Faida za Mtama

Faida za Mtama

Mtama ni nafaka iliyo na kiwango kingi cha protini, vitamini B6 na B1 pamoja na madini chuma, copper, magnesium, selenium na zinc.


Pia, huwa na kiasi cha kutosha cha kampaundi za Flavonoids, phenolic acids na tannins ambazo hutumiwa na mwili kama viondoa sumu.

Husaidia kupambana na aina mbalimbali za uvimbe mwilini, huboresha mfumo wa chakula pamoja na kupunguza hatari ya kuugua magonjwa ya moyo, kisukari na sararani.

Sifa nyingine kubwa ya mtama ni kutokuwa na Gluten, aina ya protini inayofanana na gundi ambayo huleta mzio (allergy) kwa baadhi ya watu hasa wale wenye ugonjwa wa Celiac (Celiac disease).

Chanzo: American Sorghum
.. ni kimea kizuri kwa kutengenezea pombe
 
Naskia lishe ya mtama inaongeza heshma hasa kwa wanaume wa daslam...teh😜
 
Mtama ni jina la general humo humo kuna serena nyeupe/nyekundu,uwele nk hata ukienda kununua mbegu watakuuliza unataka mtama aina gani? sisi kuna aina zaidi ya aina 5 za mtama ukiwemo na uwele
Inawezekana Mkuu, maana nipo na wagogo wanasema ni tofauti,Labda kwa hapo kisayansi kuwa ni aina ya mbegu,nakubsliana na Wewe!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom