Familia ya Edward Lowassa imewastukia CHADEMA!

Familia ya Edward Lowassa imewastukia CHADEMA!

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,185
Reaction score
24,055
Kuna methali inayosema, Mja hakosei mara moja, kurudia ndio kosa.

Hii ina maana kuwa mtu anaweza akafanya kosa mara ya kwanza. Hiyo si hoja. Lakini akirudia kosa lile lile, basi hapo amekusudia na anafaa kuadhibiwa au kulaumiwa.

Familia ya Edward Lowassa amekataa kurudia kosa mara ya pili baada ya kukataa kuwa chanzo cha mapato kwa baadhi ya viongozi wa CHADEMA mkoani Arusha.

Kabla hata ya kuongea na kukubaliana na familia ya Lowassa, baadhi ya viongozi wa CHADEMA katika Mkoa wa Arusha wakiongozwa na Diwani wa CHADEMA katika Kata ya Sombetini, Ally Bananga na Godbless Lema waliamua kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kuwa mgombea wa Ubunge katika Jimbo la Monduli na kuzipeleka nyumbani kwa Fred Lowassa wakishinikiza azijaze na watazirudisha.

Baada ya kutumia muda mwingi wakimshawishi akubali maombi yao, Fred aliwaambia wamuache kwanza atafakari kwa kina kabla ya kutoa uamuzi wa mwisho.

Majibu ya Fred yaliwapa moyo kiasi kwamba wakaanza kutangaza kwenye mitandao mbalimbali kuwa wanapeleka mgombea katika Jimbo la Monduli ambaye ni ‘’machine’’ na kwa sababu hiyo, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo aanze kutafuta kazi nyingine.

Habari za Fred kupelekewa fomu zilipomfikia Mama yake, Regina Lowassa aliagiza na kusema hizo fomu zilirudishwe mara moja kwa wahusika kwa sababu familia haina tena pesa za kuchezea hovyo hovyo. ‘’Tumetumia pesa nyingi wakati wa Uchaguzi Mkuu bila mafanikio, hatuwezi kuendelea kuwa shamba la kutajirisha viongozi wa CHADEMA’’ Mama Lowassa alisikika akisema.

Habari hizi ziliwafikia viongozi wa CHADEMA ambao waliamua kwenda kuonana na Edward Lowassa ili amshawishi mwanaye. Lowassa aliwaambia Fred ni mtu mzima na hawezi kumpangia nini akifanye au kuamua hatma ya maisha yake kwa sasa.

Majibu ya Lowassa yaliwafanya viongozi wa CHADEMA kuanza kusaka mgombea mwingine.

Habari zinaeleza kuwa kwa sasa familia ya Lowassa ameanza kujiweka mbali na harakati za CHADEMA ndio maana kwa sasa huwezi kumuona Mke wa Lowassa katika shughuri za Balaza la wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) kama ilivyokuwa hapo zamani.

Kuna msuguano mkali kati ya familia ya Lowassa na wapambe wa Lowassa kama Khamis Mgeja na Sheikh Rajab Katimba ambapo familia yake inamtaka aachane na siasa huku wapambe wakimshawishi kuwa ana nafasi tena ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania mwaka 2020 ili waendelee kunufaika kifedha na uwepo wake katika siasa.
 
lowassa keshasema msimlishe maneno ya uongo lakini hamsikii. haya kapokee hiyo buku 7 hapo lumumba
huyu MsemajiUkweli ni masikini wa akili anayetumika mithili ya mashine ya kubangua korosho , Lowassa alishaondoka ccm akawashinda kwenye urais kwa tofauti ya zaidi kura mil 6 , wakampora lakini bado wanajipendekeza .
 
huyu MsemajiUkweli ni masikini wa akili anayetumika mithili ya mashine ya kubangua korosho , Lowassa alishaondoka ccm akawashinda kwenye urais kwa tofauti ya zaidi kura mil 6 , wakampora lakini bado wanajipendekeza .
Unakodoa macho, kusoma na kujibu andiko la mtu unayefahamu ni masikini wa akili! Basi wewe utakuwa ni zaidi ya masikini wa akili.
 
...Habari za Fred kupelekewa fomu zilipomfikia Mama yake, Regina Lowassa aliagiza na kusema hizo fomu zilirudishwe mara moja kwa wahusika kwa sababu familia haina tena pesa za kuchezea hovyo hovyo. ‘’Tumetumia pesa nyingi wakati wa Uchaguzi Mkuu bila mafanikio, hatuwezi kuendelea kuwa shamba la kutajirisha viongozi wa CHADEMA’’ Mama Lowassa alisikika akisema....
Duuh, afadhali wameshtuka mapema.
 
Jaman kuna watu hawataki kabisa kuskia chadema ikiwa chama ndani ya nchi hii.

Usiposkia ya mbowe utayaskia ya Lowassa Kila siku khaaaaaa!
Historia ya Tanzania inabaisha tulikuwa na NCCR-Mageuzi, tukapata CUF na sasa tuna CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani.

Historia hiyo hiyo itaihukumu CHADEMA kama ilivyoihukumu NCCR-Mageuzi na CUF.

Usiwe na wasi wasi kwa sababu wenye CHADEMA wanatuambia walianza na mungu na watamaliza na mungu!
 
Back
Top Bottom