sio dharau lengo la kila mmoja ni kulinda haki na muonekano wake ktk jamii
(to maintain status quo) Sii kweli kuwa kesi hiyo inachelewesha kesi zingine
kwani sheria ya mwenendo madai inawaruhusu kufanya hivo.
kwa mtazamo wangu sio dharau wala kupotezeana muda ni technicali za kisheria ndio maana mzee mengi anahudhuria sana mahakamani kila kesi inapotajwa. anafahamu akishindwa na manji. ataamriwa kulipa gharama za kesi kwa manji. na kwa uelewa wangu zitakuwa fedha nyingi sana .na hata mzee Mengi akishinda manji naye ataamriwa alipe gharama za kesi ambazo nazo zitakuwa nyingi. hivyo shilingi 1 ni ujanja tu kuna zaidi ya hicho kiasi.
Majaji wa mahakama za common law, kama hapa kwetu, wanaruhusiwa na sheria za bunge kujitungia kanuni za kuratibu mchakato mzima wa kuanzisha na kuendesha kesi, rules of civil procedure. Wangeweza kujiwekea taratibu za kuzuia kesi hizi za shilingi moja moja.
Katika nchi nyingine kuna "jurisdictional amount" ambayo ni kiwango cha chini kabisa ambacho ni lazima ukidai kabla mahakama haijajisumbua kukusikilizeni.
Mahakama ni sehem ambayo kila mtu anao uhuru wa kupeleka malalamiko yako kama anaona kuna sehem hajatendewa haki na anao uhuru wa kufungua kesi kutokana na anavyojisikia so kwa haya mabwana hasa Manji ambae ni mshitaki anao uhuru wa kudai hiyo TSH 1 na alikuwa hata sahihi kudai Mengi akiri kusema maneno ya kumkashifu bila fidia yyte.
M-pesa mi nakuunga mkono, pia wewe kutuletea hii thread humu ni kuidharau jf na kutupotezea mudaNimekuwa nikitafakari sana hii kesi ya bw. Reginald Mengi Vs Yusuph Manji.
Kwa mtazamo wangu naona ni dharau pamoja na kipotezea mahakama muda. Kuna kesi ngapi zilizorundikana mahakamani huku watu wakiteseka kusubiri haki itendeke? Lakini hawa mabwana kutokana na kiburi cha pesa wameamua kunyima haki wananchi wengine kwa kuendeleza kesi ya kipumbavu. Wenye kujua sheria mnasemaje?