Familia inaangamia kwa UKIMWI...

Hamna shida/tabu ... huwa nadhani kila mtu ni msukuma! Pole


Annina

asante kwa uafafnuzi,

unajua mimi ni mzito kidogo kujifunza lugha za wengine, nimeishi na wasukuma kitambo fulani lakini huwezi kuamini, hata salamu naumauma maneno!

sasa itabidi niongeze bidii ktk kujifunza kisukuma. just 4 you dear
 
Preta, nadhani kuna uwezekano huo pia maana mara nyingi watu huwa wanauguzana nyumbani - inasikitisha sana. Kuhusu elimu nadhani wanayo, tatizo ni kufuata maelekezo inakuwa ngumu wakati mwingine, huwezi kuacha kumhudumia mgonjwa wako sababu gloves zimeisha au ziko mbali na unahitaji kumhudumia haraka. nadhani kama wengi walivyosema pamoja na tahadhari na kumshirikisha Mungu kunahitajika sana sana.


Annina
 
Preta, nadhani kuna uwezekano huo pia maana mara nyingi watu huwa wanauguzana nyumbani - inasikitisha sana. Kuhusu elimu nadhani wanayo, tatizo ni kufuata maelekezo inakuwa ngumu wakati mwingine, huwezi kuacha kumhudumia mgonjwa wako sababu gloves zimeisha au ziko mbali na unahitaji kumhudumia haraka. nadhani kama wengi walivyosema pamoja na tahadhari na kumshirikisha Mungu kunahitajika sana sana.


Annina

mambo mengine ni mitihani migumu sana,

kisaikolojia, mtu ambaye siku zote mnashirikiana vizuri kisha baada ya kuugua avae gloves kabla hajakuhudumia, lazima utahisi unyanyapaa, na madhara ya unyanyapaa nayo si madogo, hivyo ni mtihani kwelikweli na unahitaji ujasiri sana na kumwomba Mungu apishilie mbali.
 
Kuna familia tupo nayo karibu inaangamia kwa ukimwi. Alianza baba na mama, akafuatia kaka, dada na leo dada mwingine - wamebaki 2 tu sasa kwenye familia ya watu 7! Kuna watu wanasema ukimwi ukiingia kwenye familia unaweza kuondoka na watu kadhaa... kitaalam haikubaliki lakini kuna kesi nyingi za namna hii sijui kwanini


Annina



Annina, ninataka nikueleze kitu sijui utakubali,kinahusu hao wagonjwa......

I have solution, which I have seen it works
 
Waberoya, nitashukuru sana, pls.


Annina


Dear Annina, I am not sure how you will handle this information, wengine wanatukana,, kusonya au kubisha, ila mimi nasema ukweli wa nililoliona kwa macho yangu, kupapasa kwa mikono yangu!

Kuna wagonjwa ambao nimewaona wakipona ugonjwa huu kwa jina la Yesu. Nilikuwa katika timu ya maombezi nikiwa Tz, kuna wagonjwa walikuwa wakija kanisani hawawezi kabisa, baada ya maombi wakapona kabisa, wengine huwezi hata kuwatambua tena kuwa walikuwa wanaumwa.Kuna mchungaji anaitwa Tosha yuko Mwanza yeye ndiye alileta hii semina na watu tukaiweka katika practise

Nimesema nimeona kwa macho yangu maana pale kanisani walipoanza kuombewa wagonjwa wa awali baadaye kanisa likabadilika na kuwa kituo cha wagonjwa, wengi walikuja na wengi walipona, wako ambao hawakupona, I can not say anthing about that, wako walioombewa na kwa bahati mbaya wakafariki ila wengi wao walikuwa wanakuja too late wakati ubongo umeshashambuliwa kiasi cha mtu kutokuwa na imani au kutoelewa unamweleza nini.

Nakuambia ili hao ndugu 2 wawe mashuhuda wa matendo makuu ya Yesu faida watakazopata.

1. watapata kuona na kushuhudiwa bila uoga na wenzao waliokuwa wakiumwa ukimwi hapo awali na wakapona
2. hawatakuwa discriminated kutokana na kuona wenzao wote ni wa aina hiyo

3. watapata tumaini jipya

Narudia, nasisitiza ninachoongea hapa si fiction is reality with my degrees in engineering; I do believe Jesus heals, Nasema hivyo kwa sababu watu huwa hawaamini, mwanzoni hata mie sikuwa naamini mpaka nilivyokuwa mmoja wa waombezi; wako waliokuwa rafiki wa karibu wakaombewa wakapona, wakapima majibu negative na leo wameolewa na kuoa,

wako wanaopima na kukuta negative, wako wanaopima na kukuta bado wana wadudu, japo hali zao zimebadilika; wako wasiotaka kabisa kupima na kuamini wamepona na kweli unaona hali zao. Hii inatokana na tofauti ya Imani, kwani pastors ni initiators tu wa imani ya uponyaji, they are not expert of healing!

Kuna watu walienda hawatembei, wamebebwa, dhaifu, magonjwa yote ya ukimwi, lakini tukaona wanabadilika na furaha na tumaini lao la kuishi kurejea tena. for those 2 people najua watakuwa mashuhuda wakisema ni ''sisi tu tumepona kuleta habari''

Dear Annina it is certain a new thing, unbelievable and you may shock you as well.But believe, I am not drunk! my senses are working perfectly beyond doubt, I am not dreaming either! I am telling something that my n-a-k-e-d eyes saw!. Please be one of people who will witness this in this very world!

Kanisa hilo liko changanyikeni mbuyuni, nyuma ya chuo kikuu cha DSM simu ya mchungaji ni 0754 454517.Mimi siko hapo, niko Canada hivi sasa. hakuna gharama zozote! wakifika watapokelewa na kuhudumiwa!

Just convince them to go, give them this number let them see this pastor and I am sure their agony of fear and pain will be history! I guess you want this!
 
Hawa watu ni wastaarab angalau kwa kadri ya ufahamu wangu - hasa watoto, inasikitisha sana wanavyokwisha wakijiona, kwa vyovyote baada ya misiba 2 ya mwanzo watoto watakuwa walijitahidi kuwa makini zaidi (busara ya kawaida) lakini bado wameambukizwa na vilio vinaendelea

Annina
......... .......Samahani Anina sikujua kama ni watu wastaarabu, mie nilifikiri ni watu wasiokuwa na uaminifu kwenye mahusiano yao.
Kama ni hivyo basi kutakuwa na ukosefu wa elimu jinsi ya kumhudumia mwathirika wa ukimwi.
Vile vile kuna uwezekano wanawapenzi ambao si waaminifu, hao ndugu zako watakuwa ni wastaarab lakini wapenzi wao labda sio wastaarab.

Bongo ukimwi kumbe bado upo?

Na wewe nawe kuna sehemu kusipokuwa na ukimwi hapa duniani.Hata huko ughaibuni ukimwi upo kama kawaida..........watu wengine bwana aaahhhhhhhh!!!
 
swala ukimwi kusemakweli sijui tufanyaje hili kuokoa maisha ya ndugu zetu manake wengi wetu kwenye jamii wanachukulia kama utani.kujikinga watu hawataki,kupima hawataki,kuoa na kutofanya mapenzi nje ya ndoa hawataki,sasa tuwasaidie vipi?


mie naona tujaribu kuweka picha za mfano wa waathirika kila kona labda watu wataogopa.
 
swala ukimwi kusemakweli sijui tufanyaje hili kuokoa maisha ya ndugu zetu manake wengi wetu kwenye jamii wanachukulia kama utani.kujikinga watu hawataki,kupima hawataki,kuoa na kutofanya mapenzi nje ya ndoa hawataki,sasa tuwasaidie vipi?


mie naona tujaribu kuweka picha za mfano wa waathirika kila kona labda watu wataogopa.
Wewe ukiathirika kwa namna yeyote ile utaweza ku volunteer kuweka picha yako kwenye hizo kona? Maana si kila anayeathirika ni mzinzi, na kuwa anastahili adhabu na majuto.

Na hata kama ni mzinzi, kwanini wapenda kumhukumu mwenzako?
 
mkuu waberoya,mungu akubariki sana.nimefurahishwa na ushuhuda wako kuhusu uponyaji wa wagonjwa wa ukimwi na ninapenda kuungana na wewe kuwaambia wapendwa wengine kwamba mungu anaweza na hakuna ugonjwa wala tatizo ambalo ukilipeleka mbele za mungu kwa kuomba huku uliwa na imani litashindikana.nimeona mengi katika maisha yangu yanyoonyesha ukuu wa mungu ktika maisha yetu. Naomba niseme tu kwamba damu ya yesu ina nguvu katika uponyaji na inaponya magonjwa yote.
 
Na vipi kuhusu kufanya mpango wa upimaji kwa lazima? Nasema hivi kwani nimekwishashuhudia ugomvi wa mke na mume; Mume kwa kuhisi mkewe kutokuwa muaminifu aliomba waende wakapime kama wameathirika au la; mke aligoma katakata kuwa yeye alishapimwa wakati akijifungua (miaka 2 nyuma) hivyo mume aende mwenyewe! Mume kwa uajsiri amekwenda amepima na yuko salama; hataki tena ushirikiano na mkewe na anajiandaa kutoa talaka! Hili gonjwa jamani litatumaliza na tunakoelekea litamaliza kabisa nguvu kazi ya taifa hili kwa sababu naona tafiti nyingi zikituonyesha kuwa kundi la nguvukazi ndio linaloathiriwa zaidi! Naona kuna haja ya kulitungia sheria za kutubana sisis wenyewe! Haya mambo ya hiari hayatusaidii kwa sasa!
 
kisayansi inakataa augment kwamba ukimwi ukiingia kwenye familia wote mnapukutika...but my take is familia ya hivyo imeshamiri kwa uzinifu ndo maana

Sio lazima wote wawe wazinifu...kuna njia nyingi za kuambukiza UKIMWI..inawezekana hiyo familia hawakujijua mapema hivyo hawakuchukua measures mblaimbali za kuepuka..mfano sharing baadhi ya vitu..
 
Kuna kesi baba alitembea na house girl ambae ameathirika. Baba akamwambukiza mama. Walikuwa na watoto wakubwa wa kiume nao wanatembea na house girl. Mwisho wa siku nyumba yote iliangamia.

Cha msingi sio kuhukumu watu kwa yaliyotokea bali sisi tuchukue tahadhari tusimwamini mtu awaye yote kwamba ni salama.

Mchukue mwenzako mkapime na muwe waaminifu
 
Waberoya, asante sana kwa ushuhuda na ushauri, nitajaribu kufikisha ujumbe na no ya simu kwa hao na wengine ninaowafahamu. Kuna kaka mmoja tulikuwa nae chuo amejaribu maombi katika makanisa mbalimbali lakini naona hali yake bado si njema, kwa kuwa yeye ni mtu wa imani sasa (baada ya kupata huu ugonjwa alimrudia Yesu) nitamshauri ajaribu na huko.

Asante sana,


Annina
 
Waberoya, asante sana kwa ushuhuda na ushauri, nitajaribu kufikisha ujumbe na no ya simu kwa hao na wengine ninaowafahamu. Kuna kaka mmoja tulikuwa nae chuo amejaribu maombi katika makanisa mbalimbali lakini naona hali yake bado si njema, kwa kuwa yeye ni mtu wa imani sasa (baada ya kupata huu ugonjwa alimrudia Yesu) nitamshauri ajaribu na huko.

Asante sana,


Annina

Amen, thanks for believing
 
swala ukimwi kusemakweli sijui tufanyaje hili kuokoa maisha ya ndugu zetu manake wengi wetu kwenye jamii wanachukulia kama utani.kujikinga watu hawataki,kupima hawataki,kuoa na kutofanya mapenzi nje ya ndoa hawataki,sasa tuwasaidie vipi?


mie naona tujaribu kuweka picha za mfano wa waathirika kila kona labda watu wataogopa.

Arsene Wender, sio wote walio na maambukizi hawakujali ndio maana wameathirika. Kuna wengi ambao wameupatia ndani ya ndoa zao wakiwa waaminifu ila mwenzi mmoja anatoka na kukuletea, kuna watoto waliozaliwa na huo ugonjwa na sasa wamekuwa wakubwa na wanasoma vyuo vikuu, kuna bibi na babu ambao wanaathirika kwa sababu ya kuhudumia wajukuu ambao watoto wao waliofariki wamewaachia, hivyo ukiweka picha zao hadharani utakuwa unawaonea sana. Cha msingi ni kuendelea kuelimisha jamii kila siku kuhusu athari za ugonjwa huu.
 
Mahai umesema sawa kabisa, wengi tu wameambukizwa licha ya kuwa waaminifu kwenye ndoa zao. Tuzidishe maombi

Asante sana,


Annina
 
Annina
Hili swala ni tete sana hasa kwenye unyanyapaa. Kwa kuwa watu wanaogopa unyanyapaa, wanajificha, hawafuati masharti ya dawa za kurefusha maisha na pia wanaendelea kuambukiza. Nadhani tukiweza kuvunja ngome ya unyanyapaa, tutakuwa tumeanza kupata suluhu kuelekea kubadili tabia. Kama Mzee Mwinyi alivyosema, "hili swala limekaa mahali ambapo wengi tunapapenda"
 
Back
Top Bottom