Familia ya Edward Lowassa imewastukia CHADEMA!

Familia ya Edward Lowassa imewastukia CHADEMA!

Historia ya Tanzania inabaisha tulikuwa na NCCR-Mageuzi, tukapata CUF na sasa tuna CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani.

Historia hiyo hiyo itaihukumu CHADEMA kama ilivyoihukumu NCCR-Mageuzi na CUF.

Usiwe na wasi wasi kwa sababu wenye CHADEMA wanatuambia walianza na mungu na watamaliza na mungu!

Hii hasa ndio ilikuwa lengo la hii post yako. Mwanzo nillijiuliza mbona leo umeanza kuleta post ya kimbea? Kumbe lengo lako ilikuwa kuonyesha cdm itadhoofu kama hivyo vyama kwa kutaka kuonyesha historia ndio ilivyo. Na ninapenda ujue Lowassa hamna mvuto na msukumo mnaojidanganya anao, na kama huamini ngoja uone akirudi ccm jinsi watu watakavyoshukuru.

Juzi ulileta uzi ukionyesha kuna chama kitaletwa na kitengo kwa maana ya kwamba hivi vilivyopo ni matakwa ya kitengo kutokana na ccm kuwa chama dola. Na sasa naona umerudia humohumo kwa mantiki ya kwamba ndio tuko mbioni kwenda kwenye chama hicho. Ni hivi kwa sasa wajinga wameisha isipokuwa wamebaki waoga. Na hizi mbinu chafu za kuiua cdm zina lengo hilo, kwa bahati mbaya mbinu zonatumika ni za kizee huku mnaotarajia wabadilike wameshahama kwenye ujinga huo. Kwa maneno marahisi hiyo Tiss imebaki analogue huku wananchi wako Digital, na ndio maana unaona zinatumika nguvu nyingi na akili kidogo kufanikisha huo upuuzi.
 
We have had had so much of EL politically in the course of three years, it is high time he considered retiring from active politcs. He can continue to advise nevertheless. Mwanae akitaka ajiingize mwenyewe na sio kuwa dragged into the theatre unwillingly.
 
Historia ya Tanzania inabaisha tulikuwa na NCCR-Mageuzi, tukapata CUF na sasa tuna CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani.

Historia hiyo hiyo itaihukumu CHADEMA kama ilivyoihukumu NCCR-Mageuzi na CUF.

Usiwe na wasi wasi kwa sababu wenye CHADEMA wanatuambia walianza na mungu na watamaliza na mungu!
Sasa kama mnafahamu CHADEMA itakufa by default kulikuwa na haja gani ya kuzuia Shughuli zao za kisiasa?? Chaguzi ndogo vipi mpaka mtumie manguvu makubwa kama mnajua CHADEMA itakufa by default

Kama watanzania wote mnawaza hivi basi tutaendelea kuwa LDC kwa miaka 50 ijayo
 
Japo umeandika kipropaganda sana.. Kuna nukta zinatoa mwanga..

Bi Regina alikataa kupewa Ubunge wa Viti Maalum. Leo Fred nae amechomoa kuwa Mbunge. Inaonesha hii EL Family haitaki longterm string na CHADEMA.

Siamini kama hii inatokea tu!
 
A LIABILITY OR AN ASSET? Hapo ndo mjue kuwa huwa kuna akili na fuvu la kichwa.
He's an ASSET.... Na alileta mtaji wa kura na rasilimali fedha n.k ila hakuna asset inayodumu milele ndio maana kuna depreciation factor kwenye Asset management kwahiyo hakuna uhusiano wa hyo kauli na lowassa maana mpaka sasa cjajua anakuwa liability kwa lipi hasa wakati aliwapa mtaji CHADEMA ila umeharibiwa tu na udikteta

Na kama lowasa ndio shida CHADEMA vp CUF na ACT au NCCR? Mbona mnajifanya hamuoni?? Hivi mngeruhusu siasa na zile nyomi kama kawa unafkiri mngekuwa mnaleta hizi pumba zenu kuwa CHADEMA inakufa??

Mnakera sana Wabongo..... Mmejaa ushabiki tu na unakuta watu wazima wanakunywa kahawa alafu wanaongea hii hoja na ndio maana linchi letu bado masikini maana shida inaanzia kichwani kabla ya kiuchumi
 
Historia ya Tanzania inabaisha tulikuwa na NCCR-Mageuzi, tukapata CUF na sasa tuna CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani.

Historia hiyo hiyo itaihukumu CHADEMA kama ilivyoihukumu NCCR-Mageuzi na CUF.

Usiwe na wasi wasi kwa sababu wenye CHADEMA wanatuambia walianza na mungu na watamaliza na mungu!
Huku nyinyi mlianza na policcm ili mpate ushindi usiohalali nakumalizia na policcm+nec ili mdumu maisha hapo?

Hivi kweli ndugu ikiwa mnajiamini kisawasawa kiuwingi WA wananchi+kupendwa kwa kila leo na raia kwanini makatibu wenu wamajimbo+policcm wanasababisha fujo kibao.


Na ndio maana ccm maisha yake yote haitashinda hata chaguzi moja kikura.

Mtabaki kuwatumilia policcm ili wawapatie ushindi halafu mkae kwenye maiki mjisifie uchaguzi ulikuwa huru na haki aibu zenu.

Jua kwamba mwisho WA maji ni tope.
 
Kuna watu wanawewekesa sana aisee yaani küwachukua mâdiwani wote hao bado tu mna Lowasa fever?
Ni kweli, pamoja na kuchukua pesa zake wakati wa Uchaguzi Mkuu lakini bado wanataka waendelee ''kumkamua''!
 
Unakodoa macho, kusoma na kujibu andiko la mtu unayefahamu ni masikini wa akili! Basi wewe utakuwa ni zaidi ya masikini wa akili.
Kwanini upotoshe ukweli uachwe unaangaliwa kisa ya utahir wako?mkue wanaccm tafuteni habari za joketi mtuletee sio huu utoto
 
Shameless,ideally backed man from Chattle unatia aibu!!!!Mkuu wa wako wa propaganda anaona unatoa ushuzi wa kondoo.
Mkuu;
Ninashukuru sana umetimiza haki yako ya kujieleza pamoja na kwamba ulichokiandika kimesadifiwa na akili za kijinga!
 
Kuna methali inayosema, Mja hakosei mara moja, kurudia ndio kosa.

Hii ina maana kuwa mtu anaweza akafanya kosa mara ya kwanza. Hiyo si hoja. Lakini akirudia kosa lile lile, basi hapo amekusudia na anafaa kuadhibiwa au kulaumiwa.

Familia ya Edward Lowassa amekataa kurudia kosa mara ya pili baada ya kukataa kuwa chanzo cha mapato kwa baadhi ya viongozi wa CHADEMA mkoani Arusha.

Kabla hata ya kuongea na kukubaliana na familia ya Lowassa, baadhi ya viongozi wa CHADEMA katika Mkoa wa Arusha wakiongozwa na Diwani wa CHADEMA katika Kata ya Sombetini, Ally Bananga na Godbless Lema waliamua kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kuwa mgombea wa Ubunge katika Jimbo la Monduli na kuzipeleka nyumbani kwa Fred Lowassa wakishinikiza azijaze na watazirudisha.

Baada ya kutumia muda mwingi wakimshawishi akubali maombi yao, Fred aliwaambia wamuache kwanza atafakari kwa kina kabla ya kutoa uamuzi wa mwisho.

Majibu ya Fred yaliwapa moyo kiasi kwamba wakaanza kutangaza kwenye mitandao mbalimbali kuwa wanapeleka mgombea katika Jimbo la Monduli ambaye ni ‘’machine’’ na kwa sababu hiyo, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo aanze kutafuta kazi nyingine.

Habari za Fred kupelekewa fomu zilipomfikia Mama yake, Regina Lowassa aliagiza na kusema hizo fomu zilirudishwe mara moja kwa wahusika kwa sababu familia haina tena pesa za kuchezea hovyo hovyo. ‘’Tumetumia pesa nyingi wakati wa Uchaguzi Mkuu bila mafanikio, hatuwezi kuendelea kuwa shamba la kutajirisha viongozi wa CHADEMA’’ Mama Lowassa alisikika akisema.

Habari hizi ziliwafikia viongozi wa CHADEMA ambao waliamua kwenda kuonana na Edward Lowassa ili amshawishi mwanaye. Lowassa aliwaambia Fred ni mtu mzima na hawezi kumpangia nini akifanye au kuamua hatma ya maisha yake kwa sasa.

Majibu ya Lowassa yaliwafanya viongozi wa CHADEMA kuanza kusaka mgombea mwingine.

Habari zinaeleza kuwa kwa sasa familia ya Lowassa ameanza kujiweka mbali na harakati za CHADEMA ndio maana kwa sasa huwezi kumuona Mke wa Lowassa katika shughuri za Balaza la wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) kama ilivyokuwa hapo zamani.

Kuna msuguano mkali kati ya familia ya Lowassa na wapambe wa Lowassa kama Khamis Mgeja na Sheikh Rajab Katimba ambapo familia yake inamtaka aachane na siasa huku wapambe wakimshawishi kuwa ana nafasi tena ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania mwaka 2020 ili waendelee kunufaika kifedha na uwepo wake katika siasa.
Yajayo yanafuraisha
 
Mkuu;
Ninashukuru sana umetimiza haki yako ya kujieleza pamoja na kwamba ulichokiandika kimesadifiwa na akili za kijinga!
I respect your regret to get hacked off your personal defamation.Its a good step towards self realisation. Just keep in touch!!!
 
huyu MsemajiUkweli ni masikini wa akili anayetumika mithili ya mashine ya kubangua korosho , Lowassa alishaondoka ccm akawashinda kwenye urais kwa tofauti ya zaidi kura mil 6 , wakampora lakini bado wanajipendekeza .

Unajua mke ukimwaacha na ukampa talaka yake, kila apitapo utasikia aah bwana gani yule nimeshit NA wala asinijue
 
Anachofanya anatengeneza bajeti kubwa,anaomba kamati kuu akikopeshe chama milioni 500,za uchaguzi buyungu
kwa kua yeye ni mkuu wa kambi ya upinzani,anapewa tiketi ya ndege na mlinzi wake kutoka ofisi ya bunge bure, anaruka hadi kigoma,anawajaza wafuasi gesi kesho anarudi Dar,hapo hajatoa hata senti tano,gharama za kampeni atajijua mgombea na wabunge wanachanga
Ruzuku ikiingia tu anapiga panga milioni 500 yake!
Kwa maelezo haya ndio maana vyama vinapata hati chafu kutoka kwa CAG.
 
Back
Top Bottom