Familia ya Edward Lowassa imewastukia CHADEMA!

Familia ya Edward Lowassa imewastukia CHADEMA!

Mmeshasema Lowassa ni Fisadi, na amewakimbia mnafatafata wa nini? Kwanza wewe ndihe msemaji wake. Au ndio kuwashwa alikokusema Mwenyekiti wenu?
 
Watanzania karibia wote ni CHADEMA na chaguzi zote huwa anashinda ila huwa wanatangazwa wengine. Mfano mzuri ni buyungu. Hata wewe soon utaanza kumuunga Mbowe mkono


Mbowe hoyeeee!
Ninashukuru umetumia haki yako kifikra kujenga hoja pamoja na kwamba ulichokiandika ni njozi za mchana!
 
Mmeshasema Lowassa ni Fisadi, na amewakimbia mnafatafata wa nini? Kwanza wewe ndihe msemaji wake. Au ndio kuwashwa alikokusema Mwenyekiti wenu?
Mkuu;
Nimeambiwa waliosema Lowassa ni fisadi hawa hapa,

DWytHSCX0AAQdrX.jpg
 
Ila sababu unajulikana kwamba wewe upo lumumba na unalipwa elfu saba kwa kila post hatuna budi kuwapuuza hivi lizaboni kaenda wapi maana changamsha genge umebaki wewe tu aisee
 
Ila sababu unajulikana kwamba wewe upo lumumba na unalipwa elfu saba kwa kila post hatuna budi kuwapuuza hivi lizaboni kaenda wapi maana changamsha genge umebaki wewe tu aisee
Mkuu;
Ninachofurahi ni kuwa unafuatilia mada zangu!

Kusoma na kujibu mada zangu sio kupuuza kama unavyodhani. Nadhani hujui maana ya kupuuza.

Karibu sana na endelea kuwa mfuasi wangu katika mada zangu!
 
Ndio maana kule bunyungu wakatelekeza mgombeaaaaa duh kumbe iko hivi ruzuku anakula peke yake!
Mkuu;
Mbowe hawezi kuweka pesa yake sehemu ambayo anafahamu atapoteza.

Mbowe ni mfanyabiashara mzuri!
 
Kuna methali inayosema, Mja hakosei mara moja, kurudia ndio kosa.

Hii ina maana kuwa mtu anaweza akafanya kosa mara ya kwanza. Hiyo si hoja. Lakini akirudia kosa lile lile, basi hapo amekusudia na anafaa kuadhibiwa au kulaumiwa.

Familia ya Edward Lowassa amekataa kurudia kosa mara ya pili baada ya kukataa kuwa chanzo cha mapato kwa baadhi ya viongozi wa CHADEMA mkoani Arusha.

Kabla hata ya kuongea na kukubaliana na familia ya Lowassa, baadhi ya viongozi wa CHADEMA katika Mkoa wa Arusha wakiongozwa na Diwani wa CHADEMA katika Kata ya Sombetini, Ally Bananga na Godbless Lema waliamua kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kuwa mgombea wa Ubunge katika Jimbo la Monduli na kuzipeleka nyumbani kwa Fred Lowassa wakishinikiza azijaze na watazirudisha.

Baada ya kutumia muda mwingi wakimshawishi akubali maombi yao, Fred aliwaambia wamuache kwanza atafakari kwa kina kabla ya kutoa uamuzi wa mwisho.

Majibu ya Fred yaliwapa moyo kiasi kwamba wakaanza kutangaza kwenye mitandao mbalimbali kuwa wanapeleka mgombea katika Jimbo la Monduli ambaye ni ‘’machine’’ na kwa sababu hiyo, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo aanze kutafuta kazi nyingine.

Habari za Fred kupelekewa fomu zilipomfikia Mama yake, Regina Lowassa aliagiza na kusema hizo fomu zilirudishwe mara moja kwa wahusika kwa sababu familia haina tena pesa za kuchezea hovyo hovyo. ‘’Tumetumia pesa nyingi wakati wa Uchaguzi Mkuu bila mafanikio, hatuwezi kuendelea kuwa shamba la kutajirisha viongozi wa CHADEMA’’ Mama Lowassa alisikika akisema.

Habari hizi ziliwafikia viongozi wa CHADEMA ambao waliamua kwenda kuonana na Edward Lowassa ili amshawishi mwanaye. Lowassa aliwaambia Fred ni mtu mzima na hawezi kumpangia nini akifanye au kuamua hatma ya maisha yake kwa sasa.

Majibu ya Lowassa yaliwafanya viongozi wa CHADEMA kuanza kusaka mgombea mwingine.

Habari zinaeleza kuwa kwa sasa familia ya Lowassa ameanza kujiweka mbali na harakati za CHADEMA ndio maana kwa sasa huwezi kumuona Mke wa Lowassa katika shughuri za Balaza la wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) kama ilivyokuwa hapo zamani.

Kuna msuguano mkali kati ya familia ya Lowassa na wapambe wa Lowassa kama Khamis Mgeja na Sheikh Rajab Katimba ambapo familia yake inamtaka aachane na siasa huku wapambe wakimshawishi kuwa ana nafasi tena ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania mwaka 2020 ili waendelee kunufaika kifedha na uwepo wake katika siasa.
Leo mmeanza kumshabikia lowassa tena!
 
‘’Tumetumia pesa nyingi wakati wa Uchaguzi Mkuu bila mafanikio, hatuwezi kuendelea kuwa shamba la kutajirisha viongozi wa CHADEMA’’ Mama Lowassa alisikika akisema.
doh😀😀😀😛😛😛
 
Mleta Uzi ushawahi finywa na maza wako mapajani mbele za watu halafu anakutolea macho usilie.
 
Back
Top Bottom