Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,498
Huyu Faris amerudia kauli zake za vitisho baada ya kusema wakiwapoteza watu polisi wasiingilie amerudia tena kwa Watu waliopanga kuandamana Oktoba 29
=
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kagera ndugu Faris Buruhani, amewasihi na kuendelea kuwaomba wananchi wa mkoa wa Kagera kujitokeza kwa wingi Oktoba 29 mwaka huu kwenda kupiga kura nyingi kwa wagombea wa Chama Cha Mapinduzi na kuachana na upotoshaji unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uvunjifu wa amani siku hiyo ya uchaguzi.
Soma > Mwenyekiti UVCCM Kagera, Faris Buruhan: Tukiwapoteza wanaomtukana Rais Samia mitandaoni, Polisi msiwatafute
Faris amesema ubora, uweledi na umahiri wa wagombea walioletwa na CCM kwa wananchi, ni kielelezo tosha cha wananchi kuwapigia kura nyingi ili wakaisimamie Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2025-2030 inayolenga kusogeza huduma kwa wananchi.
Faris ameyasema hayo Septemba 23, 2025 kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea ubunge wa jimbo la Bukoba Mjini, Injinia Johnston Mutasingwa uliofanyika kwenye kata ya Kibeta na kuhudhuriwa na wananchi wengi wa Kibeta na Bukoba mjini kwa ujumla.