Fataki............ Umewahi kujiuliza haya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fataki............ Umewahi kujiuliza haya?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by WomanOfSubstance, Jul 25, 2010.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Katika kuwalinda wasichana dhidi ya KUDANGANYIKA na KUHARIBU NDOTO ZA MAISHA YAO... kuna matangazo kadhaa yanatoka kwenye redio na TV kuhusu "FATAKI".Hivi ndugu zanguni, pamoja na nia njema kabisa ya kutetea haki za watoto wa kike, mmeshawahi kujiuliza athari wazipatazo wakina kaka, baba wenye majina ya FATAKI, na vile vile watoto ambao baba zao wana majina ya FATAKI? Leo nilisikia kisa cha mtoto aliyetaka baba yake anayeitwa FATAKI abadili jina maana shuleni watoto wenzie wanamcheka! Baba naye akajaribu kumshari mwanae kuwa jina hilo lina historia ndefu sana katika ukoo na hawezi kubadili! Nikajiuliza, huyu mtoto naye si ana haki zake? Huko shule kama anataniwa ni dhahiri kuwa anapoteza kujiamini, ana athirika kisaikolojia na hatimaye athari hizi zina uwezekano kum haribia ndoto zake za maisha bora huko mbeleni.

  Kwa haraka haraka, nikasema hili linahitaji mjadala mrefu ili kudadavua yaliyomo kama yamo ninavyoyaona mimi.
  Karibuni tujadili ili tuwalinde wenye majina ya FATAKI na kutetea haki zao.
   
Loading...