nzima sbb wazuri tupo wengiiiiiiiiiiiiiiiiii na wengine kila kukicha wanazaliwa.
 
Huyo ni mzuri lakini my wife ni mwisho wa maneno, kwani huwa ananipa ile kitu inapenda, ananifanya nitembee kifua mbele mtaani.
 
Kwa mimi huyo ni mrembo sio mzuri sababu hapo full makeup. Apige picha bila kuweka kope, kutinda nyusi, hajaweka lensi machoni, yaani awe asilia.
Ukienda ilala watoto wa kiarabu na kipemba warembo na wazuri kupita huyo fathima
 
Fathima+Kulsum+Saudi+Arabia+queen+3.jpg



Fathima+Kulsum+Saudi+Arabia+queen+1.jpg



KWA UFUPI

Licha ya kujifunika mwili wake wote kwa mavazi yenye stara, hiyo haijawa sababu ya kuficha uzuri

wa asili mwanadada huyu, ambaye kwa sasa anaonekana kuwa mzuri zaidi akilinganishwa na

wanawake wote duniani.



Licha ya usemi unaosema uzuri upo machoni kwa mtu, lakini ukweli utabaki palepale kwamba kitu au mtu hadi kuonekana mzuri, lazima kiwe kimekubalika na watu wengi.

Wengi tumekuwa na fikra kuwa pengine Angelina Jolie na Aishwarya Rai, ndiyo wanawake wazuri duniani. Hiyo imesababishwa na umaarufu walionao walimbwende hao.

Lakini, umaarufu siyo kigezo cha kuwa mzuri kwani wapo watu wazuri mno na hawatambuliki, kwa sababu tu hawana umaarufu kama ilivyo kwa Angelina Joliea au Aishwarya Rai.

Miongoni mwa watu hao ni Fathima Zohar Godabari, raia wa Saudia Arabia, anayesadikiwa kuwa mwanamke mrembo kuliko wote walio duniani kwa sasa.

Licha ya kujifunika mwili wake wote kwa mavazi yenye stara, hiyo haijawa sababu ya kuficha uzuri wa asili mwanadada huyu, ambaye kwa sasa anaonekana kuwa mzuri zaidi akilinganishwa na wanawake wote duniani.

Mwonekano wa sura yake, urefu na wembamba wa wastani unatosha kudhihirisha mvuto wa hali ya juu alionao Fathima. Rangi ya ngozi, uzuri wa nywele na midomo yake inatosha kueleza na kukubali kuwa ndiye mrembo zaidi duniani kwa sasa.

Mrembo huyu anatoka katika familia ya kifalme ya nchini Saudi Arabia akitajwa pia kuwa mstari wa mbele kushiriki katika masuala yenye manufaa kwa wanawake.

Godabari pia ni mwanaharakati anayejihusisha na utetezi wa haki za wanawake na mshauri anayewakusanya wanawake katika makundi madogo madogo kwa lengo la kujisimamia na kupingana na aina yoyote ya ukatili dhidi yao.

Licha ya urembo na moyo wa kujitolea alionao, Godabari anatajwa pia kuwa ni miongoni mwa wanawake wachache kutoka nchi za kiarabu waliofanikiwa kupata kiwango cha juu cha elimu.

Kwa hivi sasa yuko nchini Uingereza ambapo anachukua shahada ya uzamili katika masomo ya uongozi wa biashara.Fathima Zohar Godabari alizaliwa Oktoba 22,1986 nchini India. Kwa sasa amefunga ndoa na Sheikh Awadi Al Muhammad wa ukoo wa kifalme nchini Saudia Arabia.


Imeandaliwa na Elizabeth Edward.chanzo. Fathima Godabar; Mwanamke anayeongoza kwa uzuri duniani - Makala - mwananchi.co.tz




Ni maisha bora tu! Nenda kwetu Maramba tanga ukakutane na vitu mkuu.Sema vimepigika kwa maisha ya kibongo.
 
aaaah mke wang mzuri sana, i love her african beauty popote ulipo..... ila uzuri wa mwanamke sio urembo(wanja,poda,lipshines) ni tabia ati salam zifike
 
Back
Top Bottom