Fanya mambo kama mwanaume ili uwe mume

Fanya mambo kama mwanaume ili uwe mume

Nakubaliana na mwanaume kusimamia show. Ila naomba niulize swali Sky.

Hivi uanaume ni nini? Ni kuhudumia familia/mwanamke?

Je, mwanamke akihudumia familia 100% naye ni mwanaume? Je, mwanaume asipomhudumia mwanamke uanaume unakwisha?
 
Ukiwa kama baba wa nyumba unatakiwa ujue mahitaji ya familia pesa yetu ni ya kuongezea pale inapohitajika lakini isitegemewe
Ndio maana wanaume wa kiafrika tunawahi kufa na hatuendelei. Mke badala ya kua msaidizi anakua mnyonyaji, kupe, yeye ni kuhakikisha unakamlika hadi ufe.

Wanawake wa kiafrika ndio maana wanapenda sana kuolewa, hawaoni kama hawawezi kuishi bila mume maana akili yao yote iko kwenye kumtegemea mume hata kama mke ana kipato kikubwa kuliko mke.

Ndio maana watu kama mimi tushaona hakuna umuhim wa kuoa, kama ni watoto unazaa na wanawake wawili au watatu mtoto mmoja mmoja kisha unatunza watoto, maisha mukide.
 
Mleta mada umeteleza. Hakuna mwanaume anayejitambua anayeweza kukwepa majukumu yake kama ana uwezo huo. Dunia imebadilika sana, kwa sasa Wanawake wengi tu wana Kazi nzuri na wanalipwa vizuri sawa na wanaume au hata zaidi. Sasa kama wewe na mumeo mna vipato vizuri na amekuomba mchango wako ili kusukuma familia na nyingine ziende kwenye maendeleo shida iko wapi? Hii tabia ya kichoyo ya kutaka mwanaume akufanyie kila kitu wakati majukumu ya nyumbani anayafanya house girl sio nzuri hata kidogo. Kumbe maisha ni ya wawili, kama yeye ndo maisha anayoyataka kwanini usiende nae na umsupport?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli unavyosema, mwanaume ukikubali kuwa dunia imebadilika na unaishi na co-partner basi na wewe ukumbuke kupuga deku chooni na kufua mashuka J' most. Huwezi kuwa na keki yako na kuila kwa wakati mmoja
 
Kha! Huku tunapoelekea wanawake wanazidisha uchoyo ya vijipesa vyao. Yani baadhi ya wanawake wa kileo ni bora akupe tigo kuliko akupe pesa zake. Why? Ishini kijamaa ndani ya ndoa. Ndoa ni kusaidiana. Huyu akipata huku na huyu akipata kule mkaunganisha nguvu, mnapiga hatua haraka...
 
me love u you know

Ndio maana zamani kijana akitaka kuoa anaulizwa uwezo wa kuhudumia familia. Kuwa na shamba, makazi na uwezo wa kujishughulisha..

Mambo yakienda vibaya kwenye nyumba, anaelaumiwa ni mwanaume. Sikatai kuna kipindi mambo yanagoma kwa kitamvo lakini isiwe utaratibu wa kumfanya mke abebe jukumu lisilo la kwake, na ukitekeleza wajibu wako, bila hiyana unakuta anasaidia baadhi ya mambo hata bila shurti, nnachopinga ni ile mke kuingizwa kwa ulazima abebe kuhudumia familia.

Barikiwa sana rafiki
 
Nakubaliana na mwanaume kusimamia show. Ila naomba niulize swali Sky.

Hivi uanaume ni nini? Ni kuhudumia familia/mwanamke?

Je, mwanamke akihudumia familia 100% naye ni mwanaume? Je, mwanaume asipomhudumia mwanamke uanaume unakwisha?
Daby mwanaume anaebeba majukumu ya familia ana mamlaka kamili ya familia yake. Kama ma waume unajisikiaje ufike nyumbani fridge imejaa na unakaa kabisa kwenye sofa unaomba uletewe bia unywe. Kesho mke akichelewa kurudi una ubavu wa kumuuliza ulikuwa wapi?
 
Ndio maana zamani kijana akitaka kuoa anaulizwa uwezo wa kuhudumia familia. Kuwa na shamba, makazi na uwezo wa kujishughulisha..

Mambo yakienda vibaya kwenye nyumba, anaelaumiwa ni mwanaume. Sikatai kuna kipindi mambo yanagoma kwa kitamvo lakini isiwe utaratibu wa kumfanya mke abebe jukumu lisilo la kwake, na ukitekeleza wajibu wako, bila hiyana unakuta anasaidia baadhi ya mambo hata bila shurti, nnachopinga ni ile mke kuingizwa kwa ulazima abebe kuhudumia familia.

Barikiwa sana rafiki
Ni kweli kabisa na mwanaume anaebeba majukumu tunakuwaga wepesi sana kugundua kuwa mambo yake si mazuri. Kuna vitu kama cornflakes za watoto, socks, kalamu ambavyo mwanamke anaona huruma hata kumwambia baba yao
 
kama kuna nia ya kujenga familia imara haina hata haja ya kuhimizana. zitatoka hata zaidi ya 50%. Napenda mwanamke muwajibikaji katika familia. Mwanamke akiwajibika hata mimi nitawajibika asilimia zote.
Kwa hali hiyo atakunyanyasa tu
 
Daby mwanaume anaebeba majukumu ya familia ana mamlaka kamili ya familia yake. Kama ma waume unajisikiaje ufike nyumbani fridge imejaa na unakaa kabisa kwenye sofa unaomba uletewe bia unywe. Kesho mke akichelewa kurudi una ubavu wa kumuuliza ulikuwa wapi?
Nakubaliana na hili...

Nwei, labda nimeshindwa kuweka vizuri swali langu lieleweke
 
Nina vitoto viwili under 5yaani kwa jinsi vinavyompelekesha mama yao natamani hata niwe namlipa mshahara maana mimi hata kukaa nao nusu saaa ni shida ila mke anavumilia masaa 14 wakati niko kazini achana na majukumu mengine ya kifamilia....50%?hapana kujitolea kwake lkunihudumia mimi na haya majembe inatosha sana, mimi natafuta nampelekea yeye na akiba naweka asee, ukimpata mwanamke anayeridhika na kipato ulichonacho na bado kile kidogo unachompa anameki.....unabahati sana now days....huu ni mfano mdogo tuu...umemuachia mkeo 10000 asubuhi baadhi ya vitu muhimu vipo nyumbani, mwenzako anaweza tumia 7000 nyingine akaweka, hawasemagi kama wanaweka ila fahamu kuwa hawatumiagi yote, siku umekwama kabisa amini hamtolala njaa, na ikipita sendozi nzuri utanunuliwa na hata nguo....kwa pesa ile ile anayomeki....ukiwa na akili ndoa ni tamu sana....ila ukiwa unaenda mwenyewe sokoni au unapiga hesabu kwa kila unachotoa hapo hata pesa ya pampas ya mtoto utatoa wewe.
 
Ni kweli kabisa na mwanaume anaebeba majukumu tunakuwaga wepesi sana kugundua kuwa mambo yake si mazuri. Kuna vitu kama cornflakes za watoto, socks, kalamu ambavyo mwanamke anaona huruma hata kumwambia baba yao
Mawazo yako ni mazuri sana ila wengi wenu mnaharibiwa na ndugu zenu kuwaeleza wanaume hawatabiriki anaweza kuoa mwingine. Inatakiwa nawe ujenge kwa siri etc. Aidha mwanamke akihisi unachepuka atakomoa tu hata akiwa na mamillion hatoi hata ndululu.
 
Ni pale mwanaume anapokhimiza utoe 50% ya budget yenu ya ndani, hapo si umeshajiweka kuwa unaishi na co-partner? Baada ya hapo unaamka asubuhi unategemea utandikiwe kitanda na boxers zako kule bafuni zifuliwe. Kama mke mambo yake yake yakienda vibaya si unamuweka kwenye hatari ya kupata kidume cha kumpa ile 50% ambayo unaitegemea? Kama unataka kuweka heshima ya ndoa ndani jitume kama mwanaume kwanza pesa yetu ni ya chumvi na mchuzi mix.
Enzi za babu, bibi, baba na mama zetu ningekubaliana nawe kwa hili, ila kwa maisha ya sasa, HAPANA 110%, sababu wafua boxers n.k. isiwe kisingizio cha mke asitoe mchango wake ndani ya nyumba, mbona ni kujipanga tu, kwanza kiasi gani?! Wataka hela zenu zote ziishie Boutique na Saloon? Kwa sasa mwadai usawa, mwataka kila kitu kitu kiwe pasu kwa pasu, sasa huoni usawa uanzie nyumbani kwetu kwanza? Mamie ili mambo yaende kila mtu kwenye boma letu lazima a chip in, kuanzia sisi, watoto wetu kama wakubwa n.k.
Note : Wanaume wengi wanapenda vitu natural, punguzeni vikolombwezo feki kama nywele, eyelashes, makeup, nails n.k. mbona hela itatosha tu ndani ya nyumba..
 
Kwahiyo unakubali kuwa dunia hii ya leo tunaishi na co-partners?
 
Sky, kwa nini basi wote tuamke asubuhi, tuwaache watoto wadogo kabisa(imagine after three months mama anamuacha kichanga home anaenda kazini), twende kazini, turudi saa mbili usiku, watoto hawatujui vizuri coz tunatafuta pesa.

Then kipato cha mmoja kiwe "optional" kutumika? Hivi, what's the point you waking up at 0500hrs, coming back home at 2200hrs if you are stingy to your own family and can't share your income?

Nilidhani point ya wote kuamka saa 11 na kurudi saa nne ni kutafuta pesa kwa ajili ya familia. Sasa kama mmoja anaona kipato chake sio cha familia, anaitwaje family member? Na kwa nini aamke saa11, angekaa tu home ingekuwa busara zaidi.
 
Mwanamme akikubali 50/50 kwenye kuhudumia (matumizi)...hana budi kukubali 50/50 kwenye majukumu mengine.
Mfano, kupika, kufua, kuangalia watoto, usafi wa nyumba nk.
Isiwe tu kwenye budget. ...
I concur
 
Back
Top Bottom