Familia ya Lowassa yapelelezwa London kwa Utakatishaji fedha

Ni dalili tu ya jinsi vyombo vyetu sisi wenyewe vilivyo dhaifu.. think about it.

Udhaifu ni asili yetu Waafrika, kumbuka suala LA ndege ya rais enzi za mkapa......maumivu ya udhaifu wetu ulitatuliwa Na wakubwa kwa kutuonea huruma juu ya udalali tuliopigwa na WADHAIFU WENYE MAMLAKA hadi walichelea kusema hata tukila NYASI ndege lazma inunuliwe, pamoja Na dharau hiyo tuliendelea kunyongea na UDHAIFU WETU.
 
Naona mnapambana kwa nguvu kweli,
You are right, magamba yanapambana na kukanyagana na 'kunyongana' ile mbaya.

Majuzi tu tuliisoma ile list ya vigogo ambao 'wamegawana' zile bilioni 200 za Escrow account, ambapo almost haikuacha mgombea yeyote, miongoni ya wagombea wa magamba waliotangaza nia ya kugombea urais, mwaka 2015, except jina la mzee wa mamvi ndilo pekee lililomiss kwenye hiyo list of shame!

Leo hii tunapewa 'Breaking News' kuwa mzee wa mamvi ahojiwa na kitengo cha SFO cha Uingereza, kuhusiana na kumshuku kuwa nyumba zake 2 zilizoko UK, kuhisiwa kuwa zimenunuliwa na 'vijisenti vichafu'

Hata hivyo imenenwa kuwa vita ya panzi furaha ya kunguru, na pia imenenwa waache wafu wajizike wenyewe!

Kutokana na hali hiyo, it is obvious that, there is no single presidential candidate, from CCM camp who is at least 10% clean!

Kwa maana hiyo jinsi 'mnyukano' huo wa wenyewe kwa wenyewe, unavyozidi kupamba moto, ndivyo ambavyo hao wagombea wa magamba, kwa kujua au kutokujua, wanavyozidi, kumsafishia njia UKAWA PRESIDENTIAL CANDIDATE kuelekea Magogoni in the year 2015!
 
Vita kubwa Dhidi Ya Mh Lowassa Kwa Sasa Ni Baada Ya Kuonekana IPTL Na Escrow Account Kuwamaliza Watangaza Nia Wote Wengine Wa CCM:
Katika Siku Za Karibuni Kumekuwa Na Vita Kubwa Kwenye Mitandao Ya Jamii Dhidi Ya Mhe Lowassa Haswa Baada Ya Kuonekana Report Ya Escrow Account Imewamaliza Watangaza Nia Karibu Wote Ndani Ya CCM. Report Ya Escrow Ambayo Tayari Imewasilishwa Kwa Mhe Rais Jakaya Kikwete Inasemekana Kuwataja Viongozi Ambayo Inaweza Kupelekea Mhe Rais Kuvunja Serikali, Jambo Ambalo Linajaribu Kuepukwa Kwa Kila Namna, Lakini Watu Waliotajwa Wengi Ni Wenye Nia Na Matarajio Kuwania Urais 2015, Na Inaonekana Kuzika Nafasi Zao Na Ndoto Zao Hizo, Haswa Baada Ya Wengi Wao Hao Hao Kushabikia Uongo Na Uzushi Wa Report Ya Richmond Iliyotumika Kwa Ustadi Mkubwa Kumushughulikia Lowassa.

Wameanza Kujenga Uzushi Wa Kila Namna ili Kujaribu Kumchafua Mzee Lowassa, Ambaye Ameonekana Kuwa Kimya Na Kutii Onyo La Chama Chake CCM Na Kutoonekana Sehemu Yoyote.Hii Ni Kutaka Kuwaondoa Watanzania Kwenye Mjadala Wa Escorw Account.Pamoja Na Ukimya Wa Lowassa, Tendo La Gazeti La Mwanachi Kujumuika Naye Kwenye Jogging Ya Asubuhi Akiwa Dodoma Kwenye Bunge La Katiba, Limewafadhaisha Hawa Maadui Wengi Waliokuwa Wakipiga Debe Kuhusu Afya Yake , Na Baada Ya Hoja Hiyo Kufa, Sasa Wameleta Hoja Ya 2010 Iliyotoka Raiamwema Kwaajili Ya Vurugu Za Cabinet Wakati Huo. Bahati Mbaya Wanasahau Kuwa Watanzania Wameerevuka Siku Hizi, Habari Ya Uongo Ya 2010 Waliyoitumia Kumtishia Rais JK Dhidi Ya Mh Lowassa, Imefanywa Ni Habari Ya Leo. Mzee Lowassa Yupo Kijijini Monduli Kwenye Mikutano Ya Migogoro Ya Ardhi Na Hajawahi Kuhojiwa Na Mtu Yoyote Uingereza.
Waacheni wafu wajizike wenyewe!
 
Siasa ngumu sana ila nadhani mzee atakuwa na tatizo kwenye uadilifu wake kazi ipo ngoja tusubiri moto.
Kumbe Simiyu yetu, haupo kambi ya mzee wa mamvi?

Pengine utakuwa upo kambi ya yule anayepigiwa debe na Prince, ambao wao wameona falsafa pekee ya kummaliza EL, ni kwa kujiapiza kuwa Rais ajaye kamwe hawezi kutoka kanda ya kaskazini!
 
Kwa maana hiyo jinsi 'mnyukano' huo wa wenyewe kwa wenyewe, unavyozidi kupamba moto, ndivyo ambavyo hao wagombea wa magamba, kwa kujua au kutokujua, wanavyozidi, kumsafishia njia UKAWA PRESIDENTIAL CANDIDATE kuelekea Magogoni in the year 2015!
Mkuu Fumbo, asante kwa hii, naunga mkono hoja, ila UKAWA, inakabiliwa na matatizo makuu mawili.
  1. Its only a "Marriage of convenience", wameungana kwa conveniences za Katiba, conveniences hizi zikiisha, ni kila mtu na lwake!.
  2. Hata wakiamua rasmi sasa washirikiane kiukweli kusimamisha mgombea mmoja, its still very unfortunately hawana mtu to march mgombea wa CCM, endapo CCM itaamua kumsimamisha yule "The One and Only!" best they have!. Kama ile kutangaza tuu "naianza safari!", kuta zote za siasa za 2015 zimetetemeka!, atakapoianza rasmi, who will dare stand on his way?!. By now we all know the best from CCM, haws UKAWA wan a nani hata wa kufikirika tuu na uwezo wa kuchagulika ili kuanzia sasa awe groomed?!. They have none!, no one!.

Thanks.

Pasco
 
Fred Lowasa hakuhojiwa hata kidogo. Kumbuka aliwaeleza wanahabari direct kuwa yeye siyo Mzee wake wanaendelea kumchafua. Wakiendelea kumzushia mambo ya uongo atawafikisha kwenye vyombo vya sheria. Fred ni kijana mdogo mtaratibu na anayeheshimu wakubwa Kwa wadogo.

Kinachoonekana hapa EL kawazidi kete sasa mnakuja na simulizi za uongo. Mkitaka kujua Lowassa anakubalika na watanzania wengi chagua nusu ya mikoa ya Tanzania randomly au nenda kama kwenye forum ya watu wa kawaida or panda daladala sikiliza mjadala wa urais 2015 utakapo anzishwa ndiyo mtajua kuwa mnapoteza muda wenu bure kumchafua Edward.
 
Fred Lowasa hakuhojiwa hata kidogo. Kumbuka aliwaeleza wanahabari direct kuwa yeye siyo Mzee wake wanaendelea kumchafua. Wakiendelea kumzushia mambo ya uongo atawafikisha kwenye vyombo vya sheria. Fred ni kijana mdogo mtaratibu na anayeheshimu wakubwa Kwa wadogo.

Kinachoonekana hapa EL kawazidi kete sasa mnakuja na simulizi za uongo. Mkitaka kujua Lowassa anakubalika na watanzania wengi chagua mikoa nusu ya mikoa ya Tanzania randomly kama kwenye kijiwe chochote kile au panda daladala sikiliza mjadala wa urais 2015 utakapo anzishwa ndiyo mtajua kuwa mnapoteza muda wenu bure kumchafua Edward.

Lowasa ni mwizi, acha tena ukome kutuambukiza ujinga.
 
Mkuu Fumbo, asante kwa hii, naunga mkono hoja, ila UKAWA, inakabiliwa na matatizo makuu mawili.
  1. Its only a "Marriage of convenience", wameungana kwa conveniences za Katiba, conveniences hizi zikiisha, ni kila mtu na lwake!.
  2. Hata wakiamua rasmi sasa washirikiane kiukweli kusimamisha mgombea mmoja, its still very unfortunately hawana mtu to march mgombea wa CCM, endapo CCM itaamua kumsimamisha yule "The One and Only!" best they have!. Kama ile kutangaza tuu "naianza safari!", kuta zote za siasa za 2015 zimetetemeka!, atakapoianza rasmi, who will dare stand on his way?!. By now we all know the best from CCM, haws UKAWA wan a nani hata wa kufikirika tuu na uwezo wa kuchagulika ili kuanzia sasa awe groomed?!. They have none!, no one!.

Thanks.

Pasco
Mkuu Pasco, nashukuru kwa mchango wako na nakubaliana nawe kwa your observation kuwa ukawa 'imeibuka' katika 'marriage of convenience' lakini ukumbuke pia shari yaweza kuzaa heri.

Ikumbukwe pia obstacle no 1 ambayo imekuwa ikiwakabili kambi ya upinzani,tokea mfumo wa vyama vingi urejeshwe tena nchini mwaka 1992, ni kwa wapinzani wa nchi hii, kila mtu kujiendea 'kivyake'

Iwapo safari hii huu umoja wa ukawa, wanaotuhubiria utakuwa unatoka ndani ya mioyo, basi ninaamini itakuwa wamepata 'ufunuo' toka juu mbinguni, na hiyo itakuwa step moja kubwa ya kusonga mbele.

Kuhusu suala la kuwa kwa sasa hawana Presidential Candidate, ambaye anaweza kuuzika, hilo naweza nisikuunge sana mkono, kwa kuwa najua kwenye politics, mtu anaweza kuibuka from nowhere na akapata publicity na popularity ya kupitiliza na akafanya 'miracles'

Let us wait and see.Time will tell.
 
Ngoja tuendelee na maandamano yetu, haya ya uchunguzi mwishowe hamna lolote la mana.
 
Lowassa alishatoka serikalini 7 miaka saba iliyopita kama ni mwizi mbona hamjafikisha mahakamani. Mimi nadhani political arithmetics tayari zimewashinda sasa kilichobaki kinywani kwenu ni uongo na matusi. Naomba tuvumiliane na tuombe hekima na busara itawale mijadala yetu kwani mwakani siyo mbali mwenyezi Mungu atupe heri 2015 siyo mbali sana. Tutajua mbivu na mbichi.
 
Back
Top Bottom