nimekubali mwanjelwa, haya mambo siyo rahisi kama wengi wanavyoyachukulia. ni kweli njia kubwa ya kupata ukimwi ni zinaa, lakini sidhani kama ni sahihi kuihukumu hiyo familia kwa kuiita familia malaya na isiyo tii maagizo ya Mungu. Huenda ni kazi ya Mungu inakamilika hapo, ndo maana mtoa thread amesema hawa watu ni wastaarabu tu, hapo ni kuwaombea tu. yawezekana kuteketea kimwili kwa hii familia ni kuokoka kiroho ka upande mwingine. zaidi ni kwamba yanayotokea kwenye hiyo familia yanaweza yakawa ni chanzo cha mabadiliko miongoni mwetu, na pia hata maoni yetu yaweza kutufanya tutende dhambi juu ya hao watu- haswa pale tunapopata ujasili wa kuwahukumu kwa kuwaita wazinzi. labda niwaulize watu hapa. kama nduguyo anaumwa na anahitaju huduma yako, utatafuta gloves za kuzuia kugusana moja kwa moja , hata kabla hujajua anaumwa nini??? , ikiwa wengi waliambukizwa katika kumhudumia aliyeanza kuumwa mwanzo, wangewezaje kujizuia kuugua na kufa baada ya huyo wa kwanza kuwaambukiza???. au ni wanapi hapa tukijisikia vibaya tu tunaanza a kupima ukimwi????. siyo mpaka yote yanaposhindikana ndo tunapima ukimwi??? sasa nuda wote huo kabla ya kujua , ni kweli wauguzaji wanakuwa wamechukua tahadhari za kutosha kuzuia mugusano hatarishi na mgonjwa ?????.
haya mambo yanazungumzika yakiwa kwa wenzio, yakiwa kwako, huwezi kuona , nikama kutafuta kujibeba mwenyewe ukiwa umekaa