Familia ya Nyerere gizani

Familia ya Nyerere gizani

MAMA Maria Nyerere na familia yake hawakuhudhuria Sherehe ya Maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 17 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ilizofanyika Bariadi mkoani Simiyu jana.

Kumbukumbu hiyo hufanyika kila mwaka tangu Mwalimu Nyerere, Rais wa Kwanza wa Tanzania alipofariki tarehe 14 Oktoba 1999 alipokuwa kwenye matibabu nchini Uingereza.

Licha ya Anthony Mtaka, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kuarifu kwamba, Mama Maria Nyerere, mke wa mwalimu angehudhuria sherehe hizo, hakwenda.

Taarifa ya Mtaka aliyoitoa tarehe 5 Oktoba mwaka huu ilieleza kuwa, Mama Maria Nyerere pamoja na familia yake, wangefikia Nyamuata ambazo ni nyumba za Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Baadaye Mtaka alibadilisha makazi ya Mama Maria angefikia kwenye Hoteli ya Sumayi jambo ambalo lilithibitishwa na viongozi wasimamizi wa hoteli hiyo.

Pamoja na taarifa za Mtaka pia uthibitisho wa uongozi wa Sumayi kwamba, Mama Maria Nyerere angefikia kwenye hoteli hiyo kwa ajili ya kumbukumbu hiyo, hawakufika.

Familia ya Mwalim Nyerere imekuwa ikishiriki maadhimisho hayo ambayo ni ya kitaifa kwenye maeneo mbalimbali tangu kufariki kwa Mwalimu Nyerere.

Taarifa kutoka ndani ya familia ya Mwalimu Nyerere zinaeleza kutopata mwaliko wowote kutoka katika Serikali ya Rais John Magufuli ili kuhudhuria sherehe hizo.

Wakati serikali ikiendelea na maadhimisho yake mkoani Simiyu, familia ya Mwalumu Nyerere ilifanya ibada Maalumu katika Kanisa la Katoliki, Butiama.

Ibada hiyo ilihudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Sospiter Muhongo, Waziri wa Nishati na Madini na kwamba alimwakilisha Rais John Magufuli.

Wengine waliohudhuria ni Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini na Shyrose Bhanji Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (AELA).


Chanzo: Mwanahalisi
Kitendo cha kuchanganya siku ya kumkukumbuka baba wa taifa na kuzima mwenge ndipo serikali walipo kosea
Kwa mawazo yangu hii siku muhimu ya kumkumbuka baba wa taifa kuna mbinu chafu ya baadhi ya viongozi wanataka ifutike kabisa
Inakuwaje siku ya kuzima mwenge wabadilishe na iwe siku ya tarehe ya kifo cha baba wa taifa???????????
 
Nadhani Kwa utaratibu wa zamani alikuwa anatumiwa fedha lakini Kwa utawala huu No money


RC wa Simiyu aliandaa (hotel) mahali pa kufikia Mama Nyerere kwenye hayo maadhimisho, naamini kila kitu kililipiwa (booking)

Prof. Muhongo alishiriki ibada Butiama akimuwakilisha Rais, ikimaajisha kuwa shughuli ilipangwa kufanyika Butiama

Najiuliza kwanini serikali moja inaandaa shughuli mbili tofauti zenye dhumuni moja na kuwashirikisha wahusika walewale? Nini tafsiri ya haya yote
 
Hiyo ilikuwa sherehe ya kitaifa.. Sio ya kifamilia.. Inafaa wawepo ila sio lazima wawepo.. Sina uhakika nimesikia walifanya ibada ya kumkumbuka mwl kwao butiama na baadhi ya viongozi walikuwepo.. Hiyo inatosha kabisa.. Pia fahamuni mama maria amekuwa umli umekimbia mambo ya kusafir safir pia sio afya sana kwake.. Kama kabuli la baba wa taifa lipo butiama sasa kwanini mke wake na familia yake waje sehemu nyingine kufanya kumbukumbu? Ni muhimu familia ikiwa butiama na kupata baadhi ya viongozi butiama ili kuwafariji..tusilaumu kila kitu bhana.. Wacha serikali ibane matumizi kwanza next tym itakuwa boom

Umetumia akili sana kumjibu mtoa post. Mtoa post katoa kwa mihemuko ya kuukosa Uraisi 2015. Angefanya utafiti kidogo miaka mitatu ya nyuma iliyopita kama Mama Maria Nyerere alihudhuria maadhimisho hayo mikoani
 
swali,, Je serikali imeshasahau umuhimu wa familia ya nyerere hasa hasa mama malia nyerere?

Serikali bado inatambua umuhimu na kumuheshimu mama Maria na ndio maana bado inamtunza!! Sasa hivi mama Maria ni mtu wa makamo hivyo itakuwa busara zaidi kama atakuwa anasherehekea siku hii ya kumbukumbu ya mumewe huko huko nyumbani kwao Butiama badala ya kuhangaika na safari za huku na huko!!
 
Mwanahalisi waongo sana
Hivi mkuu wa mkoa anweza kutangaza ujio wa mama,na hoteli aliofikia ikatajwa halafu asitume mualiko?
Mama kwa sasa anasumbuliwa na utu uzima,kupanda ndege tabu,gari ndio kabisaa
Familia ya mwalimu ipewe heshima jamani,sio kusingiziwa tu kwa mgongo wa mpendwa wao ili kujipatia ujiko wa kisiasa
 
Mwacheni bibi wa watu apumzike jamani..khaaa! She is tired kwa kweli.

Hata hiyo familia ya Mwalimu wanaweza kumuenzi ndugu yao Mwalimu kwa ibada au kufanya shughuli za kijamii kuendeleza yale aliyoyapigania. Si lazima kwenda Simiyu kuzima Mwenge. Jamani lets be real! Tukiendekeza huu utaratibu..tutaishia wapi?
 
Mkuu Mwanahabari Huru, hili ni bandiko la uchonganishi ni sawa na uchochezi. Kualikwa kwa Mama Maria kulikuwa ni favour tuu, sasa hiyo favour unataka kuifanya ni right! .
Pasco
hii tafiti ya kuwa kila watz 10 wa 3 ni vichaa naona ina mashiko.uweke sherehe ya kifo cha mume mjane asihudhurie??tena bila taarifa??1.manyanya,2.muhongo,3.kigwangwala,4.nape5.ndalichako,6.tizeba,7.jafo,8.makamba,9majaliwa,10.polepole.toa wa 3
 
hii tafiti ya kuwa kila watz 10 wa 3 ni vichaa naona ina mashiko.uweke sherehe ya kifo cha mume mjane asihudhurie??tena bila taarifa??1.manyanya,2.muhongo,3.kigwangwala,4.nape5.ndalichako,6.tizeba,7.jafo,8.makamba,9majaliwa,10.polepole.toa wa 3
Sherehe ni ya kuzima mwenge ila wameiconcidisha na Nyerere Day. The right place kwa kumbukumbu ya Nyerere ni Kaburini kwake na misa takatifu. Mwenge ni tukio la Kitaifa na has nothing to do na Mama Maria. Kule katekwa kote was just a favour and not a right.
Pasco
 
Sherehe ni ya kuzima mwenge ila wameiconcidisha na Nyerere Day. The right place kwa kumbukumbu ya Nyerere ni Kaburini kwake na misa takatifu. Mwenge ni tukio la Kitaifa na has nothing to do na Mama Maria. Kule katekwa kote was just a favour and not a right.
Pasco
ok pasco.wape high TWAWEZA
 
JPM analeta mzaha sana kwenye mambo nyeti, hajui si kila theory inaaply katika siasa na anasahau kwamba nafasi aliyopo haitenganishwi na siasa.

Asiyeziba ufa .....
 
RC wa Simiyu aliandaa (hotel) mahali pa kufikia Mama Nyerere kwenye hayo maadhimisho, naamini kila kitu kililipiwa (booking)

Prof. Muhongo alishiriki ibada Butiama akimuwakilisha Rais, ikimaajisha kuwa shughuli ilipangwa kufanyika Butiama

Najiuliza kwanini serikali moja inaandaa shughuli mbili tofauti zenye dhumuni moja na kuwashirikisha wahusika walewale? Nini tafsiri ya haya yote
Well said mkuu.!!!
 
One of your problem is forgetting what you post. Go back to your post to understand why I made such a comment.
I did not forget anything. The comment was deliberately and was not meant for you or anybody specifically. I fail to understand why you were touched!?
 
Back
Top Bottom