Faida ya kitunguu maji katika mwili wa binadamu

Faida ya kitunguu maji katika mwili wa binadamu

[TABLE="class: tborder, width: 100%, align: center"]
[TR]
[TD="class: alt1, bgcolor: #FFFFFF"]Nikweli kuwa sharubati au (juice) ya limao na asali inasaidia kupunguza unene.
Mnaweza pia kusoma hapa kwa maelezo zaidi.
http://www.babyinfocenter.com/remedi...eight_loss.htm

Uhalisia juu ya unene.
Unene unasababishwa na mambo mengi yakiwemo
• Tabia ya ulaji zaidi ya mwili unavyohitaji, mwili baada ya kuchukua hitajii lake huifadhi mabaki kama fat (mafuta) kadili unavyokula zaidi vyakula vya mafuta ndivyo unavyooongeza mafuta.
• Kutofanya mazoezi ya kutosha
• Mfumo wa umeng’enyaji chakula kutofanya kazi vizuri
• Kula vyakula vinavyozozolotesha uharakishwaji wa mfumo wa umeng’enywaji kama maziwa au nyakati za usiku. au kupenda kunya maji ya baridi baada ya chakula N.k

Asali na limao zote zinakemikali itayokusaidi kurahisisha umeng’enywaji kufanyika haraka hivyo utaweza kusikia njaa baada ya muda Fulani (huenda ikawa ni mapema kuliko kawaida). Ikiwa utaendelea kula kila usikiapo njaa tiba hii haiwezai kukusaidia lolote.

Nilazima wakti Fulani tumbo lako liwe
tupu ili mwili utumie ziada ya chakula ulichohifadhi kama fat (mafuta).
Pia juice ya limao na asali zote zinasaidia kuifanya fati iliyopo mwilini mwako kutumika, utakuwa unajisikia njaa zizuie kula kila mara pia zizuie kula vyakula nyenye fati nyingi kama chipsi nyama choma ya mbuzi , supu etc

Faida nyingine ya juce ya limao na asali zinasaidia kuuwa bacteria ambao kwa namna moja au nyingie wanadhorotesha mfumo wa chakula na utoaji taka kufanya kazi vizuri. Kuvisaidia kufanya kazi vizuri kunya maji ya kutosha ikiwezekana ya vuguvugi.

Hitimisho
Tujiepushe kujiua kwa kujijengea kuwa na tabia ya kula vyakula vya mafuta bila kufanya kazi au mazoezi ambayo hupunguza mafuta mwilini. Zamani watu wengi walikuwa wanona unene ni sifa hata ukisia mtu akisema ‘umependeza umekuwa mnene’. Lakini ukweli ni kuwa unene umuweka mtu ktk mazingira hatarishi ya magonjwa malimabali ya viungo vya ndani kama Moyo, kuziba kwa mishipa ya damu, etc.

Tafit zianaonesha kuwa mafuta mwilini ni kama vichaka vya virusi na bacteria mbalimbali kujificha inakuwa ngumu kwa chembe nyeupe za damu (ambazo hujulikana kama askri wa mwili) kufikia na kuwaua.
Jiadhali na tabia hatarishi………punguza mafuta unapopika, usile vitu vingi vya sukari kwa siku, fanya mazoezi, kunywa maji ya kutosha, juepushe kujaza tumbo unapokula acha nafasi.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
heko mkuu ujumbe umefika tukishindwa ni ss wenyewe mana tiba zingine ni rahisi mno na kila cku tunazipiga mateke mitaani na njiani tunataka tuende kwa wataalamu wakatukamue mapesa mengi bila sababau za msingi kisha tunajiona wajanja
 
"THE GREATEST EXPERIENCE IS TO MEET YOURSELF AND FALL IN LOVE WITH YOURSELF" Hii imepitwa na wakati lete nyingine.Umeonaa eheeee!!!!
 
Nilisikia ulaji wa vitunguu husababisha minyoo mwilini...vipi hapo kuna ukweli wowote? tupe ufafanuzi mkuu.
 
Mzizimkavu mie naomba msaada maana tatizo nililona hata sijui ni nini, maana nina kama ukurutu miguuni, ambao huwa unawasha wakati mwingine, ambako huko kuwasha huwa kuna endelea na kunisababishia kujikuna saana nafuu yangu huwa ni endapo sehemu ninyojikuna itatoa kama kiuvimbe hivi ambacho nitakitoboa na kutoa vitu kama maji basi hapo ndo ahueni yangu, tafadhali saidia
 
Mzizimkavu mie naomba msaada maana tatizo nililona hata sijui ni nini, maana nina kama ukurutu miguuni, ambao huwa unawasha wakati mwingine, ambako huko kuwasha huwa kuna endelea na kunisababishia kujikuna saana nafuu yangu huwa ni endapo sehemu ninyojikuna itatoa kama kiuvimbe hivi ambacho nitakitoboa na kutoa vitu kama maji basi hapo ndo ahueni yangu, tafadhali saidia

Jaribu hii Dawa chukua mafuta ya Habbat-Sawdaa, mafuta ya waridi (marashi jabali) na unga wa ngano asili, vyote hivyo kwa viwango sawa, ule unga wa ngano uwe zaidi kuliko mafuta, halafu aukande vizuri. Kabla ya kujipaka, apanguse sehemu yenye ungonjwa kwa kitambaa kilichoroweshwa siki nyepesi, halafu aketi kwenye jua, baadae ajipake dawa hio kila siku.
 
Nilisikia ulaji wa vitunguu husababisha minyoo mwilini...vipi hapo kuna ukweli wowote? tupe ufafanuzi mkuu.
Ukila kwa wingi Vitunguu maji husababisha Gesi tumboni sio Minyoo. Unakula vitunguumaji vyekundu wakatim unakula chakula kama Salata tu sio kula kila wakati kwanza vitunguu vinatoa harufu mbaya mdomoni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom