Familia ya Lowassa yapelelezwa London kwa Utakatishaji fedha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Familia ya Lowassa yapelelezwa London kwa Utakatishaji fedha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ras, Dec 13, 2010.

 1. Ras

  Ras Senior Member

  #1
  Dec 13, 2010
  Joined: Mar 16, 2007
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MTOTO wa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa anayeitwa Frederick Lowassa anachunguzwa na Kitengo Maalumu cha Polisi wa Kimataifa wa Uingereza wanaofuatilia utata wa uhamishaji fedha kutoka Tanzania, Raia Mwema limedokezwa.

  Fedha hizo zinahusishwa na ununuzi wa nyumba yenye thamani ya pauni za Uingereza 475,000 (takriban Shilingi bilioni moja) katikati ya Jiji la London, .

  Hata hivyo, watu walio karibu na Frederick wameelezea kwamba kijana huyo hakuwahi kununua nyumba; bali aliwahi kutaka kupanga kwa ajili ya kuishi akiwa masomoni nchini Uingereza na fedha nyingine alizituma kwa ndugu yake aishie nchini humo.
  Nyumba ambayo inatajwa katika maelezo ya awali iko mtaa wa Leinster Gardens, jijini London.

  Hata hivyo, hakuna ofisa yeyote wa Serikali ya Tanzania aliyekuwa tayari kuzungumzia suala hilo, pamoja na kuwapo taarifa kwamba tayari vyombo vya dola vya Tanzania vimekwisha kuhusishwa katika uchunguzi huo.

  Maofisa wa Polisi wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (CID) wanaohusika na uchunguzi wa fedha haramu, wamekwepa kuzungumzia suala hilo na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Manumba, hakuweza kupatikana, na alielezwa kuwa nje ya nchi kikazi.

  Ofisa wa CID aliyeelezwa kuongoza kitengo kinachochunguza makosa ya uhalifu wa fedha na nyaraka, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Samson Kasala, alikanusha kufahamu chochote kuhusiana na suala hilo, kabla ya kukata simu alipohojiwa na Raia Mwema kuhusu taarifa hizo.

  Taarifa zinaeleza kwamba Kitengo cha Ufuatiliaji wa Fedha Haramu (Financial Intelligence Unit-FIU) kilichopo chini ya Wizara ya Fedha nchini, kilipokea taarifa kutoka Polisi wa Kimataifa wa London, Uingereza, wakitaka taarifa muhimu kuhusiana na Frederick, kabla ya kitengo hicho kuomba msaada wa polisi.

  Hata hivyo, Kamishna wa FIU, Herman Kessy, hakuweza kupatikana wiki iliyopita akielezwa kuwapo nchini Afrika Kusini kikazi, lakini hata aliporejea wiki hii Raia Mwema ilikosa ushirikiano kutoka kitengo hicho Jumatatu wiki hii.

  FIU imeanzishwa chini ya Sheria ya Udhibiti wa Fedha Haramu ya mwaka 2006 (Anti-Money Laundering Act-2006) kwa kuundiwa kanuni mwaka 2007, lakini hadi sasa kitengo hicho kimekuwa kikiendeshwa na maofisa watano tu, Kamishna Kessy, mchambuzi mmoja, mtaalamu wa mawasiliano na wasaidizi wawili wasio wataalamu, kitengo kilichopaswa kuendeshwa na watu wengi zaidi kutokana na unyeti wake.

  Habari zinaeleza kwamba hata ofisa wa Polisi aliyewahi kuhamishiwa FIU kwa kazi maalumu alijikuta akitengwa na kutopangiwa kazi na maofisa hao ambao wengi wanatoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), baada ya kuwa ‘wameaminiwa' sana na uongozi wa juu wa serikali.

  Kwa mujibu wa taarifa hizo ambazo bado zinafanyiwa kazi, Frederick ambaye baba yake alijiuzulu Waziri Mkuu kwa kuhusishwa na kashfa ya ununuzi wa mitambo ya kuzalisha umeme iliyokabidhiwa kwa kampuni tata ya Richmond Development LLC, anadaiwa kufanya mawasiliano kupitia kampuni ya uwakala iliyotajwa kwa jina la ‘Mishcon'.

  Nyaraka alizowasilisha, zilidai kuwapo ubia kati ya mtuhumiwa huyo na kampuni tatu ikiwamo Integrated Property Investment(T) Ltd na Barare Ltd Company.

  Mkataba huo unaonyesha kuwa Frederick Lowassa ana hisa kwenye kampuni hizo, na kwamba fedha za ununuzi wa nyumba hizo zinatokana na fedha za malipo ya hisa anazopata kutokana na kampuni hizo.

  Hata hivyo, mkataba huo unaonyesha kusainiwa Machi 25 mwaka 2009 siku moja baada ya Frederick Lowassa kusaini mkataba kati yake na kampuni ya Mishcon kama wakala wake katika ununuzi wa jengo hilo.

  Pia aliwasilisha nyaraka zinazoihusisha kampuni ya Alphatel kama moja ya kampuni ambayo pia yeye ni mkurugenzi wake ambayo pia ni chanzo chake kingine cha fedha anazotumia kununua jengo hilo.

  Taarifa zimedokeza kuwa ununuzi huo ulikwama baada ya kushindwa kutoa malipo hayo kwa mujibu wa mkataba kati yake na wakala wa ununuzi wa nyumba hiyo (kampuni ya Mishcon) ambao ulimtaka awe amekamilisha kulipa fedha hizo kabla ya Aprili 14, mwaka 2009.

  Hata hivyo, siku chache baadaye ndani ya mwezi huo wa Aprili, Frederick aliipelekea Mishcon kiasi cha pauni za Uingereza 199,940 zikitokea kwenye kampuni ya ununuzi fedha ya Wall Street Exchange.

  Aidha kiasi cha pauni 100,000 kiliingizwa kwenye akaunti ya kampuni hiyo hiyo ya Mishcon kwa fedha taslimu katika mikupuo 12 tofauti zikitokea kwenye matawi tofauti ya benki ya NatWest Bank plc iliyoko Kaskazini mwa Jiji la London.

  Raia Mwema limeelezwa kuwa mazingira ya kuingizwa fedha hizo kwenye akaunti ya wakala huyo (Mishcon) ndiyo yameifanya Taasisi ya SCD 6 Economics and Specialist Proceeds of Corruption Unit ya Uingereza inayosimamia uchunguzi wa sakata hilo kuwa na mashaka makubwa kuhusu uhalali wa fedha hizo.

  Kutokana na mazingira hayo, SCD 6 Economic and Specialist Crime Proceeds of Corruption Unit yenye ofisi zake Victoria Block, New Scotland Yard, London, ililazimika kuwasiliana na FIU ikitaka maelezo ya awali kuwezesha kufanyika kwa uchunguzi kuhusu fedha hizo.
  Raia Mwema iliwasiliana na Fred ambaye alikana kununua nyumba Uingereza lakini alikiri kuwahi kutuma fedha huko. Aliliambia Raia Mwema pia kwamba hajawahi kuhojiwa na yeyote kuhusu suala hilo, na pia kwamba hana taarifa kuwa polisi wa Uingereza wanampeleleza.

  Hata hivyo kwa upande mwingine, gazeti hili limebaini kuwa, maelezo ya awali ambayo yalitakiwa kutoka Tanzania na makachero hao wa Uingereza, ni pamoja na kutaka kufahamu kama kweli Frederick Edward Lowassa amezaliwa Agosti 26, 1977, Mwanza Tanzania na anamiliki hati ya kusafiria yenye namba AB 109402 iliyotolewa Tanzania na kwamba anwani yake nchini Uingereza ni 71 Hendrix Drive, Milton Keynes, MK8 0DY.

  Pia makachero hao waliitaka Serikali ya Tanzania kutoa ufafanuzi wakitaka kujua kama Frederick Lowassa ni mbia katika kampuni za Alphatel Partnership (Tanzania) Barare Ltd na Intergrated Tanzania Limited, kampuni ambazo zimefahamika kumilikiwa na familia ya Lowassa.

  Asasi hiyo ya Uingereza pia imeomba kujua kama FIU wana taarifa zozote za uhalifu dhidi ya Frederick Lowassa na kama baba yake Edward Lowassa anachunguzwa kwa tuhuma yoyote ya rushwa na mamlaka za uchunguzi wa rushwa nchini Tanzania kuhusu fedha haramu.

  Uchunguzi wa awali uliofanywa na vyombo vya dola, ulielezwa na taarifa hizo kwamba Frederick Lowassa si mbia katika kampuni hizo na kwamba Barare Ltd wenye hisa ni Edward Ngoyai Lowassa mwenye hisa 500 na Regina Mumba Lowassa mwenye hisa 500 huku wakurugenzi wakiwa ni hao hao.

  Ofisa wa Uingereza anayesimamia uchunguzi huo, George Simpson, ameliambia Raia Mwema kupitia barua pepe kwamba kanuni za uchunguzi kuhusiana na kesi zenye mguso wa kisiasa huwazuia kukanusha au kuthibitisha kuhusu uchunguzi unaoendelea hadi pale wanapofikia hatua ya kukamata mtuhumiwa ama anapofikishwa mahakamani.


  Source: Familia ya Lowassa yapelelezwa London
   
 2. C

  Chakulagani JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2014
  Joined: Jul 26, 2014
  Messages: 276
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Waziri Mkuu aliyejiuzulu Mheshimiwa Edward Lowassa muda huu amehojiwa na makachero wa TAKUKURU wakiongozana na makachero kutoka Uingereza wa kikosi cha Serious Fraud Office (SFO) kuhusiana na vyanzo vya fedha za ununuzi wa nyumba mbili anazomiliki Mheshimiwa Lowassa huko Uingereza.

  Itakumbukwa kwamba mwezi Novemba 2010, Rais Kikwete aliwekwa chini ya shinikizo kubwa kumrudisha Mhe Lowassa kwenye Baraza la Mawaziri.

  Hata hivyo, taarifa za umiliki wa nyumba hizi ambazo inasemekana zimenunuliwa kwa fedha chafu zilimfanya Rais Kikwete kuachana na fikra hizo.

  Itakumbukwa kwamba gazeti la Raia Mwema liliandika habari hii mwezi Novemba 2010 na kutoa picha ya nyumba hizo kwenye ukurasa wa mbele.

  Katika taarifa iliyotolewa jana na Afisa Mahusiano ya Umma wa SFO, Mr. Stewart Johnston, amekiri kuwepo kwa uchunguzi huo kwa kushirikiana na taasisi za Tanzania lakini akasema kwamba hawana utaratibu wa kutolea maelezo uchunguzi unaoendelea.

  Kwa mujibu wa taratibu za Uingereza, mmiliki wa nyumba anapaswa kuelezea chanzo cha mapato ya ununuzi wa nyumba pamoja na kodi ya nyumba inayolipwa kila mwaka.

  Inaaminika kwamba nyumba hizo zina thamani ya pauni milioni mbili na nusu au sawa na shilingi zaidi ya bilioni tano. Wadadisi wa mambo wanaamini kwamba chanzo cha fedha hizo ni malipo ya mkataba haramu wa ufisadi wa Richmond.

  Haijaweza kueleweka kwanini Mhe Lowassa ameamua kununua nyumba mbili Uingereza. Watu wa karibu wa Mhe Lowassa wanaamini kwamba ni maandalizi ya kuondoka nchini pale lengo lake la kutaka Urais litakapokwama.

  "Unajua Mzee kuna kipindi alikuwa amechoka kabisa na siasa za majitaka hapa nchini na alishaamua kuchukua familia yake na wajukuu na kujiondokea akaishi kwa amani na kula utajiri wake huko Uingereza", alikaririwa mmoja wa wapambe wake ambaye alikuwa ni Mbunge katika Bunge lililopita kutoka Kanda ya Ziwa.

  Ukichanganya na suala la afya yake inayozorota, historia ya kukataliwa na Mwalimu Nyerere, ufisadi wa Richmond, na maelewano madogo na viongozi wakuu wa Chama, uchunguzi huu mpya ni pigo la ziada kwa Mhe Lowassa katika harakati zake za kutafuta Urais wa Tanzania kwa mwaka 2015.
   
 3. yegowasu

  yegowasu Senior Member

  #3
  Sep 19, 2014
  Joined: Jun 29, 2014
  Messages: 141
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mhhh!! Ufisadi wa huyu Lowasa unatisha tuache utani. Hafai hafai kabisa. Kamateni wekeni ndani huyu jangiri hafaiiii!!
   
 4. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2014
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  kampuni ya hewa ya Richmond iliundwa nchini uingereza katika mji wa Birmingham
   
 5. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2014
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Sawa, hatua nzuri ya kuondoa uovu kwa mkono
   
 6. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #6
  Sep 19, 2014
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Ccm imara lazima ichuje makada wake kwenye vikao.tuwajue undani wao
   
 7. MoudyBoka

  MoudyBoka JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2014
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 842
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Fred Lowasa ndio alihojiwa miaka minne iliyopita,habari imeletwa leo ili kuzidisha machafuano ya uraisi uliokuwa urahisi na warahisi wa CCM!!!
   
 8. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #8
  Sep 19, 2014
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Labda siku upinzani wakimweka mgombea wao Tundu Lissu au Gagnija. Those are the only two I know that can deal with these thugs.
   
 9. k

  kasinge JF-Expert Member

  #9
  Sep 19, 2014
  Joined: May 22, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  LOWASA stop.
   
 10. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #10
  Sep 19, 2014
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Wakuu,

  Kimenuka!!!

  Waziri Mkuu aliyejiuzulu Mheshimiwa Edward Lowassa muda huu amehojiwa na makachero wa TAKUKURU wakiongozana na makachero kutoka Uingereza wa kikosi cha Serious Fraud Office (SFO) kuhusiana na vyanzo vya fedha za ununuzi wa nyumba mbili anazomiliki Mheshimiwa Lowassa huko Uingereza. Itakumbukwa kwamba mwezi Novemba 2010, Rais Kikwete aliwekwa chini ya shinikizo kubwa kumrudisha Mhe Lowassa kwenye Baraza la Mawaziri. Hata hivyo, taarifa za umiliki wa nyumba hizi ambazo inasemekana zimenunuliwa kwa fedha chafu zilimfanya Rais Kikwete kuachana na fikra hizo. Itakumbukwa kwamba gazeti la Raia Mwema liliandika habari hii mwezi Novemba 2010 na kutoa picha ya nyumba hizo kwenye ukurasa wa mbele.

  Katika taarifa iliyotolewa jana na Afisa Mahusiano ya Umma wa SFO, Mr. Stewart Johnston, amekiri kuwepo kwa uchunguzi huo kwa kushirikiana na taasisi za Tanzania lakini akasema kwamba hawana utaratibu wa kutolea maelezo uchunguzi unaoendelea.

  Kwa mujibu wa taratibu za Uingereza, mmiliki wa nyumba anapaswa kuelezea chanzo cha mapato ya ununuzi wa nyumba pamoja na kodi ya nyumba inayolipwa kila mwaka. Inaaminika kwamba nyumba hizo zina thamani ya pauni milioni mbili na nusu au sawa na shilingi zaidi ya bilioni tano. Wadadisi wa mambo wanaamini kwamba chanzo cha fedha hizo ni malipo ya mkataba haramu wa ufisadi wa Richmond.

  Haijaweza kueleweka kwanini Mhe Lowassa ameamua kununua nyumba mbili Uingereza. Watu wa karibu wa Mhe Lowassa wanaamini kwamba ni maandalizi ya kuondoka nchini pale lengo lake la kutaka Urais litakapokwama. "Unajua Mzee kuna kipindi alikuwa amechoka kabisa na siasa za majitaka hapa nchini na alishaamua kuchukua familia yake na wajukuu na kujiondokea akaishi kwa amani na kula utajiri wake huko Uingereza", alikaririwa mmoja wa wapambe wake ambaye alikuwa ni Mbunge katika Bunge lililopita kutoka Kanda ya Ziwa.

  Ukichanganya na suala la afya yake inayozorota, historia ya kukataliwa na Mwalimu Nyerere, ufisadi wa Richmond, na maelewano madogo na viongozi wakuu wa Chama, uchunguzi huu mpya ni pigo la ziada kwa Mhe Lowasa katika harakati zake za kutafuta Urais wa Tanzania kwa mwaka 2015.
   
 11. Nnangale

  Nnangale JF-Expert Member

  #11
  Sep 19, 2014
  Joined: Jul 20, 2013
  Messages: 1,240
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Anachosema nikwamba lile fisadi no1tz limehojiwa litoe maelezo liliko pata fedha zote hizo uk wanajua ni jizi pasco na wenzie wanalitetea hawana huruma na nchi hii,matumbo yao yameziba macho na ubongo.
   
 12. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #12
  Sep 19, 2014
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Naona mmeambiana kuandika hizi pumba mwenzako ameishakuwahi kuanzisha uzi kama huu.
   
 13. kadoda11

  kadoda11 JF-Expert Member

  #13
  Sep 19, 2014
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 16,314
  Likes Received: 8,417
  Trophy Points: 280
  vp kumekucha tayari?!
   
 14. Anthony Mtaka

  Anthony Mtaka Verified User

  #14
  Sep 19, 2014
  Joined: Jun 19, 2013
  Messages: 317
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  SIASA yataka Moyo Hasaa
   
 15. kbosho

  kbosho JF-Expert Member

  #15
  Sep 19, 2014
  Joined: Jun 4, 2012
  Messages: 12,505
  Likes Received: 3,314
  Trophy Points: 280
  billion 5?? guys hampo serious, billion tano ata mtoto wa Jk wa form four anazo sembuse Lowassa?
  ccm ni kichaka cha mafisadi, ila kwa sasa wana baguwana na kuchafuwana....thread imekaa kishabiki, kimbea,kizandiki,kinafiki,kimipasho...tunajuwa lowassa ana maadui wengi,lengo la thread hii ni kumchafuwa.Hakika ndani ya ccm hakuna anaweza kumnyooshea lowassa kidole..
   
 16. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #16
  Sep 20, 2014
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Vita kubwa Dhidi Ya Mh Lowassa Kwa Sasa Ni Baada Ya Kuonekana IPTL Na Escrow Account Kuwamaliza Watangaza Nia Wote Wengine Wa CCM:
  Katika Siku Za Karibuni Kumekuwa Na Vita Kubwa Kwenye Mitandao Ya Jamii Dhidi Ya Mhe Lowassa Haswa Baada Ya Kuonekana Report Ya Escrow Account Imewamaliza Watangaza Nia Karibu Wote Ndani Ya CCM. Report Ya Escrow Ambayo Tayari Imewasilishwa Kwa Mhe Rais Jakaya Kikwete Inasemekana Kuwataja Viongozi Ambayo Inaweza Kupelekea Mhe Rais Kuvunja Serikali, Jambo Ambalo Linajaribu Kuepukwa Kwa Kila Namna, Lakini Watu Waliotajwa Wengi Ni Wenye Nia Na Matarajio Kuwania Urais 2015, Na Inaonekana Kuzika Nafasi Zao Na Ndoto Zao Hizo, Haswa Baada Ya Wengi Wao Hao Hao Kushabikia Uongo Na Uzushi Wa Report Ya Richmond Iliyotumika Kwa Ustadi Mkubwa Kumushughulikia Lowassa.

  Wameanza Kujenga Uzushi Wa Kila Namna ili Kujaribu Kumchafua Mzee Lowassa, Ambaye Ameonekana Kuwa Kimya Na Kutii Onyo La Chama Chake CCM Na Kutoonekana Sehemu Yoyote.Hii Ni Kutaka Kuwaondoa Watanzania Kwenye Mjadala Wa Escorw Account.Pamoja Na Ukimya Wa Lowassa, Tendo La Gazeti La Mwanachi Kujumuika Naye Kwenye Jogging Ya Asubuhi Akiwa Dodoma Kwenye Bunge La Katiba, Limewafadhaisha Hawa Maadui Wengi Waliokuwa Wakipiga Debe Kuhusu Afya Yake , Na Baada Ya Hoja Hiyo Kufa, Sasa Wameleta Hoja Ya 2010 Iliyotoka Raiamwema Kwaajili Ya Vurugu Za Cabinet Wakati Huo. Bahati Mbaya Wanasahau Kuwa Watanzania Wameerevuka Siku Hizi, Habari Ya Uongo Ya 2010 Waliyoitumia Kumtishia Rais JK Dhidi Ya Mh Lowassa, Imefanywa Ni Habari Ya Leo. Mzee Lowassa Yupo Kijijini Monduli Kwenye Mikutano Ya Migogoro Ya Ardhi Na Hajawahi Kuhojiwa Na Mtu Yoyote Uingereza.
   
 17. Hornet

  Hornet JF-Expert Member

  #17
  Sep 20, 2014
  Joined: Apr 29, 2013
  Messages: 10,500
  Likes Received: 3,849
  Trophy Points: 280
  Naona mnapambana kwa nguvu kweli,
   
 18. Simiyu Yetu

  Simiyu Yetu JF-Expert Member

  #18
  Sep 20, 2014
  Joined: Apr 29, 2013
  Messages: 18,897
  Likes Received: 1,560
  Trophy Points: 280
  Kunahaja ya kujua ukweli siyo kubisha tu.
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Sep 20, 2014
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ni dalili tu ya jinsi vyombo vyetu sisi wenyewe vilivyo dhaifu.. think about it.
   
 20. kandukamo1

  kandukamo1 JF-Expert Member

  #20
  Sep 20, 2014
  Joined: Aug 21, 2012
  Messages: 938
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 60
  Siasa si ngumu bali UADILIFU ndio mgumu kwetu Waafrika. Yawezekana Lowasa si muadilifu kama wengi tunavyoaminishwa, lakini kuna watu si WAADILIFU zaidi ya Lowasa kuanzia ngazi ya familia hadi taifa.
   
Loading...