yuleyulenimewachokaa
Senior Member
- Nov 8, 2014
- 146
- 32
Huyu jamaa watu8 anazaana usiku na mchana, sijui anakula nini?
Kwa maisha gan unazaana ivyo
Last edited by a moderator:
Huyu jamaa watu8 anazaana usiku na mchana, sijui anakula nini?
Wacha weee kumbe hata miss bibi bomba ni mkubwa kwako
Kuna mahali humu ndani imeripotiwa kuwa Mbowe anadai aliibiwa kura katika uchaguzi uliopita. Wakati wengine tukitaka kuamini hivyo, yeye huyo huyo anaonyesha kukiri kuwa "aligaragazwa" na sasa kishaamka. Kukiri huku kuwa "aligaragazwa" nakuchukulia kuwa ni kukubali kuwa alishindwa kihalali!
Mbowe atamba kumng'oa Kikwete 2010,awataka wapinzani kuungana
Na Ally Sonda, Manyara
MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Freeman Mbowe, amesema chama chake kinajipanga vilivyo kuhakikisha kuwa mwaka 2010, Rais Jakaya Kikwete anangoka madarakani.
Mbowe ambaye yupo kwenye ziara ya Tumaini jipya, alisema hayo juzi Jumanne mbele ya umati wa watu waliofurika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mererani, wilayani Simanjro mkoani Manyara.
Alisema Rais Kikwete ajiandae kuiachia Ikulu mwaka huo kwa madai kuwa mbinu na mikakati iliyotumiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupata ushindi wa miujiza imefahamika na sasa Chadema inaifanyia kazi.
Mbowe ambaye mwaka jana aliwania urais kwa tiketi ya Chadema na kushindwa, alikiri mbele ya hadhara kuwa Rais Kikwete na CCM yake walimgalagaza kwa kura nyingi mwaka jana, lakini alisema yeye kama mwanaume ameishanyanyuka na kujikunguta.
Napenda nikiri mbele yenu wananchi wa Mererani kuwa Rais Kikwete na CCM yake walinigalagaza vibaya mwaka jana. Lakini mimi ni mwanaume, nimenyanyuka, nimejikunguta na sasa nina hasira ya kuwakomboa watanzania wanaonyanyasika ndani ya nchi yao, alisema Mbowe.
Alisema Serikali ya Kikwete ambayo wananchi wengi maskini walidhani itawakomboa kimaisha, bado inaendelea kukumbatia ubabe wa kila aina na sasa baadhi ya makamanda wa polisi wamefikia hatua ya kutangaza vita ndani ya nchi yenye Amiri Jeshi Mkuu, jambo ambalo ni la hatari.
Alitoa mfano wa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Manyara ambaye hivi karibuni alinukuliwa na gazeti moja la Kiswahili la kila siku (siyo Mwananchi) kwamba ameruhusu wawekezaji wa kigeni wa Kampuni ya Kuchimba Madini itumie silaha za moto kuwapiga wanaapolo.
Alidai kuwa hayo ni maagizo yanayostahili kulaaniwa na kumtaka Rais Kikwete na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali Saidi Mwema, kumfukuze kazi mara moja kamanda huyo, kama kweli alitoa kauli hiyo yenye lengo la kuhatarisha amani kwenye eneo lote la Miererani.
Alisema serikali ya Kikwete inaweza kuingia kwenye balaa kubwa la vurugu za wenyeji na wageni, hususan wawekezaji endapo itaendelea kuwakumbatia wageni hao na kuwanyanyasa wazalendo.
Mimi simtetei mchimbaji mdogo anayekwenda kuvamia wageni kwenye machimbo yao, bali ninachopinga ni serikali ya CCM kutoa raslimali zote muhimu kwa wawekezaji wageni na kuwaacha vijana wa kizalendo wakizurura hovyo, alisisitiza.
Mbowe, ametoa wito kwa vyama vyote vya upinzani nchini kuungana ili kupata ya nguvu ya kukingoa chama tawala madarakani.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara juzi uliofanyika katika viwanja vya NMC Unga Ltd uliohudhuriwa na mamia ya watu, Mbowe alisema bila vyama hivyo kuungana ni vigumu kushinda katika uchaguzi mkuu ujao.
Leo hii nimekuja hapa na ujumbe wa tumaini jipya, ni kweli tulishindwa katika uchaguzi uliopita kwa kuhujumiwa, lakini tumepata funzo hivyo lazima tuanze mikakati ya mwaka 2010 sasa na kuna umuhimu wapinzani wote kuungana ili kuwa nguvu kubwa, alisema Mbowe.
Mwenyekiti huyo alisema katika uchaguzi uliopita chama chake kilipatia kushinda wa viti 40 na kwa mujibu wa takwimu walizonazo kuna majimbo 10 walishinda lakini wasimamizi wa uchaguzi walitangaza washindi kuwa ni CCM.
Tulishinda kwenye majimbo mengi ikiwepo Ubungo, Hai na sehemu nyingine lakini kama ambavyo mlisikia jamaa wakajitangazia ushindi. Tulikaa tukaona haina haja ya kuendeleza mapambana, ila tusibiri uchaguzi ujao, alisema Mbowe.
Akizungumzia tatizo la rushwa na madawa ya kulevya, alisema Rais Jakaya Kikwete kamwe hawezi kuyamaliza kwani viongozi na marafiki wanaomzunguka ndio watuhumiwa wakubwa.
Mbowe alisema, Watanzania wengi na hata yeye awali walikuwa na matumaini makubwa na uongozi wa Rais Kikwete, lakini kadri siku zinavyoongezeka matumaini hayo yanatoweka.
Ningekuja hapa baada ya miezi mine mara baada ya kuchaguliwa Kikwete na ningemsema vibaya, nadhani mgenipiga mawe lakini leo hii naamani kuwa mnakubaliana na mimi kuwa mlijazwa upepo tu, nusra na mimi niingie mkenge, alisema Mbowe.
Hata hivyo, alisema kinachotakiwa kufanywa hivi sasa ni kuungana kwa watanzania wote wanaopenda mageuzi ya kweli, ili kuhakikisha kuwa wanaiondoa CCM na serikali yake madarakani katika uchaguzi wa 2010.
Kama nilivyosema awali, mikutano ninayofanya sasa ni ya matumaini mapya kwa watanzania, hivyo lazima tukae na kujifunza makosa yaliyopita ili tusiyarudie tena, alisema Mbowe.
Katika mkutano huo, Mbowe aliwaalika viongozi kadhaa wa vyama vya upinzani na wagombea wao wa ubunge, ambao pia walipewa nafasi ya kuwasalimia wananchi.