Faida ya kitunguu maji katika mwili wa binadamu

Faida ya kitunguu maji katika mwili wa binadamu

Jaribu hii Dawa chukua mafuta ya Habbat-Sawdaa, mafuta ya waridi (marashi jabali) na unga wa ngano asili, vyote hivyo kwa viwango sawa, ule unga wa ngano uwe zaidi kuliko mafuta, halafu aukande vizuri. Kabla ya kujipaka, apanguse sehemu yenye ungonjwa kwa kitambaa kilichoroweshwa siki nyepesi, halafu aketi kwenye jua, baadae ajipake dawa hio kila siku.
Nashukuru Nitakujulisha matokeo
 
Humu ndani tuna mpaka mabingwa wa mabingwa yani akisikika MwanaJF amekufa kwa uzembe yani ni shauri yake,anika ugonjwa wako na utapata matibabu mara moja!

Kweli mkuu, jamaa anatufaa ktk dhiki, ni rafiki a kweli.
 
Kama ni sumu basi mie ningekuwa nimeaga dunia siku nyingi! maaba ndio dawa yangu kubwa sana ya kupunguza uzito.
 
Thanx mkuu! Mzizimkavu, mimi tatizo langu ni low constipation, yaani hadi maumivu wakati wa ile kubwa. Sasa hapa naanza dozi mara moja!!
 
Mkuu mimi tatizo langu ni ugonjwa wa ngozi ni wasiku nyingi,nimetumia dawa nyingi za hospitali bila mafanikio unaacha halafu unarudia.Unakuwa kama m-ba sugu kichwani na usoni.Ningeomba msaada wako mkuu.
 
Mkuu mimi tatizo langu ni ugonjwa wa ngozi ni wasiku nyingi,nimetumia dawa nyingi za hospitali bila mafanikio unaacha halafu unarudia.Unakuwa kama m-ba sugu kichwani na usoni.Ningeomba msaada wako mkuu.
Mbaa hutokana na ngozi iliyokufa katika kichwa yaani dead cell.

Dawa zilizopo ni :


Ndimu au limau: Kabla kwenda kukoga jisugue limau ndani ya kichwa na baadae yale maganda ya limau yatie katika maji ya kukoga yaani yawe Uvuguvugu halafu ukoshe kwa maji yale kwanza na baadae utumie maji yaliyo safi.

(Uwatu) kwa kiingereza inaitwa (Fenugreek) Hii unachukua vijiko 2 vya chai vya (fenugreek) unazirowesha katika maji usiku mzima ili zipate kulainika, halafu unazipoda ponda na baadae unapakaa ndani ya kichwa na uwache kwa muda wa saa moja na baadae kuzikosha ikiwa utafanya hivi siku zote mbaa wataondoka Inshallah bila tabu yoyote.

Au tumia Dawa hii Mafuta ya Habbat Sauda Kwa kiingereza inaitwa
(Nigella Sativa oil)na Mafuta ya Nazi. Kinachotakiwa Kufanya ni kuwa Wakati ukienda Kuoga Kichwani Yakupasa Uoshe nywele kwa maji Ya uvugu vugu kisha Ukifute kichwa Uzuri sana kiasi Kisibakiwe na Maji maji mengi, Ila nywele ziw zimelainika tu!..
Kisha Unachukua Mafuta ya Nazi
(coconut oil) then unaichanganya na Mafuta ya Habbat Sauda kwa lugha ya kiingereza inaitwa ( Nigella sativa oil) . kisha unajipakaa kichwani mafuta ya kutosha . Asubuhi na usiku.
 
mimi nilikuwa nataka ya kupunguza unene....mzizi ulishaleta hiyo...?.....kama bado hebu nitupie......

Duuuh!!! kumbe nawe BONGE ila angalia usije ukatumia ya mzizi kupita kiasi ukasinyaa kupitiliza ukawa zaidi hata ya wale wanaoshinda na njaa wenyewe wanajiita sijui ni ma-- m-c sjui vile.
 
Thanx mkuu! Mzizimkavu, mimi tatizo langu ni low constipation, yaani hadi maumivu wakati wa ile kubwa. Sasa hapa naanza dozi mara moja!!
Kuna Watu wengi wana mushkila wa Qabz ya tumbo (Constipation) kwa kiswahili kukosa kufanya haja kubwa. Kuna sababu tofauti:

1- Kukosa kunywa maji
2- Kukosa kula kwa wakti
3- Kukosa kula vyakula vya maana
4- Kukosa kwenda chooni wakati unapojihisi unataka kwenda na kujizuia.

Na hii husababisha uvivu na viungo kuuma na pia kujiona saa zote unataka kulala.

VIPI KUJITIBU BILA YA KUTUMIA HALULI

1- Kunywa maji gilasi 8 kwa siku
2- Kula kwa wakti wake.
3- Kula vyakula vya maana sio unaokotea tu.
4- Uwende chooni wakati unapojihisi unataka kwenda na usijizuie.
5- Kunywa maji baina ya kila tonge 2 au 3.
6- Kunywa mafuta ya Halzet (Olive Oil) au kutia kwenye chakula kama salad kila siku inasaidia kulainisha tumbo.
7- Kunywa maji kama gilasi 3 au 4 kisha ukawa unakwenda ukirudi kwa muda wa robo saa au dakika 20.
8- Kuchukua chupa ya Tanuf (litre 1 na nusu) na kutia chumvi kidogo kisha ukaichanganya sawa sawa halafu ukainywa yote kwa pamoja na hii mtu akifanya mwezi mara moja kwani kama haluli.
9-Kila Asubuhi na usiku - gilasi ya maji ya moto moto utachanganya na kijiko kikubwa cha asali na utakunywa.
10-Haba Sawda utasaga na uchanganye na asali na uwe unakula kijiko asubuhi kijiko usiku kila siku.
11- Fruits - Papai , Embe, Machungwa na kama unaweza ule maganda meupe.
12- Kwa watoto wadogo - juice ya chungwa - sukari na maji - asali na maji moto moto.
 
Sawa mkuu ila inaonesha ugonjwa wangu ukondani kwasababu nikitumia dawa za kupaka unapona ila unarudia nikiacha.
 
View attachment 39580





Wiki iliyopita tulianza makala haya kwa kuangalia jinsi kitunguu kinavyoweza kutibu ugonjwa wa kutokwa damu wakati wa kutoa haja kubwa. Katika makala hayo, watu wengi wameonekana kuguswa nayo. Wiki hii, pamoja na mambo mengine, nitakujuza jinsi ya kuitengeneza juisi hiyo.

Halikadhalika katika makala ya leo, utajua magonjwa mengine yanayoweza kutibika kwa kitunguu, iwe kwa kunywa juisi yake au kwa kula kitunguu chenyewe. Kitu kimoja napenda kukuhakikishia kuwa, unayoyasoma hapa kuhusu kitunguu, tayari yalishafanyiwa utatifi na kuthibitishwa na wataalamu waliobobea katika masuala ya vyakula tangu enzi za mababu zetu.

Vile vile, watu wanaoamini lishe kama tiba na kutumia, matokeo yake siku zote huwa dhahiri na wako wengi wanaoweza kuthibitisha jinsi afya zao zilivyo imara leo tofauti na miaka kadhaa iliyopita kabla ya kugundua siri ya chakula kama tiba.

JINSI YA KUTENGENEZA
Kinachotakiwa ni kitunguu maji kimoja cha ukubwa wa wastani ambacho utatengenezea juisi na kupata kiasi cha glasi moja saizi ya kati. Safisha kitunguu chako kwa kuondoa gamba la juu kisha katakata vipande vidogo vidogo ili kurahisisha usagaji.

Kuna njia mbili unazoweza kuzitumia kutengeneza juisi hiyo. Ya kwanza ni ya kisasa ambapo unaweza kutumia ‘blender’ au ‘juicer’, kwa kuweka maji kidogo na kuanza kuisaga hadi kupata juisi. Njia ya pili ni ya kiasili, ambapo utatumia kinu kidogo na maji kidogo kwa kutwangwa hadi kupata juisi.

Ukimaliza kusaga (kwa njia utakayoitumia) kamua na ichuje juisi yako kwa kutumia chujio la kawaida ili kupata juisi pekee ya kitunguu na kuacha masalia ya maganda peke yake. Mara baada ya kuiweka juisi yako kwenye glasi, HAKIKISHA UNAINYWA HAPO HAPO. Hairuhusiwi kuihifadhi au kuinywa baadaye, kwa sababu itapoteza virutubisho vyake muhimu.

Kunywa glasi moja mara moja kwa siku au mara mbili, ukiona tatizo lako ni kubwa. Fanya zoezi hilo la kundaa juisi na kuinywa kwa muda wa siku saba hadi 14.
Kama nilivyoeleza wiki jana, hali ya kuchafuka kwa tumbo na kujisikia vibaya baada ya kunywa, isikuogopeshe, baadaye utaizoea na utajisikia vizuri zaidi.

Mbali ya kutibu tatizo la kusikia maumivu na kutokwa na damu wakati wa kwenda haja kubwa (Hemorrhoids au piles), juisi hiyo pia itatoa ahueni au kinga kubwa dhidi ya matatizo mengine ya kiafya yafuatayo:
Pumu, mafua, magonjwa ya kuambukizwa na bakteria, matatizo ya kupumua kwa shida, kiungulia na kutapika.

Itaongeza kinga ya mwili dhidi ya magonjwa nyemelezi, vile vile kwa kutafuna vitunguu vibichi na kukaanavyo mdomoni kwa sekunde kadhaa, kutaua bakteria wote wa kinywani na kutoa kinga dhidi ya kuoza kwa meno na kuondoa harufu mbaya.

Ulaji wa vitunguu maji vibichi mara kwa mara, hulainisha damu na kuzuia kuganda ambako husababisha mishipa kuziba na kusababisha magonjwa ya moyo, ikiwemo presha ya kupanda.

Juisi ya kitunguu ni dawa mara moja ya kuzuia kutapika, mtu anayetapika mfululizo akinywa juisi ya kitunguu, hupata nafuu haraka. Vile vile juisi hii ni dawa ya tumbo linalouma na hutoa kinga dhidi ya magonjwa ya uvimbe tumboni.

Kama unasumbuliwa na chunusi, pakaa juisi ya kitunguu iliyochanganywa na asali sehemu yenye chunusi vitaondoka na kukuacha na ngozi nyororo. Chukua kiasi kidogo cha juisi na kijiko kimoja kidogo cha asali changanya kisha pakaa.

Juisi ya kitunguu pia ni dawa ya kutibu majeraha ya kuumwa na nyuki. Kama unapata maumivu wakati wa haja ndogo au unatoa mkojo mchafu sana, kunywa maji mengi yaliyochanganywa na juisi ya kitunguu kiasi kidogo, tatizo litakwisha.

Juisi ya kitunguu ina virutubisho vyenye uwezo wa kudhibiti chembechembe hai za mwili zenye kansa na hivyo kuwa kinga nzuri dhidi ya ugonjwa wa saratani (cancer).

Ulaji wa vitunguu au juisi pia hutoa ahueni kwa mgonjwa wa kifua kikuu. Juisi iliyopashwa moto pia ni dawa ya sikio linalouma. Weka matone mawili tu kwa kila sikio linalouma.

Juisi ya kitunguu pia ni dawa ya majeraha yatokanayo na moto. Ukiungua, pakaa juisi hiyo sehemu zilozoungua kwa nafuu ya haraka. Pia kitunguu ni dawa ya mbu, pondaponda vitunguu, kisha jipakae sehemu za miguu na mikono - mbu hawatakugusa.

Faida za kitunguu na juisi yake ziko nyingi na zote ni muhimu kwa ustawi wa afya zetu. Nakushauri kuanzia leo, kunywa juisi hiyo au kula kitunguu katika kila mlo kwa jili ya kutibu maradhi uliyonayo au kwa kuupa mwili wako kinga imara, na kamwe hutajuta!
Asante sana mkuu. vipi kuhusu kitunguu saumu, kikitafunwa au juice yake ina saidia nini kiafya?
 
Asante sana mkuu. vipi kuhusu kitunguu saumu, kikitafunwa au juice yake ina saidia nini kiafya?

Faida za Kiafya za Kitunguu Swaumu (Garlic) Featured


1 garlic .jpg
Kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambayo kwa kitaalamu huitwa Allium sativum. Jamii hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita. Matumizi makuu nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba.


Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi mbalimbali yasababishwayo na bakteria, matatizo katika mapafu, matatizo katika mfumo wa umen'genyaji chakula, na matatizo ya kuishiwa nguvu.


Historia inaonesha kuwa, vitunguu swaumu vilianza kutumika China mwaka 510 K.K na pia vilitumiwa na wanajeshi wa Ugiriki na Roma. Aidha wasafiri wa vyombo vya baharini na vijijini pamoja na wakulima barani Afrika walivitumia sana.


Mwaka 1858, mtafiti na mwanasayansi wa nyakati hizo, Louis Pasteur aligundua uwezo wa kitunguu swaumu katika kuua vimelea mbalimbali vinavyosababisha magonjwa, na hivyo vikaanza kutumika kama dawa ya kusafishia vidonda na kuzuia kidonda ndugu hasa zama za vita ya kwanza na pili ya dunia. Isitoshe, mpaka sasa zipo dawa kadhaa zilizotengenewa kwa kutumia jamii hii ya vitunguu swaumu ikiwemo dawa ya kusafisha mdomo (mouth wash) ingawa watumaiji wake wengi huilalamikia dawa hiyo kwa sababu ya harufu mbaya ya dawa hiyo inayowasababishia kunuka kwa mdomo.


Faida za vitunguu swaumu


Katika tafiti mbalimbali vitunguu swaumu vimeonekana kuwa na uwezo wa kutibu maambukizi ya bakteria, fangasi na virusi vya aina mbalimbali. Aidha husaidia kuzuia magonjwa ya moyo ikiwemo kuondoa lijamu katika mishipa ya damu na hivyo kusaidia katika kurekebisha shinikizo la damu. Faida nyingine za vitunguu swaumu ni pamoja na
  • Kutibu saratani ikiwemo saratani ya tumbo na utumbo mkubwa. Tafiti zinaonesha idadi ndogo ya wagonjwa wa saratani katika nchi ambazo wakazi wake wana utamaduni wa kutumia vitunguu swaumu kwa wingi.
  • Vitunguu swaumu husaidia kudhibiti kiwango cha sukari katika damu. Hata hivyo inashauriwa kwamba wagonjwa wa kisukari wanaotumia sindano za insulin wasitumie kitunguu swaumu kwa wingi mpaka watakaposhauriwa na daktari.
  • Huzuia kusanyiko la chembe sahani zinazosaidia kuganda kwa damu (platelet aggregation)
  • Husaidia ufyozwaji wa thiamin, hivyo kusaidia kuepusha mwili na ugonjwa wa beriberi
  • Ina kiasi kikubwa cha vitamini C ambayo husaidia kuzuia ugonjwa wa kiseyeye
  • Hutumika kutibu magonjwa nyemelezi kama toxoplasmosis, hasa kwa watu wenye upungufu wa kinga mwilini.
Ushahidi wa Kitafiti

Katika utafiti uliofanyika nchini Czech ilionekana kuwa matumizi ya vitunguu swaumu yalisaidia sana katika kupunguza kusanyiko la lijamu (cholesterol) pamoja na mafuta yasiyofaa mwilini (low density lipoproteins) katika mishipa ya damu. Aidha, mwaka 2007 BBC iliripoti matumizi ya vitunguu swaumu katika kusaidia kumkinga mtumiaji dhidi ya aina fulani ya mafua iliyosababishwa na virusi. Mwaka 2010, ulifanyika utafiti mwingine ambao ulijumuisha wagonjwa 50 wenye shinikizo la damu sugu ambalo lilikuwa ni vigumu kudhibitiwa hata kwa matibabu yaliyozoeleka ya dawa na njia nyingine. Kama njia ya kuchunguza ufanisi wa vitunguu swaumu katika kutibu shinikizo la damu, baadhi ya wagonjwa hao walipewa vitunguu swaumu wakati wengine walipewa dawa isiyohusika na matibabu ya shinikizo la damu (au placebo). Ilionekana kuwa wale waliopewa vitunguu swaumu kama dawa ya shinikizo la damu walionesha maendeleo mazuri kwa vitunguu swaumu kuweza kushusha vizuri kiwango cha shinikizo la damu, hususani systolic pressure, tofauti na wale waliopewa placebo.


Nini siri ya kitunguu swaumu?


2 garlic.jpg
Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida zilizoainishwa hapo juu ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake wa kiutendaji unatokana na mambo yafuatayo;

  • Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu.
  • Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na kupunguza madhara ya kisukari.
  • Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bateria, na phytoncide ambayo huua fangasi wa aina mbalimbali.
  • Harufu mbaya ya kitunguuu swaumu hutokana na gesi aina ya hydrogen sulfide ambayo inayotolewa baada ya kuvila.
Nini Madhara ya vitunguu swaumu?


Ukiacha faida zake, vitunguu swaumu pia vina hasara na madhara mbalimbali kwa mtumiaji. Madhara hayo ni pamoja na;
  • Harufu mbaya mdomoni ambayo hutokana na kemikali ya AMS (allyl methyl sulfide). Harufu mbaya hii, hata hivyo, yaweza kupunguzwa kwa kunywa maziwa au kunywa maji mengi.
  • Kwa baadhi ya watumiaji, vinaweza kuwaletea mzio au mcharuko mwili (allergies au inflammatory reactions)
  • Kichefuchefu, Kutapika na kuharisha.
  • Huweza kusababisha hatari ya kuvuja damu, kwa sababu huzuia kazi ya seli sahani (platelets) zenye kusaidia kuganda kwa damu kushindwa kufanya kazi yake vizuri, na hususani kwa mama wajawazito, baada ya upasuaji au mara baada ya kujifungua.
  • Huingiliana katika utendaji kazi wake na dawa kadhaa kama vile warfarin, antiplatelets, saquinavir, dawa za shinikizo la damu kwa ujumla hasa calcium channel blockers, na antibiotiki za jamii ya quinolone kama vile ciproflaxacillin.
  • Aidha, vinaelezwa pia kuwa na madhara kwa wanyama jamii ya paka na mbwa.
 
Mzizimkavu mm nasumbuliwa na fangas (fangas wa ikulu) wa kudumu yan nimetumia dawa ya kila aina lakini wapi kama vip nishauri dawa mbadala ambayo nikitumia 2 zitaisha kabisa maana nawashwa balaa
 
Mzizimkavu mm nasumbuliwa na fangas (fangas wa ikulu) wa kudumu yan nimetumia dawa ya kila aina lakini wapi kama vip nishauri dawa mbadala ambayo nikitumia 2 zitaisha kabisa maana nawashwa balaa
hujaniambia wewe ni mwanamke au mwanamme?Nijibu nitakupa ushauri wa kutumia dawa
 
me mwanamke
jaribu kutafuta hii Dawa inaitwa ('DAKESEN' Prickly Heat Powder) uwe unajipaka huko ikulu kila wakati wa kulala huenda inshallah ikakusaidia. Au dawa hii tumia Betamethasone Valerate and Neomycin.
 
mmmh...Mzizi....si ndio hii wanasema limao/ndimu na asali ni sumu....?
Hiyo wanasema tu lakini haina ukweli wowote. Dhana ya kuwa asali na ndimu inatokana na chemical reaction ya asali na citrus (inatoa mapovu ukichanganya hapo hapo, lakini ni kama mapovu ya soda, huisha hapo hapo). Wengine husema eti ukiupiga mzinga wa nyuki kwa ndimu nyuki huwa wakali zaidi, hebu jaribu kuupiga mzinga kwa jiwe uone kama nyuki watakuja kukupongeza na kushangilia ulichowatendea.

Binafsi nimekuwa nikitumia ndimu/limao na asali ku"stabilize" body temperature na kutibu kikohozi wakati wa baridi badala ya chemical cough syrups. Mara nyingi asali kama "base" ukiichanganya na vitu vyengine kama bungo, ukwaju, chungwa, maziwa, haba soda n.k. inatibu magonjwa na kuondoa matatizo mengi ya kiafya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom