Family intelligence; Utajuaje mchumba wako ni muaminifu kwenye mapato au Fedha?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,891
FAMILY INTELLIGENCE; UTAJUAJE MCHUMBA WAKO NI MWAMINIFU KATIKA MAPATO/FEDHA?

Kwa Mkono wa, Robert Heriel.

Basi Mimi Taikon nikajiingiza katika Mkondo WA mapenzi. Nikasema Acha niyapime mambo yote yaliyomo huko, kisha nitoe Hesabu Kwa kadiri ya akili yangu ilivyo Kwa wakati huu ningali kijana Mdogo.

Basi maneno haya nimeyapima nayo nikayathibitisha yakuwa ni kweli. Na hii ndio sehemu ya Hesabu ya majibu yake Kwa habari za uaminifu katika mapato na Fedha.
Basi andiko hili lawafaa zaidi Vijana ambao bado hawajaoa, walitumie ili wasaidike.

Niite Taikon wa Fasihi, Mpimaji wa Dura ya Mapenzi.

Family intelligence ndio msingi na nguzo kuu ya familia na mahusiano ya ndoa family intelligence ndio inayoweza kuifanya ndoa na familia kuwa Bora au kuwa familia dhaifu.
Hakuna maisha pasipo intelligence, hakuna Utawala pasipo intelligence,

Vijana wanapochumbiana huanza Kwa kuchunguzana wao Kwa wao Kwa mambo madogo madogo Kama vile Majina, koo, elimu, tabia na mambo mengine ya kiafya.
Uchumba msingi wake Mkuu ni Upendo Kama yalivyo maisha, lakini upendo ni kitu aghali na cha thamani Sana kuliko vitu vyote Duniani hivyo hauwezi kuwekwa sehemu pasipo upelelezi wa kina kufanyika.

Intelligence na hapa namaanisha masuala yote ya kipelelezi/uchunguzi na kijasusi yanayohusu usalama na ulinzi.
Hapana Upendo pasipo intelligence.
Wanasema siku zote ni salama panapoupendo, lakini nami nasema siku zote panaupendo palipo na intelligence.

Upendo pasipo intelligence ni Dalili ya wendawazimu, kutojitambua na kutojua thamani ya Upendo wenyewe.
Huwezi penda kitu usichokijua, kumaanisha huwezi mpenda mtu usiyemjua, huko ni kuchanganyikiwa.
Na ili umjue mtu sharti intelligence IFANYE kazi yake.

Kama ilivyo katika biashara kubwa, huwezi wekeza biashara kubwa pasipo kufanya uchunguzi wa kina, labda uwe mwendawazimu uliyepungua kiakili.

Siku hizi Vijana wengi wameshindwa mambo mengi mpaka Yale yaliyorahisi kabisa Kwa sababu ya upumbavu na upuuzi.
Vijana mapenzi yamewashinda Kwa sababu wanachukulia mambo kirahisi hata Kama ni mambo mazito yenye thamani. Upendo na Mapenzi ni mambo mazito ambayo yanagusa moyo na roho yako, lazima mtu awe macho anapoingia katika mapenzi.

Vijana hawataki intelligence wao wanafikiri mambo yanaenda kiholela Kama waishivyo wanyama wa mwituni.
Huwezi tafuta mchumba ambaye ni mke WA baadaye Kama jogoo akimbizavyo mtetea.

Family intelligence inaanzia kwenye Uchumba kabla ya kuingia ndoani.

Unapofanya uchunguzi kuna mambo makuu lazima uyazingatie na kuyatolea ripoti ya mchumba utakayemuoa, mambo hayo ni;

1. Asili ya mchumba wako.
Majina yake, ukoo wake, kabila lake, je wanamagonjwa ya kurithi, tabia za kurithi Kama uchoyo, umalaya, udokozi, na ulozi n.k
Asili itakusaidia kujua alipotoka, alipo na atakavyokuwa miaka ijayo.
Mara nyingi maji hufuata Mkondo, ingawaje wapo Exceptional lakini hawa ni wachache mno.
Umuonavyo Mama wa mchumba wako alivyo basi kuna uwezekano 90% mchumba wako akawa vivyo hivyo Kama Mama yake.
Hiyo 10% huwa Kwa wale Exceptional.

2. Maumbile na tabia zake binafsi.
Mbali na Asili kutoka kwao pia chunguza maumbile yake, tabia zake binafsi ambazo hajarithi.
Inafahamika kuwa kila mtu anaupekee wake, lazima uufahamu upekee wa mchumba utakayemuoa.
Hiyo itakusaidia kumdhibiti nyakati za hatari.


3. Matazamio, ndoto na malengo yake.
Lazima uchunguze ndoto ya mchumba wako ya baadaye ni ipi. Usije baadaye ukumuona amebadilika kumbe ni baada ya kuona uwezekano wa kufikia ndoto zake kupitia wewe ni mdogo.
Hakuna mwanamke mwenye tamaa isipokuwa kila mwanamke anandoto yake au matazamio yake. Vile ambavyo ubongo wake uliyafikiri maisha yake yatakavyokuwa hapo baadaye.

Ndoto za mchumba wako ni nini, je mchumba wako anataka baada ya miaka kumi ijayo awe katika maisha ya kiwango na namna gani?
Usijeoa binti wa watu kumbe anataka miaka 10 ijayo muwe mpo kwenye nyumba yenu, ndani ya Gari na safari za Kwenda nje ya nchi kutembea kufurahia maisha.

Utasema Mkeo anatamaa kumbe wewe ndio haukumuelewa. Lazima umpime, uchunguze na kujua ndoto na matazamio ya mchumba wako.

4. Uwezo wa kufanya tendo la ndoa.
Lazima uchunguze mchumba wako anauwezo upi Kwa kiwango gani cha kufanya mapenzi(Yale ya kitandani).
Wapo wanawake wenye uwezo wa juu kabisa na kiwango cha juu kabisa hawa hutaka walau Kwa siku mara moja au mbili. Kundi hili wapo wachache
Wapo wa kiwango cha Kati ambao hawa mara moja kwa siku au kila baada ya siku mbili tatu Hufanya tendo la ndoa, ikiwa wanaafya njema. Kundi hili wapo wengi

Na wapo Wale ambao uwezo wao ni wachini Kabisa, hawa Mapenzi huyaona kero, hawa kufanya mara moja Kwa mwezi au kila baada ya wiki mbili. Kundi hili wapo wachache.

Uchunguzi huu utakusaidia wakati ujao mkiwa mmeingia ndoani, usije ukaoa mwanamke ambaye uwezo wake ni wakimataifa yaani level ya juu yeye kila siku anataka mara mbili alafu mwenzangu na miye uwezo mdogo. Utakwama.
Au wewe unataka kila siku alafu mchumba wako uwezo wake ni mdogo. Mtakwama.


5. Fedha, Mali na mapato.
Lazima uchunguze akili na moyo wa mchumba wako unachukuliaje Mali, Fedha na ishu za mapato
Kipengele hiki ni moja ya vipengele nyeti ndani ya ndoa.
Hapa kuna mambo mawili, la Kwanza ubinafsi na lapili ni uaminifu na ukarimu.

Andiko hili lililenga Kueleza Kwa ufupi family intelligence katika kipengele cha Fedha, Mali na mapato.

Family economy ni moja ya nguzo na kipengele nyeti kinachoijenga Familia. Hii ndio injini ya familia, uchumi wa familia ndio unaoendesha mahusiano na kufanya familia na watoto wawe vile uwaonavyo.

Unapoingia ndoani mtu yeyote makini iwe mke au mume lazima macho yake yote yawe kwenye uchumi wa familia, lazima Fedha zinazoingia na kutoka ziangaliwe Kwa jicho la kipekee na mwanandoa yeyote makini. Fedha ni sehemu ya eneo ambalo ndoa nyingi huanguka Kwa kutokuelewana, aidha mke au mume kuwa msiri au mbadhirifu wa pesa za Familia.

Kama kijana unayetaka kuwa na familia imara, lazima umchunguze mkeo mtarajiwa katika kipengele cha uaminifu ndani ya mahusiano yenu.
Fedha ni nzuri ndani ya familia lakini pia hizo hizo ndio hutumika kuiangamiza familia, wapo wengi wameuawa na wenza wao kisa Fedha za Familia.

Family intelligence lazima ianzie kwenye Uchumba kabisa ambapo ndio msingi Mkuu wa ndoa.


Namna gani ya Kupima uaminifu wa mchumba wako Kwa masuala ya Fedha na mapato?

1. MPE PESA MCHUMBA WAKO KISHA KESHO YAKE MPE JARIBIO.
Wanawake wengi ni Wabinafsi na wachoyo, tena ukikutana na ambaye hakupendi ndio Kabisa. Ila mwanamke anayekupenda haoni shida ku-share na wewe pesa Kwa pamoja.
Utakapoenda Out na mchumba wako jaribu kujifanya Kama pesa zimeanguka au hazitoshi hivyo anapaswa akusaidie kulipia Bills, mpime angalie response yake, angalia body language yake utajua mchumba wako ni mtu wa namna gani.

2. MTUMIE PESA MCHUMBAAKO KUPITIA KWA WAKALA ALAFU USIMPE TAARIFA.
Jaribio la Kwanza ni jepesi Hilo wengi watashinda lakini hili lapili 90% watashindwa.

Taikon nilishawahi kufanya jaribio hili Kwa wanawake kumi kwa nyakati tofauti tofauti, nane walishindwa, wawili tuu ndio walishinda.

Mwanamke yeyote ambaye utamtumia pesa Kwa njia ya wakala au namba nyingine ambayo sio yako asiyoitambua, alafu akakaa kimya bila kukuuliza kuwa kuna hela umemtumia huyo usimuamini, huyo ishi naye tahadhari zaidi kwani hapo hauna mke mwaminifu anayekupenda na kukutii.
Mwanamke wa hivyo huweza kutakatisha pesa haramu azipatazo nje pasipo wewe kujua.

Ni wanawake hao hao ambao huweza kuwa wakawa wanacheza michezo hatari ya pesa Kwa siri pasipo kukushirikisha.

Lazima ujiulize ni Kwa nini asikushirikishe wakati wewe ndiye Mume wake.

Family intelligence katika uchumi wanfamilia ni muhimu kwani pia katika kutekeleza miradi ya familia inayozalisha pato la familia inaweza ingiliwa na ufisadi.
Hujawahi sikia mtu kaoa mke, wanaishi nyumba ya kupanga lakini mke wake Hana kazi lakini anajenga kwao?

Hujawahi sikia mtu anamhudumia mke wake alafu pesa hizo hizo zinatumika kuhonga wanaume wengine wanaolala na Mkeo?
Hujawahi sikia Mke anatumia pesa hizo hizo za mumewe kwenda kumloga?

Hujawahi sikia Mke anatumia pesa hizo hizo kuhonga madaktari pale unapoenda Kupima DNA siku mume akikutwa na mashaka na watoto?

Family intelligence ni Jambo Pana ambalo licha ya ukubwa wake bado Mume unapaswa kulimudu kikamilifu.

Endapo utakwama hapo kwenye Family intelligence basi Hesabu huna familia, Mkeo atakuchezesha na watoto watakupasua kichwa.

Kufika hapa sina la ziada.

Ni yule Mtibeli

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Pesa yoyote inayozalishwa iwe na mume au mke baada ya kuoana ni pesa ya Familia.
Pia siku hizi kuna njia nzuri sana imeingia mjini. Njia nzuri kabisa ya kumpima mwenza wako (hasa kwa wanaume kuwapima wanawake) siku hizi ni social media (kwa wale wenye account kwenye hizi social media). Nakuhakikishia kwa kungalia picha anazopenda kupost, caption anazoandika, marafiki zake nk unaweza kujua tabia na mwenendo wake kwa asilimia kubwa.
 
MKEO ANA 5000 WEWE UNA 5000 JUMLA NI 10,000 LAKINI SIKU HIZI WANASEMA FAMILIA INA 5000 TENA YA MUME SIO YA MKE


Muachishe kazi ili ibaki hiyo elfu tano.

Mwanamke akiwa na nguvu ya pesa mnyime moyo wako. Usimpende.

Mwanamke ili umtawale yakupasa akose nguvu ya pesa au upendo au vyote viwili.

Kitendo cha kuwa na pesa alafu ukampa moyo hapo umempa kukutawala.
 
Muachishe kazi ili ibaki hiyo elfu tano.

Mwanamke akiwa na nguvu ya pesa mnyime moyo wako. Usimpende.

Mwanamke ili umtawale yakupasa akose nguvu ya pesa au upendo au vyote viwili.

Kitendo cha kuwa na pesa alafu ukampa moyo hapo umempa kukutawala.
NDIO MAANA TUNAAMBIWA TUSAKE HELA AU SIO

WE ARE PROVIDERS
 
Back
Top Bottom