Familia ya Gwajima imemkosea Waziri wa Afya, kiungwana wamtafute wamuombe radhi

Moja ya watu ambao siwaelewi kwenye i serikari ukitoa presidaa ni uyo waziri
 
TRA itatusaidia kutambua credility ya Gwajima kama kiongozi wa kanisa; anatumia kanisa lake kutanganza hoja ambazo hana uwezo wa kuziprove- ukwerli wa kiongozi yeyote wa dini hupimwa kwa jinsi anavyotumia sadaka.

Kuhusu hoja chanjo tuawasikiliza madaktari na na wataalam wa wizara ya afya! Mpaka leo watoto wanapozaliwa Tanzani kuchanjwa BCG, mbaona hamjazuia BCG isidungwe kwa watoto hao wenye umri wa wiki moja tu wasio na uwezo wa kujimaulia wenyewe? Unafiki mtupu hu0.
Wakulaumiwa ni Dorothy, alituambia tutumie njia asilia kupambana na uviko
Tena akaongeza chanjo hazifai
Leo huyuhuyu Dorothy anatuswaga twende kwenye chanjo

Busara ingetumika Dorothy angebadilishwa wizara apelekwe wizara yeyote ili mtu mpya ambaye hakupinga chanjo aongoze kampeni
 
Tell her that she is walking at the edge of Thim,on top of that,her days are numbered,I have never seen a minister holding a special ministry like that one hence behaving like a minister of comedy
Hata nyie mmeanza kuraruana au comedy pia?
 
DRAMA NDIO TATIZO:
1."Wanaochanja wanatamka "NIMECHANJA",hawasumbuliwi.
2."Wasiochanja wakitamka "SITACHANJA",wanasumbuliwa.
3.Tamko la Serikali:"CHANJO NI HIARI"!!

Ukiangalia matamko namba 1-3,yote yameandikwa na yamesikika kwenye vyombo vya habari.
Kwa hiyo ni HIARI "kuchanja"au "kutochanja" !!!,elimu iendelee kutolewa.
Iendelee ila isiwe one sided,ubaya na uzuri wa chanjo vyote viwekwe wazi.Ilivyo sasa inaonyesha wazi kwamba chanjo si salama,kwa kuwa uzuri wa chanjo tu ndio unao zungumziwa.
 
Askofu gwajima huku akijua kwamba shemeji yake ndiye amepewa dhamana ya kusiamamia mambo ya chanjo. kiungwana tu hata kama hakubaliani na chanjo kwa kumheshimu shemeji yake angeweza kusema natumia hiari kutochanjwa basi akaishia hapo ili kuepusha migogoro ya kifamilia isiyokuwa ya lazima na pengine kumharibia shemeji yake kazi.

Lakini badala yake askofu gwajima amegeuza suala la chanjo kuwa mahubiri yake ya kila siku kanisani kwake huku akihamasisha na watu wengine kutochanjwa.

Si hivyo tu, pia kwenye mahubiri yake, askofu gwajima amekuwa akitumia mahubiri hayo kumshambulia shemeji yake na kuvuruga jitihada anazofanya kuhamasisha wananchi kuchanjwa chanjo ya UVIKO-19.

Kwa sababu ya busara ndogo ya askofu gwajima na kwa sababu ya kusaka umaarufu wa kisiasa amepelekea kuwepo kwa mzozo wa kifamilia na hata kuhatarisha ndoa ya mdogo wake.

Licha ya ndoa ya mdogo wake kuwa mashakani, pia anamharibia shemeji yake kwani mwitiko mdogo wa zoezi la chanjo unatokana na kauli zake anazozitoa akiwa madhabahuni.

Kwenye ibada ya leo, askofu gwajima ndio kaharibu kabisa kwani inaonyesha ameamua kumvunjia heshima na kumdhalilisha shemeji yake wazi wazi kwamba yeye kuolewa na mdogo wake ni hasara kwa familia yao na kwamba wamekuwa hawaelewani kwa sababu yake.

Mbaya zaidi mzee gwajima naye pamoja na uzee wake inaonyesha hana hekima wala busara kwa sababu alipaswa kuwa sehemu ya usuluhishi kwa kumshauri mwanaye 'askofu' kuacha kulumbana na shemeji yake hadharani lakini naye amezidi kukoleza moto kwa kumpa go ahead ya kumdhalilisha dorothy ambaye ni 'mwenga' wake.

Kwakweli kitendo kilichofanywa na askofu gwajima pamoja na mzee wake kumtweza Dorothy ni kitendo cha aibu na kiungwana wamtafute wamuombe radhi hili jambo walimalize kifamilia kwani msingi wa matatizo yote haya bila kupepesa macho ni Askofu Gwajima.
Samahani mkuu, UVIKO-19 ni kifupi cha nini? Japo najua ni corona-19, je uviko ni kifupi au ni neno la kiswahili?
 
Kama Dorothy asingemjibu na kumshambulia Askofu kwa maneno ya kuudhi (hata kama mengine ni kweli) bila shaka Askofu Rashid asingechomoa battery

Huna haja ya kumuonea huruma Dorothy. She is old enough to deal with whatever is thrown at her. Alijiingiza kwenye mabishano huku akijua nini kitafuata. Acha tu waonyeshane makali.

Askofu Rashid sio muumini wa “ukinitandika kofi shavu hili, nitageuza upige na huku”. Yeye ni mzee wa tit-for-tat, jino kwa jino.
Mwanaume anaposutana na mwanamke hadi kuita baba amsaidie ni dhaifu

gwajiboy ametuonyesha umama wa hali ya juu
 
Samahani mkuu, UVIKO-19 ni kifupi cha nini? Japo najua ni corona-19, je uviko ni kifupi au ni neno la kiswahili?
UVIKO-19 ni kifupisho cha maneno ya kiswahili

U-ugonjwa wa
VI- virusi vya
KO- korona
19 - mwaka ambao ugonjwa huo umegundulika
 
UVIKO-19 ni kifupisho cha maneno ya kiswahili

U-ugonjwa wa
VI- virusi vya
KO- korona
19 - mwaka ambao ugonjwa huo umegundulika
Asante sana mkuu, nilikuwa sijui kabisa, thanks a lot na ubarikiwe kwa elimu hii
 
Kwa hiyo mnataka kutuaminisha kuwa zile ngojera zake za jana jpili kanisani kwale ilikuwa ni mwendelezo wa fix zake.
 
Nilisema hapa wakati wa Uchaguzi kuwa "Askofu" Gwajima alikuwa ni mtu hasara sana kupewa ubunge. Kazi ya ubunge inahitaji mtu msikivu na mwenye busara siyo mtu tapeli kama Gwajima. Huyu inabidi TRA imchunguze kuhusu mapato na matumizi ya sadaka za kanisa lake, halafu sheria ichukue mkondo wake kwa kuanzia hapo.
Japo sikupendi lakini kumbe wakati mwingine huwa unakuwa timamu.
 
Inakuwa mbele hii movie marvel wangetoa hela nyingi Sana maana wote Hawa magwajisquare wote ni powerful kwavile ipo kwetu basi naomba Huu mpambano uwekewe ulinzi uwekewe jamani
 
Gwajima ni habari ya dunia labda wewe ndiyo hutaki ibada ya Leo waluifuatilia duniani ni 800k
Sasa anahubiri Nini dunia imsukilize? Kuhubiri Kuna sifa yake na kufitini au chokochoko Kuna sifa yake. Sielewe huko kanisani anachokifanya.
 
Japo sikupendi lakini kumbe wakati mwingine huwa unakuwa timamu.
Kama hunipendi mimi utapata tabu sana mwaka huu! Tandu watakuwa wanatembea usoni mwako wakati unapofumba macho kutaka kulala, na utakosa usingizi mwaka mzima! Afadhali ubadilishe mtazamo uwe mtu positive ambaye haendeshwi na hisia.
 
Huyo waluwalu wenu ndo aliyeanza kumuattack gajiboy.sasa tulieni ligi ifike mpaka mwisho.
 
Askofu gwajima huku akijua kwamba shemeji yake ndiye amepewa dhamana ya kusiamamia mambo ya chanjo. kiungwana tu hata kama hakubaliani na chanjo kwa kumheshimu shemeji yake angeweza kusema natumia hiari kutochanjwa basi akaishia hapo ili kuepusha migogoro ya kifamilia isiyokuwa ya lazima na pengine kumharibia shemeji yake kazi.

Lakini badala yake askofu gwajima amegeuza suala la chanjo kuwa mahubiri yake ya kila siku kanisani kwake huku akihamasisha na watu wengine kutochanjwa.

Si hivyo tu, pia kwenye mahubiri yake, askofu gwajima amekuwa akitumia mahubiri hayo kumshambulia shemeji yake na kuvuruga jitihada anazofanya kuhamasisha wananchi kuchanjwa chanjo ya UVIKO-19.

Kwa sababu ya busara ndogo ya askofu gwajima na kwa sababu ya kusaka umaarufu wa kisiasa amepelekea kuwepo kwa mzozo wa kifamilia na hata kuhatarisha ndoa ya mdogo wake.

Licha ya ndoa ya mdogo wake kuwa mashakani, pia anamharibia shemeji yake kwani mwitiko mdogo wa zoezi la chanjo unatokana na kauli zake anazozitoa akiwa madhabahuni.

Kwenye ibada ya leo, askofu gwajima ndio kaharibu kabisa kwani inaonyesha ameamua kumvunjia heshima na kumdhalilisha shemeji yake wazi wazi kwamba yeye kuolewa na mdogo wake ni hasara kwa familia yao na kwamba wamekuwa hawaelewani kwa sababu yake.

Mbaya zaidi mzee gwajima naye pamoja na uzee wake inaonyesha hana hekima wala busara kwa sababu alipaswa kuwa sehemu ya usuluhishi kwa kumshauri mwanaye 'askofu' kuacha kulumbana na shemeji yake hadharani lakini naye amezidi kukoleza moto kwa kumpa go ahead ya kumdhalilisha dorothy ambaye ni 'mwenga' wake.

Kwakweli kitendo kilichofanywa na askofu gwajima pamoja na mzee wake kumtweza Dorothy ni kitendo cha aibu na kiungwana wamtafute wamuombe radhi hili jambo walimalize kifamilia kwani msingi wa matatizo yote haya bila kupepesa macho ni Askofu Gwajima.

tuliwaambia kuishinda vita ya gwajiboy ni ngumu si unaona sasa mnaanza kuja kulia lia humu pambaneni na hali yenu
 
Back
Top Bottom