Familia ya Edward Lowassa imewastukia CHADEMA!

Familia ya Edward Lowassa imewastukia CHADEMA!

We ni Ashkimajinun!
Wakati hayo yanafanyika ya CHADEMA na familia ya Lowassa, ulikuwapo?

Una washwa bila shaka.
 
tukiacha uchafu ukitamba wananchi watapotoshwa .
Ndio maana nimeandika kuwa wewe ni zaidi ya masikini wa akili.

Nani amekupa mamlaka ya kuelimisha wananchi wakati hapa uwezo huo huna? Jisemee nafsi yako, acha kujivika mwamvuli wa fikra za wanancho wote.
 
Kwani kati ya Lowassa na CHADEMA nani alitegemea kunufaika? Lowassa yeye baada ya kupigwa panga kule kizota akajua ndio mwisho wake akatafuta mahali pa kujibanza. Ndio akaibukia CHADEMA. pamoja na mapungufu yake tulimkubali sababu kulikuwa hamna namna tena maana adui yetu ni CCM, na viongozi wetu washatuletea tungefanyaje. Kwa taarifa yako tu hata tungeletewa mtu kama le mutuz tungemkubali tu.

Kwa hiyo yeye ndio alikuwa mnufaika na si chadema kama unavyodai wewe mzigo mleta mada unayeendesha maisha kwa umbea nakupewa 7000. Njaa mbaya
 
Historia ya Tanzania inabaisha tulikuwa na NCCR-Mageuzi, tukapata CUF na sasa tuna CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani.

Historia hiyo hiyo itaihukumu CHADEMA kama ilivyoihukumu NCCR-Mageuzi na CUF.

Usiwe na wasi wasi kwa sababu wenye CHADEMA wanatuambia walianza na mungu na watamaliza na mungu!
Wewe unadhani ukaribu wa Zitto na CHADEMA ni nini, watakapoanza kuparurana ACT watakuwa kama KUNGURU wanaokota mizoga kilaaaini!
 
Chadema walipokaa na familia ili mzee Lowassa ahamie Ukawa Mama alikataa,

Mama alijua uwanja ambao mzee anapelekwa ni uwanja wa fisi, tofauti na ilivyokuwa katika uwanja wa CCM ambao alikuwa wanauelewa vyema.

Matokeo yake Mzee Lowassa akafanywa ATM na wahuni mbalimbali, kumkomba mzee kila alichokuwa nacho.
 
..binafsi nimefurahi Fred Lowassa kujitoa.

..naiona cdm kama chama cha wanaharakati, na sidhani kama Fred ataweza kuendana na siasa za chama.

..pia nitafurahi kama Lowassa atastaafu siasa.

..kwanza, I was not inspired na jinsi alivyofanya kampeni zake za Uraisi.

..pili, amedhoofika mno. Ni vizuri akapumzika sasa na aangalie zaidi afya yake.
 
Kuna methali inayosema, Mja hakosei mara moja, kurudia ndio kosa.

Hii ina maana kuwa mtu anaweza akafanya kosa mara ya kwanza. Hiyo si hoja. Lakini akirudia kosa lile lile, basi hapo amekusudia na anafaa kuadhibiwa au kulaumiwa.

Familia ya Edward Lowassa amekataa kurudia kosa mara ya pili baada ya kukataa kuwa chanzo cha mapato kwa baadhi ya viongozi wa CHADEMA mkoani Arusha.

Kabla hata ya kuongea na kukubaliana na familia ya Lowassa, baadhi ya viongozi wa CHADEMA katika Mkoa wa Arusha wakiongozwa na Diwani wa CHADEMA katika Kata ya Sombetini, Ally Bananga na Godbless Lema waliamua kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kuwa mgombea wa Ubunge katika Jimbo la Monduli na kuzipeleka nyumbani kwa Fred Lowassa wakishinikiza azijaze na watazirudisha.

Baada ya kutumia muda mwingi wakimshawishi akubali maombi yao, Fred aliwaambia wamuache kwanza atafakari kwa kina kabla ya kutoa uamuzi wa mwisho.

Majibu ya Fred yaliwapa moyo kiasi kwamba wakaanza kutangaza kwenye mitandao mbalimbali kuwa wanapeleka mgombea katika Jimbo la Monduli ambaye ni ‘’machine’’ na kwa sababu hiyo, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo aanze kutafuta kazi nyingine.

Habari za Fred kupelekewa fomu zilipomfikia Mama yake, Regina Lowassa aliagiza na kusema hizo fomu zilirudishwe mara moja kwa wahusika kwa sababu familia haina tena pesa za kuchezea hovyo hovyo. ‘’Tumetumia pesa nyingi wakati wa Uchaguzi Mkuu bila mafanikio, hatuwezi kuendelea kuwa shamba la kutajirisha viongozi wa CHADEMA’’ Mama Lowassa alisikika akisema.

Habari hizi ziliwafikia viongozi wa CHADEMA ambao waliamua kwenda kuonana na Edward Lowassa ili amshawishi mwanaye. Lowassa aliwaambia Fred ni mtu mzima na hawezi kumpangia nini akifanye au kuamua hatma ya maisha yake kwa sasa.

Majibu ya Lowassa yaliwafanya viongozi wa CHADEMA kuanza kusaka mgombea mwingine.

Habari zinaeleza kuwa kwa sasa familia ya Lowassa ameanza kujiweka mbali na harakati za CHADEMA ndio maana kwa sasa huwezi kumuona Mke wa Lowassa katika shughuri za Balaza la wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) kama ilivyokuwa hapo zamani.

Kuna msuguano mkali kati ya familia ya Lowassa na wapambe wa Lowassa kama Khamis Mgeja na Sheikh Rajab Katimba ambapo familia yake inamtaka aachane na siasa huku wapambe wakimshawishi kuwa ana nafasi tena ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania mwaka 2020 ili waendelee kunufaika kifedha na uwepo wake katika siasa.

Wewe bora uolewe tu
 
Kwani kati ya Lowassa na CHADEMA nani alitegemea kunufaika? Lowassa yeye baada ya kupigwa panga kule kizota akajua ndio mwisho wake akatafuta mahali pa kujibanza. Ndio akaibukia CHADEMA. pamoja na mapungufu yake tulimkubali sababu kulikuwa hamna namna tena maana adui yetu ni CCM, na viongozi wetu washatuletea tungefanyaje. Kwa taarifa yako tu hata tungeletewa mtu kama le mutuz tungemkubali tu.

Kwa hiyo yeye ndio alikuwa mnufaika na si chadema kama unavyodai wewe mzigo mleta mada unayeendesha maisha kwa umbea nakupewa 7000. Njaa mbaya
Mkuu;
Maelezo marefu lakini hayana hoja ya msingi!

Soma kwa makini mada yangu na uelewe vizuri.

Ulichofanya hakina tofauti na mtu kujitungia mtihani na kujibu yeye mwenyewe nje ya mtihani halisi!
 
Wewe unadhani ukaribu wa Zitto na CHADEMA ni nini, watakapoanza kuparurana ACT watakuwa kama KUNGURU wanaokota mizoga kilaaaini!
Mkuu;
Funguka zaidi ili nikuelewe vizuri!

Hoja yako imeniacha njia panda!
 
Kwani kati ya Lowassa na CHADEMA nani alitegemea kunufaika? Lowassa yeye baada ya kupigwa panga kule kizota akajua ndio mwisho wake akatafuta mahali pa kujibanza. Ndio akaibukia CHADEMA. pamoja na mapungufu yake tulimkubali sababu kulikuwa hamna namna tena maana adui yetu ni CCM, na viongozi wetu washatuletea tungefanyaje. Kwa taarifa yako tu hata tungeletewa mtu kama le mutuz tungemkubali tu.

Kwa hiyo yeye ndio alikuwa mnufaika na si chadema kama unavyodai wewe mzigo mleta mada unayeendesha maisha kwa umbea nakupewa 7000. Njaa mbaya
2020 tutawaletea mwingine
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom