Familia ya Edward Lowassa imewastukia CHADEMA!

Familia ya Edward Lowassa imewastukia CHADEMA!

Chadema walipokaa na familia ili mzee Lowassa ahamie Ukawa Mama alikataa,

Mama alijua uwanja ambao mzee anapelekwa ni uwanja wa fisi tofauti na ilivyokuwa katika uwanja wa CCM ambao alikuwa wanauelewa vyema.

Matokeo yake Mzee Lowassa akafanya ATM na wahuni mbalimbali kumkomba mzee kila alichokuwa nacho.
Nimeanza kuelewa vizuri kwa nini Mama Lowassa hataki kujiingiza tena kwenye siasa za CHADEMA!
 
..binafsi nimefurahi Fred Lowassa kujitoa.

..naiona cdm kama chama cha wanaharakati, na sidhani kama Fred ataweza kuendana na siasa za chama.

..pia nitafurahi kama Lowassa atastaafu siasa.

..kwanza, I was not inspired na jinsi alivyofanya kampeni zake za Uraisi.

..pili, amedhoofika mno. Ni vizuri akapumzika sasa na aangalie zaidi afya yake.
Mkuu;
Huu ushauri wako watu kama Khamis Mgeja na Sheikh Rajab Katimba hawawezi kukuelewa hata kidogo!
 
Kuna methali inayosema, Mja hakosei mara moja, kurudia ndio kosa.

Hii ina maana kuwa mtu anaweza akafanya kosa mara ya kwanza. Hiyo si hoja. Lakini akirudia kosa lile lile, basi hapo amekusudia na anafaa kuadhibiwa au kulaumiwa.

Familia ya Edward Lowassa amekataa kurudia kosa mara ya pili baada ya kukataa kuwa chanzo cha mapato kwa baadhi ya viongozi wa CHADEMA mkoani Arusha.

Kabla hata ya kuongea na kukubaliana na familia ya Lowassa, baadhi ya viongozi wa CHADEMA katika Mkoa wa Arusha wakiongozwa na Diwani wa CHADEMA katika Kata ya Sombetini, Ally Bananga na Godbless Lema waliamua kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kuwa mgombea wa Ubunge katika Jimbo la Monduli na kuzipeleka nyumbani kwa Fred Lowassa wakishinikiza azijaze na watazirudisha.

Baada ya kutumia muda mwingi wakimshawishi akubali maombi yao, Fred aliwaambia wamuache kwanza atafakari kwa kina kabla ya kutoa uamuzi wa mwisho.

Majibu ya Fred yaliwapa moyo kiasi kwamba wakaanza kutangaza kwenye mitandao mbalimbali kuwa wanapeleka mgombea katika Jimbo la Monduli ambaye ni ‘’machine’’ na kwa sababu hiyo, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo aanze kutafuta kazi nyingine.

Habari za Fred kupelekewa fomu zilipomfikia Mama yake, Regina Lowassa aliagiza na kusema hizo fomu zilirudishwe mara moja kwa wahusika kwa sababu familia haina tena pesa za kuchezea hovyo hovyo. ‘’Tumetumia pesa nyingi wakati wa Uchaguzi Mkuu bila mafanikio, hatuwezi kuendelea kuwa shamba la kutajirisha viongozi wa CHADEMA’’ Mama Lowassa alisikika akisema.

Habari hizi ziliwafikia viongozi wa CHADEMA ambao waliamua kwenda kuonana na Edward Lowassa ili amshawishi mwanaye. Lowassa aliwaambia Fred ni mtu mzima na hawezi kumpangia nini akifanye au kuamua hatma ya maisha yake kwa sasa.

Majibu ya Lowassa yaliwafanya viongozi wa CHADEMA kuanza kusaka mgombea mwingine.

Habari zinaeleza kuwa kwa sasa familia ya Lowassa ameanza kujiweka mbali na harakati za CHADEMA ndio maana kwa sasa huwezi kumuona Mke wa Lowassa katika shughuri za Balaza la wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) kama ilivyokuwa hapo zamani.

Kuna msuguano mkali kati ya familia ya Lowassa na wapambe wa Lowassa kama Khamis Mgeja na Sheikh Rajab Katimba ambapo familia yake inamtaka aachane na siasa huku wapambe wakimshawishi kuwa ana nafasi tena ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania mwaka 2020 ili waendelee kunufaika kifedha na uwepo wake katika siasa.
Mjinga ni Mjinga tu, na MACCM wakuu wanapenda watu wenye akili hizi.
 
Nimeanza kuelewa vizuri kwa nini Mama Lowassa hataki kujiingiza tena kwenye siasa za CHADEMA!
Mzee alikuwa halali usiku simu inapigwa M-pesa zinatumwa mikakati ya kumtapeli mzee ilikuwa full speed,Mama alikuwa akishuhudia kadhia yote hiyo.
 
Mkuu;
Huu ushauri wako watu kama Khamis Mgeja na Sheikh Rajab Katimba hawawezi kukuelewa hata kidogo!

..Lowassa anaweza kubakia kwenye chama kama mzee mstaafu na mshauri.

..lakini kuwa mgombea nadhani ni kutomtendea haki, na kutokitendea haki chama.

..hata Shekhe Katimba na Mzee Mgeja nao wanatakiwa wabakie ktk nafasi za ushauri.
 
Yaani hawa ng'ombe wasiotoa maziwa wakiungana na wale waliowanunua bila mikia wanafanana kila kitu.
 
huyu MsemajiUkweli ni masikini wa akili anayetumika mithili ya mashine ya kubangua korosho , Lowassa alishaondoka ccm akawashinda kwenye urais kwa tofauti ya zaidi kura mil 6 , wakampora lakini bado wanajipendekeza .
Alishinda Urais wa mitandao ya kijamii lkn aliyeshinda Urais wa Tanzania no John Pombe Mgufuli
 
..Lowassa anaweza kubakia kwenye chama kama mzee mstaafu na mshauri.

..lakini kuwa mgombea nadhani ni kutomtendea haki, na kutokitendea haki chama.

..hata Shekhe Katimba na Mzee Mgeja nao wanatakiwa wabakie ktk nafasi za ushauri.
Hoja zako zina mashiko lakini nani wa kumfunga paka kengele ndani ya CHADEMA?
 
Mkuu;
Careful, usije ukajikuta uko nyuma yake peke yako!

Nadhani unajifunza kuwajua wanasiasa wa Tanzania hasa wa upinzani!
Watanzania karibia wote ni CHADEMA na chaguzi zote huwa anashinda ila huwa wanatangazwa wengine. Mfano mzuri ni buyungu. Hata wewe soon utaanza kumuunga Mbowe mkono


Mbowe hoyeeee!
 
Back
Top Bottom