mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,664
- 18,040
Nianze kwa kutoa pongezi ya dhati maana kulipwa asilimia 0.156 ya tulichokuwa tunadai si haba! Lakini LA maana zaidi ni yale maboresho mbele ya safari!
Lakini kuna mtego mbaya kwenye haya makubaliano! Sijui kama hilo limewekwa sawa. Unaposema mtagawana faida nusu kwa nusu maana yake ni kuwa hata hasara mtagawana nusu kwa nusu! Vinginevyo iwekwe wazi kuwa faida tutagawana sawa ila hasara itabebwa na mwekezaji, kitu ambacho mwekezaji si rahisi kukikubali maana hakiendani na logic!
Ikumbukwe kuwa wameahidi kugawana faida ambayo mpaka sasa kwa mujibu wa CAG hawajawahi kuipata ndio maana hawajawahi kulipa kodi itokanayo na faida! Ila miaka yote "vitabu" vyao huonyesha wamepata "hasara" kubwa tu! Kwa hiyo kama haya makubaliano yakawa "back-dated" tangu walipoanza kuchimba dhahabu, hakuna hata senti moja ya faida ambayo tutagawana, ila kuna mamilioni ya dola ya hasara ya kugawana pia!
Labda waanze kuzalisha faida kuanzia Leo, vinginevyo tutegemee kugawana hasara badala ya faida!
Kitakachotokea tusipoliweka hili sawa ni kuwa tutajikuta tumepelekana mahakamani tutakapogoma kugawana hasara wakati tulikubali kugawana faida! Mahakama itatafsiri kwa logic tu kuwa kama faida tunafaidi nusu kwa nusu maana yake ni kuwa na hasara tufaidi nusu kwa nusu! Hapo ndipo ile sh. bilioni 700 itakapotutokea puani maana hasara "itatengenezwa" kubwa kuliko hiyo!
Angalizo: Iwepo sentensi kabisa inayosema " tutagawana faida tu lakini hasara ni mzigo wa mwekezaji". Huo mtego tukiutegua mapema nina uhakika watakataa na majadiliano yataanza upya!