Fanya haya kutatua changamoto ya spika simu inayokoroma

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,568
1691421731660.png

Simu yako imeingia maji?, spika yako inatoa sauti ambayo huipendi? sawa pole kwa changamoto hiyo karibu hapa kwa suluhisho.

Usipeleke simu kwa fundi kwanza, wala usiweke kwenye mchele.

Kama umekutana na changamoto tajwa hapo juu au za namna hiyo, kwa muda huu ambao unasoma hapa, basi fanya hivi.

Ingia kwenye ''search engine'' mfano Google, Safari, Chrome na nyinginezo alafu andika ''Fixmyspeaker'' Link hii hapa Fix My Speakers - Eject water from your phone's speakers

Ukishaingia utagusa kwenye ki-mchoro cha maji mfano pichani sogeza kushoto, utasikia sauti ikitoka hiyo sauti ndio itakufahamisha kwamba spika ya simu yako bado iko njema na pia itakusaidia kutoa maji yaliyomo kwenye spika.

Nje na hapo kama bado changamoto ni ile ile ndipo unaweza kwenda kwa fundi.
 
Sasa kuomba msaada kwa watu wangu wa karibu si ndiyo kwenda kwa fundi sasa

We nae umezengua tu
 
Nisaidie na solution ya cm kujiponyeza home botton Kama iko ndani ya uwezo wako mkuu maana imebidi niache kutumia cm kubwa kwa sababu iyoo!maana kila ninapojaribu kuitumia inakuwa inakiponyeza home botton na kufungua Google assistant muda wote
 
Umejaribu ku factory reset? Naona ni njia rahisi kusuluhisha matatizo kama hayo
 
Back
Top Bottom