Familia ya Nyerere gizani

Familia ya Nyerere gizani

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
MAMA Maria Nyerere na familia yake hawakuhudhuria Sherehe ya Maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 17 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ilizofanyika Bariadi mkoani Simiyu jana.

Kumbukumbu hiyo hufanyika kila mwaka tangu Mwalimu Nyerere, Rais wa Kwanza wa Tanzania alipofariki tarehe 14 Oktoba 1999 alipokuwa kwenye matibabu nchini Uingereza.

Licha ya Anthony Mtaka, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kuarifu kwamba, Mama Maria Nyerere, mke wa mwalimu angehudhuria sherehe hizo, hakwenda.

Taarifa ya Mtaka aliyoitoa tarehe 5 Oktoba mwaka huu ilieleza kuwa, Mama Maria Nyerere pamoja na familia yake, wangefikia Nyamuata ambazo ni nyumba za Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Baadaye Mtaka alibadilisha makazi ya Mama Maria angefikia kwenye Hoteli ya Sumayi jambo ambalo lilithibitishwa na viongozi wasimamizi wa hoteli hiyo.

Pamoja na taarifa za Mtaka pia uthibitisho wa uongozi wa Sumayi kwamba, Mama Maria Nyerere angefikia kwenye hoteli hiyo kwa ajili ya kumbukumbu hiyo, hawakufika.

Familia ya Mwalim Nyerere imekuwa ikishiriki maadhimisho hayo ambayo ni ya kitaifa kwenye maeneo mbalimbali tangu kufariki kwa Mwalimu Nyerere.

Taarifa kutoka ndani ya familia ya Mwalimu Nyerere zinaeleza kutopata mwaliko wowote kutoka katika Serikali ya Rais John Magufuli ili kuhudhuria sherehe hizo.

Wakati serikali ikiendelea na maadhimisho yake mkoani Simiyu, familia ya Mwalumu Nyerere ilifanya ibada Maalumu katika Kanisa la Katoliki, Butiama.

Ibada hiyo ilihudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Sospiter Muhongo, Waziri wa Nishati na Madini na kwamba alimwakilisha Rais John Magufuli.

Wengine waliohudhuria ni Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini na Shyrose Bhanji Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (AELA).

Chanzo: Mwanahalisi
 
MAMA Maria Nyerere na familia yake hawakuhudhuria Sherehe ya Maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 17 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ilizofanyika Bariadi mkoani Simiyu jana.

Kumbukumbu hiyo hufanyika kila mwaka tangu Mwalimu Nyerere, Rais wa Kwanza wa Tanzania alipofariki tarehe 14 Oktoba 1999 alipokuwa kwenye matibabu nchini Uingereza.

Licha ya Anthony Mtaka, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kuarifu kwamba, Mama Maria Nyerere, mke wa mwalimu angehudhuria sherehe hizo, hakwenda.

Taarifa ya Mtaka aliyoitoa tarehe 5 Oktoba mwaka huu ilieleza kuwa, Mama Maria Nyerere pamoja na familia yake, wangefikia Nyamuata ambazo ni nyumba za Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Baadaye Mtaka alibadilisha makazi ya Mama Maria angefikia kwenye Hoteli ya Sumayi jambo ambalo lilithibitishwa na viongozi wasimamiazi wa hoteli hiyo.

Pamoja na taarifa za Mtaka pia uthibitisho wa uongozi wa Sumayi kwamba, Mama Maria Nyerere angefikia kwenye hoteli hiyo kwa ajili ya kumbukumbu hiyo, hawakufika.

Familia ya Mwalim Nyerere imekuwa ikishiriki maadhimisho hayo ambayo ni ya kitaifa kwenye maeneo mbalimbali tangu kufariki kwa Mwalimu Nyerere.

Taarifa kutoka ndani ya familia ya Mwalimu Nyerere zinaeleza kutopata mwaliko wowote kutoka katika Serikali ya Rais John Magufuli ili kuhudhuria sherehe hizo.

Wakati serikali ikiendelea na maadhimisho yake mkoani Simiyu, familia ya Mwalumu Nyerere ilifanya ibada Maalumu katika Kanisa la Katoliki, Butiama.

Ibada hiyo ilihudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Sospiter Muhongo, Waziri wa Nishati na Madini na kwamba alimwakilisha Rais John Magufuli.

Wengine waliohudhuria ni Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini na Shyrose Bhanji Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (AELA).
Mkuu Mwanahabari Huru, hili ni bandiko la uchonganishi ni sawa na uchochezi. Kualikwa kwa Mama Maria kulikuwa ni favour tuu, sasa hiyo favour unataka kuifanya ni right! .
Pasco
 
Kuna wimbo naupenda sana unaitwa "Misuli ya Imani". Kwamba kuna watu hata wapate shida kubwa na adha imani yao kwa Mungu huwa haiteteleki, na hawa ndio Mungu huwatumia kumsutia shetani. Familia ya Nyerere ambayo naweza kudiriki kusema Mungu huitumia kuwasutia viongozi wanafiki na walafi.
Jana usiku nilikuwa naangalia kipindi TBC1, nilipomwona wifi(mke wa kaka yake) wa Mama Maria,, Mungu wangu,, nikatamani kuwaona mawifi wa wake wa Marais waliopita na wa sasa wa Afrika nzima. Baada ya kuona kipindi kile sikushangaa tena Wakatoliki kuanzisha mchakato wa kumtangaza Mtakatifu
 
sasa hii imezidi,yaani mzee nyerere kalipigania taifa halafu mambo haya yanatokea?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mkuu Mwanahabari Huru, hili ni bandiko la uchonganishi ni sawa na uchochezi. Kualikwa kwa Mama Maria kulikuwa ni favour tuu, sasa hiyo favour unataka kuifanya ni right! .
Pasco
Copy and past toka kwa mwanahalisi.
 
R.I.p Julius nyerere
Mungu atakulipa hukohuko mbinguni.
 
Mkuu Mwanahabari Huru, hili ni bandiko la uchonganishi ni sawa na uchochezi. Kualikwa kwa Mama Maria kulikuwa ni favour tuu, sasa hiyo favour unataka kuifanya ni right! .
Pasco
Sasa Pasco we unafikiri huyu jamaa zinamtosha kichwani kwake????????? We unafikiri Familia yake ataiendesha vipi asipo leta unafiki humu ndani??????HAKUNA MWANAJAMII FORUMU MUONGO KAMA HUYU JAMAAA........
 
Hiyo ilikuwa sherehe ya kitaifa.. Sio ya kifamilia.. Inafaa wawepo ila sio lazima wawepo.. Sina uhakika nimesikia walifanya ibada ya kumkumbuka mwl kwao butiama na baadhi ya viongozi walikuwepo.. Hiyo inatosha kabisa.. Pia fahamuni mama maria amekuwa umli umekimbia mambo ya kusafir safir pia sio afya sana kwake.. Kama kabuli la baba wa taifa lipo butiama sasa kwanini mke wake na familia yake waje sehemu nyingine kufanya kumbukumbu? Ni muhimu familia ikiwa butiama na kupata baadhi ya viongozi butiama ili kuwafariji..tusilaumu kila kitu bhana.. Wacha serikali ibane matumizi kwanza next tym itakuwa boom
 
Back
Top Bottom