Sisi Waafrika ni binadamu wa aina gani?
Hebu chukulia kwa mfano janga la njaa kuu linaloendelea katika pembe ya Afrika. Sikubaliani na dhana kwamba hakuna hata nchi moja ya Kiafrika yenye uwezo wa kusaidia hata angalau kwa kuonesha nia njema tu.Ni kweli kuwa Tanzania, au Zambia, au Botwasana nchi hizi haziwezi hata kutoa tani hamsini hamsini tu za mahindi kusaidia?
Mimi nafanya kazi na shirika la kutoa misaada, na inanisikitisha kuona nchi kama Slovakia, Bangladesh au Maldive zimo katika orodha ya nchi zinazotoa misaada ya kibinadamu, wakati nchi kama Nigeria, Angola, Gabon eti haziwezi! Siku zote tumezoea kupewa sisi. Jamani, hii akili ya 'kuruzukiwa' itakwisha lini? Kweli sisi twastahiki matukio yote ya maajabu yaliyotusibu katika historia: hatujithamini na wala hatuna 'pride'.