Faida za kula ndizi mbivu

yani kusikia ndizi nahisi hadi kuumwa.... tuwaachie wanyakyusa... wachaga na wahaya... I HATE BANANA OF ALL KINDS
 
534804_290728761059522_1459491702_n.jpg

This is interesting. After reading this, you’ll never look at a banana in the same way again.Bananas contain three natural sugars – sucrose, fructose and glucose combined with fiber. A banana gives an instant, sustained and substantial boost of energy.
Research has proven that just two bananas provide enough energy for a strenuous 90-minute workout. No wonder the banana is the number one fruit with the world’s leading athletes.
But energy isn’t the only way a banana can help us keep fit. It can also help overcome or prevent a substantial number of illnesses and conditions, making it a must to add to our daily diet.
DEPRESSION
According to a recent survey undertaken by MIND amongst people suffering from depression, many felt much better after eating a banana. This is because bananas contain tryptophan, a type of protein that the body converts into serotonin, known to make you relax, improve your mood and generally make you feel happier.
PMS:
Forget the pills – eat a banana. The vitamin B6 it contains regulates blood glucose levels, which can affect your mood.
ANEMIA
High in iron, bananas can stimulate the production of hemoglobin in the blood and so helps in cases of anemia.
BLOOD PRESSURE:
This unique tropical fruit is extremely high in potassium yet low in salt, making it perfect to beat blood pressure So much so, the US Food and Drug Administration has just allowed the banana industry to make official claims for the fruit’s ability to reduce the risk of blood pressure and stroke.
BRAIN POWER
200 students at a Twickenham school ( England ) were helped through their exams this year by eating bananas at breakfast, break, and lunch in a bid to boost their brain power. Research has shown that the potassium-packed fruit can assist learning by making pupils more alert.
CONSTIPATION
High in fiber, including bananas in the diet can help restore normal bowel action, helping to overcome the problem without resorting to laxatives.
HANGOVERS
One of the quickest ways of curing a hangover is to make a banana milkshake, sweetened with honey. The banana calms the stomach and, with the help of the honey, builds up depleted blood sugar levels, while the milk soothes and re-hydrates your system.
HEARTBURN
Bananas have a natural antacid effect in the body, so if you suffer from heartburn, try eating a banana for soothing relief.
MORNING SICKNESS
Snacking on bananas between meals helps to keep blood sugar levels up and avoid morning sickness.
MOSQUITO BITES:
Before reaching for the insect bite cream, try rubbing the affected area with the inside of a banana skin. Many people find it amazingly successful at reducing swelling and irritation.
NERVES
Bananas are high in B vitamins that help calm the nervous system..
Overweight and at work? Studies at the Institute of Psychology in Austria found pressure at work leads to gorging on comfort foodlike chocolate and chips. Looking at 5,000 hospital patients, researchers found the most obese were more likely to be in high-pressure jobs. The report concluded that, to avoid panic-induced food cravings, we need to control our blood sugar levels by snacking on high carbohydrate foods every two hours to keep levels steady.
ULCERS
The banana is used as the dietary food against intestinal disorders because of its soft texture and smoothness. It is the only raw fruit that can be eaten without distress in over-chroniclercases. It also neutralizes over-acidity and reduces irritation by coating the lining of the stomach.
TEMPERATURE CONTROL
Many other cultures see bananas as a ‘cooling’ fruit that can lower both the physical and emotional temperature of expectant mothers. In Thailand , for example, pregnant women eat bananas to ensure their baby is born with a cool temperature.
So, a banana really is a natural remedy for many ills. When you compare it to an apple, it has FOUR TIMES the protein, TWICE the carbohydrate, THREE TIMES the phosphorus, five times the vitamin A and iron, and twice the other vitamins and minerals.. It is also rich in potassium and is one of the best value foods around So maybe its time to change that well-known phrase so that we say, ‘A BANANA a day keeps the doctor away!’
 
Aise hivi kumbe zamani nilikuwa na akili hivi;
daah sijui siku hizi zimekwenda wapi.
 
UMUHIMU WA KULA NDIZI - UMUHIMU WA KULA
NDIZI
Baada ya kusoma makala yangu ya leo na
kuzingatia nilichokiandika, bila shaka utaanza
kuiangalia ndizi kwa mtazamo tofauti na
uliokuwa nao hapo awali. Ndizi mbivu ni tunda
maarufu sana duniani lakini ni watu wachache
wanaojua uwezo, faida na maajabu yaliyomo
kwenye tunda hili.
Ndizi ina aina tatu za kipekee za sukari
zinazojulikana kitaalamu kama Sucrose, Fructose
na Glucose na vilevile ina kiasi kingi cha
ufumwele (fibre) ambacho husaidia sana katika
usagaji wa chakula tumboni.
Ndizi ina uwezo mkubwa wa kuongeza na
kuimarisha nishati ya mwili. Unaweza kupata
nishati ya kufanyakazi ya muda wa dakika 90
kwa kula ndizi mbili tu. Bila shaka ndizi ni tunda
muhimu sana kwa wanamichezo. Hata hivyo,
nishati siyo faida pekee unayoweza kuipata
katika ndizi, ni tunda lenye uwezo pia wa
kuponya na kuzuia matatizo mengi ya kiafya:
MFAIDHAIKO WA AKILI (DEPRESSION)
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chama Cha
Afya ya Akili cha Taifa (MIND) cha nchini
Uingereza, kwa watu wanaosumbuliwa na tatizo
la mfadhaiko wa akili, watu wengi waliondokana
na tatizo hilo na kujisikia vizuri baada ya kula
ndizi mbivu. Hali hii inatokana na ukweli
kwamba ndizi ina kirutubisho kinachojulikana
kama tryptophan, ambacho ni aina fulani ya
protini inayotumika mwilini kumfanya mtu kuwa
mtulivu na mwenye furaha.
MATATIZO WAKATI WA HEDHI
Kama wewe ni miongoni mwa wale akina mama
wanaopatwa na matatizo mbalimbali ya kiafya
wakati wa hedhi, unashauriwa kula ndizi mbivu
na unaweza kuponywa. Vitamin B6 iliyomo
kwenye ndizi, hurekebisha kiwango cha sukari
ambacho huweza kuathiri hali ya mtu.
UPUNGUFU WA DAMU (ANAEMIA)
Ndizi ikiwa ni chanzo kizuri cha madini aina ya
chuma (iron), inaweza kuwa ni dawa ya kuzuia
na kuponya upunguvu wa damu kwa sababu
madini ya chuma huamsha uzalishaji wa
chembechembe za damu mwilini.
SHINIKIZO LA DAMU
Tunda hili ni la aina ya kipekee, lina kiwango
kikubwa cha madini ya potasiamu (potassium)
na wakati huo huo lina kiasi kidogo sana cha
chumvi (sodium) hivyo kulifanya kuwa tunda
bora katika kupambana na tatizo la kupanda na
kushuka kwa shinikizo la damu.
Ukweli huo, hivi karibuni umeifanya Mamlaka ya
Dawa na Chakula ya nchini Marekani, iwaruhusu
wazalishaji na wauzaji wakubwa wa ndizi nchini
humo, kutangaza rasmi uwezo wa ndizi katika
kupambana na hatari ya shinikizo la damu na
kupatwa na kiharusi (stroke) kwa binadamu.
NGUVU YA AKILI
Hivi karibuni, wanafunzi wapatao 200 wa Shule
ya Twickenham nchini Uingereza, walisaidiwa
kufaulu mitihani yao kwa kula ndizi mbivu wakati
wa mlo wa asubuhi (breakfast), wakati wa
mapumziko na wakati wa chakula cha mchana,
ndizi ziliongeza uwezo wa akili zao. Utafiti
unaonesha kuwa potasiamu iliyojazana kwenye
ndizi, ina uwezo wa kumsaidia mwanafunzi
kuamsha uwezo wake wa kujisomea.
KASUMBA (HANGOVERS)
Moja ya dawa ya haraka ya kuondoa uchovu
unaotokana na ulevi wa jana yake (hangover) ni
kunywa �Milkshake� iliyotengenezwa kwa ndizi
na kutiwa asali. Ndizi hutuliza tumbo, ikisaidiwa
na asali, hurejesha kiwango cha sukari
kilichopungua kwenye damu wakati maziwa
hutuliza na kurejesha maji kwenye mfumo wake.
Mbali na matatizo yaliyoelezwa hapo juu, ndizi
pia husaidia katika matatizo mengine mengi
kama vile kutuliza mishipa ya fahamu, kuondoa
wasiwasi, kutuliza vidonda vya tumbo, kuondoa
asidi tumboni, kushusha joto mwilini,
kurekebisha mapigo ya moyo, n.k
Hivyo ndizi ni tiba ya magonjwa mengi na ni
bora, ukiilinganisha na Tufaa (Epo (Apple), ndizi
ina protini mara nne zaidi, wanga mara mbili,
vitamin A na chuma mara tano na vitamini na
madini mengine mara mbili zaidi ya tufaa.
Mwisho;
USIWEKE NDIZI KWENYE JOKOFU!

nb: copy and paste.
 
Mkuu asante sana!! Japo napenda sana kula ndizi mbivu na, nilikuwa najua faida zake chache; umenijuza mengi zaidi.
 
Nipeni recipe kutengeneza Juice ya banana jamani

mkuu ni easy tu nunua mtindi mdogo,ndizi mbili mbivu na fungu la spinachi au sukuma wiki, mimina mtindi kwny brenda ,tia na ndizi na spinachi kisha washa mpk zisagike vizuri baada ya hpo utakuwa tayari kwa kunywa,...actual Huu ndyo msosi ninaotumia kighegheto ninapokuwa Nina haraka au sina accès ya kupika
 
Baada ya kusoma hii hutaitazama ndizi tena kwa mazoea

Ndizi ina aina tatu ya sukari za asili zijulikanazo kama sukrozi, frutkozi na glukozi zilizochanganyika na nyuzinyuzi. Ndizi huongeza nguvu ya mwili kwa haraka. Tafiti zinaonesha ndizi mbili tu humpa mtu nguvu inayomwezesha mtu kufanya mazoezi ya kutumia nguvu kwa dakika 90 bila kuchoka. Hivyo si jambo la ajabu kwa ndizi kupendelewa zaidi na wanamichezo vinara duniani, ingawa si ndizi pekee zinazoweza kusaidia kuweka miili yetu katika hali ya ukakamavu.

Ndizi huweza pia kusaidia kuponesha au kuzuia maradhi mengi makubwa. Ili kuhakikisha kuwa unapata faida hizi za ndizi mwilini mwako kila siku, fanya tunda hili kuwa sehemu ya mlo wako wa kila siku.

Zifuatazo ni baadhi ya faida za ndizi mwilini mwako:

1. Mfadhaiko wa Akili (DEPRESSION)
Utafiti uliofanywa na MIND hivi karibuni unaonesha kwamba, wengi wa watu wenye mfadhaiko wa akili (depression) waliofanyiwa utafiti huo walisikia nafuu kubwa baada ya kula ndizi. Hii ni kwasababu ndizi zina aina ya protini ijulikanayo kama tryptophan ambayo hubadilishwa na mwili kuwa serotonin ambayo hujulikana kuufanya mwili ustarehe (relax), kuboresha hisia (mood) na kwa ujumla kufanya mtu ajisikie mwenye furaha.

2. Mfadhaiko kabla ya Hedhi (Pre Menstural Syndrome) :
Vitamini B6 iliyomo kwenye ndizi hudhibiti viwango vya glukosi kwenye damu ambayo huweza kuboresha hisia (mood) na hivyo kukuondolea mfadhaiko kabla ya hedhi. Achana na dawa – kula ndizi.

3. Upungufu wa Damu (ANEMIA)
Ndizi zina madini ya chuma (iron) kwa wingi sana, madini chuma huchochea uzalishwaji wa hemoglobini na hivyo kusaidia kuongeza damu.
4.
Shinikizo la damu (BLOOD PRESSURE):
Hili tunda la kipekee lina kiwango kikubwa cha potassium na kiwango kidogo sana cha chumvi na hivyo hufaa sana kushusha shinikizo la damu na kuzuia ugonjwa wa stroke.

5. Kuchochea Uwezo wa Ubongo (BRAIN POWER)
Wanafunzi 200 wa shule ya Twickenham (Uingereza) walifanikiwa kuongeza uwezo wa bongo zao na kufanya vizuri mitihani yao baada ya kula ndizi wakati wa kifungua kinywa na chakula cha mchana. Utafiti unaonesha kwamba tunda hili lilolosheheni potassium huweza kusaidia kuwafanya wanafunzi kuwa makini zaidi na hivyo kuongeza uwezo wao wa kujifunza.

(nadhani hii ndio siri ya urembo ya wachagga, wanyakyusa na wahaya kufanya vizuri masomoni, chakula kikuu cha makabila haya ni ndizi)

6. Matatizo ya kufunga Choo (CONSTIPATION)
Tunda la ndizi lina nyuzinyuzi kwa wingi sana hivyo kula ndizi pamoja na chakula hurejesha ratiba ya kupata choo kama kawaida kwa wale wenye tatizo la kufunga choo. Ndizi hurahishisha mmeng'enyo wa chakula na kufanya upate choo cha kawaida bila kutegemea dawa za kulainisha choo.

7. HANGOVERS (sijui kiswahili chake)
Njia moja ya haraka sana kutibu hangover ni kunywa mchanganyiko wa ndizi, maziwa na asali (banana milkshake); changanya ndizi moja na glasi moja ya maziwa kwenye blender, ongeza asali. Ndizi hutuliza tumbo na asali hurejesha kwenye damu kiwango cha sukari kilichopotea wakati huohuo maziwa yakituliza na kunyweshea mfumo wako mzima.

8. Kiungulia (HEARTBURN)
kama unasumbuliwa na kiungulia kula ndizi moja ili kupata nafuu. Ndizi zina uwezo wa asili wa kuondoa gesi mwilini.

9. Kutapika wakati wa Ujauzito (MORNING SICKNESS)
Kula ndizi mara kwa mara kabla ya mlo husaidia kuongeza kiwango cha sukari kwenye damu na hivyo kuzuia kutapika mara kwa mara wakati wa ujauzito.

10. Kutafunnwa na Mbu (MOSQUITO BITES):
Kabla ya kupaka dawa zenye kemikali sehemu ulizoumwa na mbu, jaribu kusugua maeneo hayo na sehemu ya ndani ya ganda la ndizi, watu wengi huona mafanikio hasa katika kupunguza uvimbe na kuwasha.

11. Vidonda vya tumbo ULCERS
Kwasababu ya wororo na ulaini wake, ndizi inatumika kama chakula cha diet kutibu matatizo ya utumbo. Hupunguza sana gesi na maumivu ya tumbo.

12. Kudhibiti joto la mwili (TEMPERATURE CONTROL)
Tamaduni nyingi zinatumia ndizi kama tunda la kupoza joto, inaweza kushusha joto mwili na joto la hisia pia (physical and emotional temperature) kwa wajawazito.

Hivyo ndizi ni tunda la asili linalotibu maradhi mengi. Ukiilinganisha na tufaa (apple) ndizi ina mara 4 ya protini, mara 2 ya kabohaidreti, mara 3 ya phosphorous, mara 5 ya vitamini A na madini chuma, mara 2 ya vitamini na madini nyinginezo. Imesheheni pia potashiamu and ni moja ya vyakula vyenye ubora zaidi.

Imetafsiriwa kutoka: After reading this, you’ll never look at a banana in the same way again - World Observer Online

Ongeza faida nyingine unazozijua
 
Back
Top Bottom