Fastest train-Kwa nini mchina wa Tanzania na wa nchini china ni tofauti? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fastest train-Kwa nini mchina wa Tanzania na wa nchini china ni tofauti?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zhule, Dec 27, 2009.

 1. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tutumaini iko siku tutafika?Hivi wachina wanaopewa tenda Tanzania hata barabara wanashindwa kutengeneza ndo hawa wanaotengeneza hizi Traini? Kwa nini utendaji wa mchina akiwa Tanzania na akiwa nchini kwao ni Tofauti?
   

  Attached Files:

 2. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  A train from Beijing to Wuhan enters a railway station in Wuhan, central China's Hubei province, October 22, 2006. The 201-metre-long passenger train runs with a speed of 200 kilometers per hour, the fastest in China. It has two warhead-shaped train heads on both end.
  utadhani ndege!!
   
 3. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,840
  Likes Received: 1,099
  Trophy Points: 280
  Mkuu sasa wametoa yenye speed zaidi ya 350km/hr toka Wuhan kwenda guangzhou. Hiyo ndiyo treni yenye mwendo kasi kuliko zote duniani.
   
 4. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #4
  Dec 27, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...'labda' makandarasi na bajeti za mradi ikiwemo 10% (cha juu), malengo na accountability zinatofautiana.
   
 5. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #5
  Dec 27, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,597
  Likes Received: 3,888
  Trophy Points: 280
  Mkuu mbona thread yako haieleweki? mbona hata hawa watanzania wakiwa nje wanafanya mambo makubwa , nao hawaipendi Tanzania

  Ishu ni fedha hapa mkuu, usije ukafikiri mjenzi ndiyo ana determine quality ya kitu.NI FEDHA,Mjenzi ni robot,ukimwambia jenga nyumba ya gorofa mia atajenga,ukimwambia jenga kibanda cha mbwa atajenga!

  sijaoa kabisa basis ya argument yako, unless haujuia ishu nzima za ujenzi unavyokuwa, kuna kuwa na client, dsigner, mkandarasi yeye ni mtu wa kuexcute tu ujenzi.

  .Unless sijakuelewa au haujaeleweka.

  Leo hii ukiona barabara inachelewehswa kujengwa, mbane consultant
   
 6. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #6
  Dec 27, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  In actual fact Chinese really sack. Fake products come in the name of CHINA in the world we all know BUT why? Ujamaa ndio basis yake na inaonyesha UJAMAA si njia ya uchumi sustainable and it proven FAILURE everywhere, including the bloody Tanzania. Outcome ya Ujamaa ni FAKE everything! Ufisadi, kughushi, ubinafsi nk.
   
 7. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #7
  Dec 27, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,840
  Likes Received: 1,099
  Trophy Points: 280
  mkuu upo sahihi kabisa, mimi nidhani kwamba hujamwelewa (nadhani hakuwa serious ktk kui-present issue) yeye amelalia moja kwa moja ktk assumption waliyonayo watanzania wengi kwamba kitu chochote cha China ni feki.

  Watu wanasahau kwamba China wanauza vitu mbalimbali Ulaya na USA. China ni supplier wakubwa wa vioo USA. China wako juu sana ktk teknolojia, jamaa wanauwezo mkubwa sana.

  Tutabaki tunakalia maneno, kubeza na kukejeli kumbe wenzetu ndo wanakwenda nasi tunakalia maneno.

  Mkuu Waberoya umesema sawa kabisa, client ndo anaamua quality ya kitu anachotaka. Nina jamaa yangu ni mfanyabiashara, ananunua bidhaa zake Guangzhou, jamaa anadai akiwa kule anajitambulisha kama Mkongo au Mkenya ili kukwepa kuuziwa vitu feki. ukisema wewe ni Mtz wanakuuzia vitu feki. Wanadai watz wanaangalia bei siyo quality.
   
 8. M

  Mende dume Member

  #8
  Dec 27, 2009
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  May be u are right that ujamaa sacks! But have you learnt that all economic criss in the world are a result of uncontrolled overgrown capitalistic economy? think again the problem is not ujamaa and its familly it is the level of production, look at what china is doing today is respected accross the global. Europe in moving toward china and so is US.

  let think again on our ujamaa edit it a bit and move ahead,
   
 9. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #9
  Dec 27, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  mbomoa nchi NI MWANANCHI
   
 10. e

  echonza Senior Member

  #10
  Dec 28, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 163
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu mtoa thread anaeleweka kabisa! Suala hapa siyo makandarasi bali ni utofauti uliopo kati umakini wa wanchina kusimamia miradi ya maendeleo nchini kwao na watanzania wenyewe hapa Tanzania. Watanzania tumejaa ujanja ujanja tu, utapeli, ubinafsi, kukosa uzalendo, kuwa na makundi ya wachache, kuwatenga wanyonge na kubwa zaidi kutetea wezi.

  Kwa sababu ya visababishi vichache hivyo hapo juu nilivyovitaja katika vingi ambavyo mtu anaweza kutaja kwa madhaifu ya Serikali yetu kusimamia matumizi ya fedha za umma kunasababisha Makandarasi kutoka China kupewa tenda mbalimbali hata kama hawajaonyesha uwezo wowote wa kiutendaji, ili mladi tu gharama zao zitakuwa kidogo. Na kwa sababu hiyo, kwa vile viongozi wetu unakuta wanamezea mate fedha za umma, huona ni vyema kumpa Mchina ili cha juu kitakachobaki kiweze kutumbuliwa na kundi fulani hivi.

  Suala siyo fedha, Tanzania siyo masikini wa fedha, bali sisi ni masikini wa kutekeleza mipango yetu inayoendana na vipaumbele vya nchi (mahitaji muhimu ya wakati huo kwa kuwapunguzia wananchi ugumu wa maisha). Mfano mzuri ni ujenzi wa barabara ya kutoka Dodoma kwenda Mwanza. Suala pale halikuwa ukosefu wa fedha ndugu yangu, bali lilikuwa ni utekelezaji wa mradi huo muhimu kuingiliwa na masilahi ya kundi fulani (10%)! Mbona nyumba za akina Ndulu zinajengwa? Mbona TaNESCO wanaweza kulipia miradi yao bubu? Mbona Richmond T Ltd ilikuwa inalipwa fedha kwa mujibu wa mkataba? mbona IPTL ilikuwa inalipwa fedha nyingi tu? Mbona majengo pacha yameweza kusimamishwa kwa gharama hizo zilizowafikisha watu mahakamani? Na mengi ya namna hiyo!!

  Ndiyo sasa sababu ya kwa nini Watanzania hao hao wanaoonekana kushindwa ndani ya nchi yao, wakienda nchi nyingine huonekana wakombozi wa uchumi wa nchi husika kwa sababu ziko makini kusimamia utekelezaji wa mipango yake ya kitaifa! Wana uzalendo, japokuwa kazi husika inafanya na mikono ya wataalamu kutoka Tanzania, wote wanakuwa na wito wa kuona matokeo mazuri ya walichokipanga kukitekeleza kwa ajili ya kusonga mbele kiuchumi. Ukiwa Tanzania, kutofanikiwa kwa utekelezaji wa mradi fulani ni ulaji mwingine mpya kwa watoa maamuzi kupitia 10%.

  Hadi hapo Tanzania kupitia uongozi wake itabadilika na kuvaa uzalendo ndipo hapo mafanikio ya utekelezaji wa miradi tuliyojipangia kuweza kukamilika kwa kiwango kinachotakiwa na kwa wakati unaotakiwa pia!
   
 11. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #11
  Dec 28, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante naona umenielewa.
   
 12. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #12
  Dec 28, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni kweli ukinielewa. Kwanza i didnt conclude that ishu ipo kwa mchina ila nimeona utofauti wa utendaji wao wa kazi kwao(majengo yao barabara zao madaraja nk) na kwetu nikauliza kulikoni? wao wewe unapropose kwetu pesa.lakini je yishu ni pesa au 10% au viongozi wetu?.umeambiwa garama ya kujenga majengo pacha ya benki kuu ni mara ngapi ya kujenga london?umeambiwa gavana wa benki akiwa marekani nyumba aliyokuwa akiishi ni dola.2mil. akiwa tanzania anakarabati nyumba kwa >1mil.uchumi wetu ni nusu ya marekani? China majengo kama ya machinga complex wanajenga kwa miezi miwili je hapo wamechukua miezi mingapi? uwanja wa taifa mara mabomba ya kupitisha maji ni madogo je umeona bird-nest yao wakati wa ulimpiki?. kwao barabara kilomita moja wanajenga kwa yuao milioni 6 karibia na 1.mil usd. kwetu bei pia ni hiyo hiyo ya Tshs.1bil wanapewa. Sasa njoo uone bara bara zao uimara, upana na kasi za ujenzi.nadhani swala siyo pesa. May tujiulize tena hawa wajenzi wenyekiwango cha kuunda traini hii, majengo haya na barabara hizi ndo hao wanakuja kwetu?Brand za china wanazotumia huko kwao makampuni ya simu, ujenzi, biotechnologies za kwao kweti sizioni ndo najiuliza au hawa wajenzi ni uchwara? au 10% ndo nikaileta jambini what is up?
   
 13. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #13
  Dec 28, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ukunielewa vile vile hoja ingekuwatechnologia nisingesifia hiyo train.nimeuliza kwa nini utendaji kazi wao ni tofauti wakiwa tz na kwao China na gharama za ujenzi ni zile zile?
   
Loading...