Faida ya kitunguu maji katika mwili wa binadamu

Faida ya kitunguu maji katika mwili wa binadamu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,037
Reaction score
34,742
Onion.jpg







Kitunguu maji hutibu magonjwa yafuatayo

Kikohozi

Vidonda vya tumbo

Mifupa

Ngozi

Koo

Figo

Tumbo

Mkojo

Matayarisho

Menya vitunguu maji 3 vikubwa, visage au vitwange ili upate maji yake, changanya na maji kidogo yaliyochemka. Chukua punje 3 za Kitunguu Swaumu, mwaga maji ya vitunguu maji juu yake acha mchanganyiko ukae ndani ya bilauri masaa 2, ongeza asali vijiko vikubwa 5.

Tumia kijiko kikubwa kimoja kutwa mara 2 kwa siku 3 au siku 7 inategemea ugonjwa wako jinsi ulivyo na ukubwa wake.

Ukiwa na Shida yoyote ile
Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe.fewgoodman@hotmail.com What's App +905344508169 Au Ni add Kwa Facebook tumia jina hili mzizimkavu. Au boonyeza hapa.Mzizi Mkavu


========

Faida ya kujitibu kutokana na kitunguumaji, tiba inayopatikana katika Kitunguumaji Kitunguumaji ni aina ya mboga ya yungiyungi.

Ni mboga yenye harufu kali inayochangamsha. Anaeikitumia kitunguu maji ajihadhari kukitumia baada ya kukihifadhi kikiwa kimekatwakatwa, kwasababu hufanya oksaidi (oxide) na huwa kiini chenye sumu. Kwa hivyo yatakiwa kitumiwe kikiwa fresh.

Imethibitiswa kisayansi kuwa juisi yake huuwa vijidudu vya kinamasi na vya kifua-kikuu, huuwa baada tu ya kunusa moshi wake. Nchi mashuhuri duniani katika upandaji wa kitunguumaji ni Misri (Egypt).

Razi amesema: "Kitunguu maji kikifanyiwa achari, ukali wake hupungua na hutia nguvu maida, na kitunguu kilichofanywa achari, hufungua mno hamu ya kula" Kwa ajili hiyo watu wa misri hula ktunguumaji kikiwa kimechomwa, hutia nguvu mwilini, huufanya uso kuwa mwekundu na huimarisha misuli. Ibn Baitar amesema: "

Kitunguu maji hufungua hamu ya kula, hulainisha tumbo. Kikipikwa hukojoza na huzidisha nguvu za kiume kikichemshwa. Na kinachokata harufu ya kitunguumaji ni lozi (almond). Al-Antaky amesema kuhusu kitunguu maji:"Hufungua vizuizi mwilini, hutia nguvu za shahawa kwa mwanamke na mwanaume mbili (ya kula na na kujamii) hasa kikipikwa kwa nyama, pia huondoa homa manjano (jaundice) hukojoza na kumimina hedhi pamoja na kuvunja vijiwe tumboni".

Katika gazeti moja huko Ufaransa liitwalo "Everything" (Kila kitu) limeelezea kuwa daktari mmoja aliwatibu wagonjwa kwa kuwapiga sindano (ya kitunguumaji) wagonjwa wengi waliokuwa na saratani (cancer) na akapata matokea mazuri.

Viini vyenye athari nzuri katika kitunguu maji ni Vitamin C (antiseptic) inayozuia kukua kwa bakteria (bacteria) kwenye jeraha, ngozi n.k pia hutia nishati homoni (hormones) wa nguvu za kiume, kiini cha insulini (insuline, itumikayo kutibu wagonjwa wa kisukari).

Kwa hivyo kitunguu maji ni katika dawa yenye kuwatibu wagonjwa wa kisukari, ndani yake mnapatikana salfa, chuma na vitamini zinazotia nguvu mishipa.

Vilevile hupatikana viini vyenye kukojoza, kutoa safura na vyenye kutia nishati moyo pamoja na mzunguko wa damu mwilini.

Pia imethibitishwa kuwa katika kitunguu maji muna vijiuasumu vyenye nguvu zaidi kuliko penesilini (penicillin) kwahivyo hupoza kifua kikuu, kaswende (syphillis) na kisonono (gonorrhea), na huua aina ya vijidudu vingi vya hatari.

Pamoja na kuwa tunaamini kuwa maisha ya mwanaadam yote yamo katika mikono ya Allah S.W, lakini imethibitishwa kuwa wale watumiaji wa vitunguu maji zaidi huwa na umri mrefu pia huepukana na maradhi ya saratani na kifua kikuu.

Mwandishi wa kitabu cha tiba zinazotokana na kitunguu maji yeye amekiita kitunguu maji ni " mpira wa dhahabu" kwakuwa ndani yake muna manufaa mengi yenye utajiri wa afya. Kutakasika ni kwa Allah mwenye kuneemesha peke yake.

MARADHI YANAYOTIBIWA NA KITUNGUU MAJI

Pumu: Changanya juisi ya kitunguu maji na asali halafu kunywa kiasi cha kikombe kimoja, asubuhi na jioni. Endelea hivyo kwa muda wa mwezi mmoja.

Uvimbe wa pafu (Pneumonia): Weka kibandiko cha kitunguu maji juu ya kifua na mgongo pamoja na kufunga kwa kitambaa, fanya hivyo kila siku kabla ya kulala.

Maradhi ya kinafsi: Chemsha kitunguu na maganda yake, baadae mgonjwa wa kinafsi ale, au chukua juisi ya kitunguu maji na juisi ya saladi (lettuce) na kijiko kimoja cha asali changanya vyote ndani ya blenda na baadae unywe.

Saratani(Cancer): Kausha maganda ya kitunguumaji kwenye jua, yasage na kiasi cha magamba hayo chukua magamba ya muoka (muoki, maloni, oak) halafu yakande katika asali na chukua na uchanganye katika juisi ya karoti (carrot) na unywe kiasi ya kijiko kimoja kwa muda wa mwezi mzima mfululizo,na baadae uvute moshi wa kitunguu maji kabla ya kulala.

Vidonda ya saratani: Chukua juisi ya kitunguumaji kiasi cha kikombe,chukua na kiota (kiwawi, nettle) kamua majani yake kiasi cha kijiko kimoja na ongezea juisi ya kitunguu na halafu chukua hina iponde ndani yake ili ipate kuwa marhamu inayopakwa katika vidonda; fanya hivo kila siku pamoja na kunywa juisi ya kitunguu maji iliyochanganywa na juisi ya kiota kijiko kimoja kidogo na baada ya hapo kunywa kikombe kimoja cha maziwa.

Mvilio wa damu (Bruise): Changanya juisi ya kitunguu maji pamoja na kiasi cha mafuta ya kafuri, sugua mahala pa mvilio asubuhi na jioni.

Majipu: Saga kitunguu maji na kikange katika mafuta ya zaituni bila ya kuwa rangi ya manjano, paka kama marhamu na funga bendeji juu yake. Kila siku ukibadilisha pamoja na kusafisha utokaji wa usaha umalizike, halafu utakuwa ukitumia habasouda.

Chunusi: Chukua kitunguu maji kisha ukisage, halafu ukikande katika unga wa ngano nzima, changanya na yai pamoja na mafuta ya simsim(ufuta) na upake usoni asubuhi na jioni pamoja na kula kitunguu kwa sana.

Ukurutu (Eczema): Chukua juisi ya kitunguu na nanaa (mint) vipimo sawa,tengeneza kama krimu (cream) na ujipake baadae pangusa ukurutu kwa maji ya siki nyepesi, rudia kila siku pamoja na kujiepusha na kila kinachochea hisia. Kula matunda,mboga na asali kwa wingi.

Saratani ya ngozi: Chukua juisi ya kitunguu maji, uwatu uliosagwa na salfa manjano kiasi cha robo kijiko kidogo; tengeneza marhamu jipake kila siku. Baada ya kuosha jioni jipake mafuta ya zetuni endelea hivyo kwa muda wa wiki.

Mgonjwa wa figo na vijiwe: Chukua kitunguu bila kukichambua, tia mbegu ya tende baada ya kuichoma kama vile buni na kuisaga; halafu kila siku kula kimoja kula kimoja kwa muda wa wiki.

Kikohozi kwa wakubwa na wadogo: Saga kitunguu kitie ndani ya kikombe cha asali; iwache kwa muda wa masaa matatu (3) kisha uisafishe. Kula kiasi cha kijiko kimoja kila baada ya chakula.

Kisukari (Diabetes): Kila siku kula kitunguu. Sukari itashuka na baadae kula mzizi wa kabichi (cabbage).

Maradhi ya macho: Chukua maji ya kitunguu na asali vipimo sawa halafu ujipake jichoni (kama unavyojipaka wanja) , (dawa hii naamini ni dawa bora kwa maradhi ya macho yote nakuambuka marehemu bibi yangu alikuwa akiwatibu wagonjwa wenye mtoto wa jicho kwa kutumia dawa hii) jipakae jichoni kwa kutumia glassrod au kama huna kifaa hicho unaweza kutumia nyoya la kuku au ndege yoyote.

Kikohozi: Chemsha maji ya kitunguu maji na asali kunywa kijiko kimoja kila baada ya kula na weka kibandiko cha kitunguu maji juu ya kifua na majani yake kwa bendeji kabla ya kulala. Kufungua choo: Chambua kitunguu, tia katika maziwa na kunywa.

Kutia nguvu na nishati: Choma kitunguu pamoja na maganda yake halafu kichambue na ukikande katika asali na samli,weka katika mkate wa ngano nzima kama vile sandwich. Kula wakati wa chakula cha asubuhi na unywe maziwa nusu lita.

Kupunguza uzito: Kwa anaetaka kufurahi mwili wake uwe mzuri na mwepesi, kuyayusha mafuta na kuondoa kitambi na mwili tepwetepwe miongoni mwa wanaume na wanawake basi afwate hivi:

1. Kila siku kunywa maji ya kitunguu maji kiasi cha kijiko kimoja kidogo unaweza kuchanganya katika juisi ya matunda ukanywa.

2. Soma sanakatika masaa ya mwisho wa usiku na kukizingatia ukisomacho (ukisoma Quraan utapata faida 2 kwa wakati mmoja, moja ya hapa duniani na moja ya huko tunapokwenda akhera) pia usile chakula cha usiku isipokuwa maziwa ya mgando kikombe kimoja, au matunda.

3. Tembea sana na kufanya mazoezi kwa wingi.
 
Wakuu najua labda limeshazunguzwa hili please naomba details.

View attachment 39580





Wiki iliyopita tulianza makala haya kwa kuangalia jinsi kitunguu kinavyoweza kutibu ugonjwa wa kutokwa damu wakati wa kutoa haja kubwa. Katika makala hayo, watu wengi wameonekana kuguswa nayo. Wiki hii, pamoja na mambo mengine, nitakujuza jinsi ya kuitengeneza juisi hiyo.
 
Huoni kwamba kesho atakuja mwingine kudai umuhimu na madhara ya mapera, zambarau, kitunguu saumu, maembe, mapapai, chumvi, asali, majani ya chai, biringanya, pilipili hoho, pilipili kichaa na mengine mengi?
Kuna vitu unaweza google na ukapata maelezo ya kujitosheleza.
Tafakari,chukua hatua.
 
kitunguuu.jpg

Wiki iliyopita tulianza makala haya kwa kuangalia jinsi kitunguu kinavyoweza kutibu ugonjwa wa kutokwa damu wakati wa kutoa haja kubwa. Katika makala hayo, watu wengi wameonekana kuguswa nayo. Wiki hii, pamoja na mambo mengine, nitakujuza jinsi ya kuitengeneza juisi hiyo.

Halikadhalika katika makala ya leo, utajua magonjwa mengine yanayoweza kutibika kwa kitunguu, iwe kwa kunywa juisi yake au kwa kula kitunguu chenyewe. Kitu kimoja napenda kukuhakikishia kuwa, unayoyasoma hapa kuhusu kitunguu, tayari yalishafanyiwa utatifi na kuthibitishwa na wataalamu waliobobea katika masuala ya vyakula tangu enzi za mababu zetu.

Vile vile, watu wanaoamini lishe kama tiba na kutumia, matokeo yake siku zote huwa dhahiri na wako wengi wanaoweza kuthibitisha jinsi afya zao zilivyo imara leo tofauti na miaka kadhaa iliyopita kabla ya kugundua siri ya chakula kama tiba.

JINSI YA KUTENGENEZA
Kinachotakiwa ni kitunguu maji kimoja cha ukubwa wa wastani ambacho utatengenezea juisi na kupata kiasi cha glasi moja saizi ya kati. Safisha kitunguu chako kwa kuondoa gamba la juu kisha katakata vipande vidogo vidogo ili kurahisisha usagaji.

Kuna njia mbili unazoweza kuzitumia kutengeneza juisi hiyo. Ya kwanza ni ya kisasa ambapo unaweza kutumia blender au juicer, kwa kuweka maji kidogo na kuanza kuisaga hadi kupata juisi. Njia ya pili ni ya kiasili, ambapo utatumia kinu kidogo na maji kidogo kwa kutwangwa hadi kupata juisi.

Ukimaliza kusaga (kwa njia utakayoitumia) kamua na ichuje juisi yako kwa kutumia chujio la kawaida ili kupata juisi pekee ya kitunguu na kuacha masalia ya maganda peke yake. Mara baada ya kuiweka juisi yako kwenye glasi, HAKIKISHA UNAINYWA HAPO HAPO. Hairuhusiwi kuihifadhi au kuinywa baadaye, kwa sababu itapoteza virutubisho vyake muhimu.

Kunywa glasi moja mara moja kwa siku au mara mbili, ukiona tatizo lako ni kubwa. Fanya zoezi hilo la kundaa juisi na kuinywa kwa muda wa siku saba hadi 14.
Kama nilivyoeleza wiki jana, hali ya kuchafuka kwa tumbo na kujisikia vibaya baada ya kunywa, isikuogopeshe, baadaye utaizoea na utajisikia vizuri zaidi.

Mbali ya kutibu tatizo la kusikia maumivu na kutokwa na damu wakati wa kwenda haja kubwa (Hemorrhoids au piles), juisi hiyo pia itatoa ahueni au kinga kubwa dhidi ya matatizo mengine ya kiafya yafuatayo:
Pumu, mafua, magonjwa ya kuambukizwa na bakteria, matatizo ya kupumua kwa shida, kiungulia na kutapika.

Itaongeza kinga ya mwili dhidi ya magonjwa nyemelezi, vile vile kwa kutafuna vitunguu vibichi na kukaanavyo mdomoni kwa sekunde kadhaa, kutaua bakteria wote wa kinywani na kutoa kinga dhidi ya kuoza kwa meno na kuondoa harufu mbaya.

Ulaji wa vitunguu maji vibichi mara kwa mara, hulainisha damu na kuzuia kuganda ambako husababisha mishipa kuziba na kusababisha magonjwa ya moyo, ikiwemo presha ya kupanda.

Juisi ya kitunguu ni dawa mara moja ya kuzuia kutapika, mtu anayetapika mfululizo akinywa juisi ya kitunguu, hupata nafuu haraka. Vile vile juisi hii ni dawa ya tumbo linalouma na hutoa kinga dhidi ya magonjwa ya uvimbe tumboni.

Kama unasumbuliwa na chunusi, pakaa juisi ya kitunguu iliyochanganywa na asali sehemu yenye chunusi vitaondoka na kukuacha na ngozi nyororo. Chukua kiasi kidogo cha juisi na kijiko kimoja kidogo cha asali changanya kisha pakaa.

Juisi ya kitunguu pia ni dawa ya kutibu majeraha ya kuumwa na nyuki. Kama unapata maumivu wakati wa haja ndogo au unatoa mkojo mchafu sana, kunywa maji mengi yaliyochanganywa na juisi ya kitunguu kiasi kidogo, tatizo litakwisha.

Juisi ya kitunguu ina virutubisho vyenye uwezo wa kudhibiti chembechembe hai za mwili zenye kansa na hivyo kuwa kinga nzuri dhidi ya ugonjwa wa saratani (cancer).

Ulaji wa vitunguu au juisi pia hutoa ahueni kwa mgonjwa wa kifua kikuu. Juisi iliyopashwa moto pia ni dawa ya sikio linalouma. Weka matone mawili tu kwa kila sikio linalouma.

Juisi ya kitunguu pia ni dawa ya majeraha yatokanayo na moto. Ukiungua, pakaa juisi hiyo sehemu zilozoungua kwa nafuu ya haraka. Pia kitunguu ni dawa ya mbu, pondaponda vitunguu, kisha jipakae sehemu za miguu na mikono - mbu hawatakugusa.

Faida za kitunguu na juisi yake ziko nyingi na zote ni muhimu kwa ustawi wa afya zetu. Nakushauri kuanzia leo, kunywa juisi hiyo au kula kitunguu katika kila mlo kwa jili ya kutibu maradhi uliyonayo au kwa kuupa mwili wako kinga imara, na kamwe hutajuta!
 
Wiki iliyopita tulianza makala haya kwa kuangalia jinsi kitunguu kinavyoweza kutibu ugonjwa wa kutokwa damu wakati wa kutoa haja kubwa. Katika makala hayo, watu wengi wameonekana kuguswa nayo. Wiki hii, pamoja na mambo mengine, nitakujuza jinsi ya kuitengeneza juisi hiyo.
 
Hii nimeona sehemu moja nilikuwa na raia wa Misri walikuwa wanakula sasa vitunguu sana vibichi..

Na mimi nikawa najaribu mpaka nimezoea saizi kila mlo wangu lazima vitunguu viwepo..tunakuombea dua MziziMkavu
 
Swadacta.... Hakuna shaka hata kidogo. Ukienda India (South India.....Madras, Mysore, Bangalore nk) kila mlo utakuta wanakuwekea na vitunguu kibao wee utafuneee ili upate japo faida hata moja.

Big up!
 
Mzizi mkavu big up,sijui kama ulisha wahi kutaja tiba ya presha ya kupanda kama ulishawahi mimi ilinipita.

mimi nilikuwa nataka ya kupunguza unene....mzizi ulishaleta hiyo...?.....kama bado hebu nitupie......
 
Mzizi mkavu big up,sijui kama ulisha wahi kutaja tiba ya presha ya kupanda kama ulishawahi mimi ilinipita.

Dawa ya pressure kwa jumla (imewafaa watu wengi), ni majani ya mbaazi

>yaliokua bado machanga. Chukua kiasi majani 4 mpaka matano hivi na

>utafune tafune huku unameza mate, kisha majani yatupe baadae, usimeze.

>Tumia kwa muda wa

> siku mbili au tatu hivi na baadae ukapime. Inshaallah utahisi

>upungufu mkubwa.

>Usiendelee kutafuna kwa muda wa masiku mengi bila ya kupima, kwani

>huenda pressure ikashuka sana.

>Mwenye ugonjwa huu jaribu kutumia, kwani haina madhara yoyote yale.

>Kuna watu wa karibu sana na mie wametumia na imewafaa sana. Walikua

>vidonge haviwatoki na baadae wakaacha kabisa, mpaka madakitari

>walistaajabu ni dawa gani wametumia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom