FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 92,894
- 109,227
Toka nilipoanza kuzisoma na kuzifanyia tafiti zangu binafsi R 4 za mama Samia nimeona na nnaendelea kuona kuwa R 4 za mama Samia zimelenga kumpa uhuru wa kweli kila mmoja wetu kivyake na siyo uhuru wa kukusanywa kikundi na kujazwa ujinga na "viongozi".
Tatizo kubwa na la kipekee la Watanzania ni ujinga, hili nimelirudia mara kwa mara na naendelea kulirudia. Naamini kwenda shule pekee na kujaza vyeti ukuta mzima siyo kuelimika, kuelimika ni zaidi ya hapo. Hutoelimika mpaka uwe na uwezo wa kusikiliza na kufata hekima njemaza qwengine daima.
Kuondoa ujinga ni pale wewe kama wewe utapoanza kufikiri, kuwaza na kutenda kwa faida ya jamii na kuwacha mazowea ya ujinga wa u "mimi", "u yangu" na "u vyangu". Anza u sisi, u vyetu. Fikiria wenzako kabla hujajifiria nafasi yako. uwa huru ni kuwa na fikra za faida kwa wengine, siyo kwako. Bila kuwa na faida kwa wengine huna faida yoyote.
Ujinga mwengine ni ujinga wa kuwa tegemezi kwa wengine tuliojazwa nao kuanzia mkoloni mpaka leo hii. Ukienda kuomba msaada kwa rafiki, kaka, dada, mjomba, shangazi (kwa mtazamo wako ana uwezo) wa kukusaidia akishindwa kukusaidia basi kishakuwa mbaya, huo ni ujinga wa utegemezi. Anza kuufuta kwa kufanya "reconciliation".
R 4 za mama Samia zina vina virefu na vipana sana na vina vyake vinatugusa sote, kila mmoja wetu kivyake kwa faida ya walio wengi.
R ya kwanza "Reconciliation" ya mama Samia ina kina (very deep) kuliko tunavoisoma kijuu juu kuwa ni kusameheana tu. Unapomsamehe mwenzako hufikirii maumivu yaliyokupata wewe bali unafikiria kuyaponya maumivu na kuondoa makovu yako kwa kumsamehe yeye kwa faida yako, yake na ya jamii kwa ujumla. Kusamehe {forgiveness) ni dhana moja tu katika "reconcialtion".
Nikiiongelea hii dhana moja tu ya "Reconciliation" ntaujaza huu uzi bila kuzigusia dhana nyingine.
Kwa ufupi "reconciliation" imelenga kukuweka huru kwanza katika fikra zako na vitendo vyako, inakupa amani ya moyo na nafsi yako na ya wale ambao ume "reconciliate" nao. Reconciliation ya kwanza kabisa ni kukubali ndani ya moyo wako kuwa upo huru na jamii yako inayokuzunguka na hauna minyororo (minyonyoro, ki mama Samia) inayokufunga nafsi na mawazo yako. Reconiciliation ni ufunguo wa kuifunguwa minyororo inayokuzonga zonga kifikra na kukuweka huru kabisa.
Leo naishia hapo, nikitoka hapo ntaingia kwenye R ya pili.
Anza kuwa huru kwa kufanya reconciliation" na nafsi yako kwanza, halafu tazama unaendelea kufanya "reconciliation" na nani kila siku ya maisha yako?
Unapochangia uzi huu kuwa huru bila kujizonga zonga na minyororo uliyojifunga au uliyofungwa kwa kufanywa u mjinga wa kuburuzwa. Fanya "reconciliation" ya kweli. Ongea na nafsi yako.
Itaebdelea.