Faida tutagawana nusu kwa nusu: Mtego ni kuwa hata hasara tutalazimika kugawana nusu kwa nusu!

hawajawah kupata hasara barrick sema faida ilikuwa inaliwa na wachach hqkuna aliyeweza kusema zaid ya kuwatetea lkn sasa kuanzia management tutakuwepo tutaona kila kitu nampongeza rais wetu jwa kweli hakuna mfano africa.
 
Kwa hiyo ripoti ya CAG si ya kweli! Maana imesema wazi kuwa hawajawahi kulipa kodi inayotokana na faida maana hawajawahi kupata faida! Zitafute ripoti za CAG kwenye mtandao ujiridhishe japo nahisi una uvivu wa kusoma na kufuatilia ndio maana unapinga hata kitu kilicho wazi!
Msingi wa madai ya malimbikizo ya kodi uliofanywa na TRA kwa Acacia unatokana na sisi kudai kuwa walipata faida lakini wao wakadai walipata hasara hivyo kutokulipa kodi!
Kupata hasara au faida ni mahesabu ya wahasibu tu hata wewe kwenye kazi zako ukitaka kupata hasara unaweza ukapika hesabu zako ili uripoti faida au hasara kulingana na malengo yako.

Kama usimamizi ni mbovu ni kweli kila siku utakutana na hasara. Hiyo ripoti ya CAG haina hata chembe ya uongo ni kweli wanacheza tu na uzembe wa mfumo wetu na sheria za uwekezaji na mitaji iliyotumika ambayo inakuwa Amortized (inagawanywa kama matumizi) kwa kipindi kirefu na unakuta wakati mwingine hiyo mitaji haikuwahi hata kuwekezwa hapo migodini.
 
Ficha ujinga wako basi....

Ni bora title ungeweka swali ukaeleweshwa na wataalam wa fedha.

Hasara inaleta athari kwenye mtaji na faida inaleta tija kwenye malipo ya mwekezaji na kukua kwa mtaji.

Siku nyingine uliza kwa wanaojua sio kukurupuka tu kama nyumbu
Ficha upumbavu wako mkuu, tangu lini na wapi ukasikia hasara inakua offset na capital? Kama nyie ni sehemu ya uwekezaji lazima mtaumizwa tu na hasara (endapo itatokea) ingawa inakua na limitations (limited liability).
 
Nianze kwa kutoa pongezi ya dhati maana kulipwa asilimia 0.156 ya tulichokuwa tunadai si haba! Lakini LA maana zaidi ni yale maboresho mbele ya safari!

Lakini kuna mtego mbaya kwenye haya makubaliano! Sijui kama hilo limewekwa sawa. Unaposema mtagawana faida nusu kwa nusu maana yake ni kuwa hata hasara mtagawana nusu kwa nusu! Vinginevyo iwekwe wazi kuwa faida tutagawana sawa ila hasara itabebwa na mwekezaji, kitu ambacho mwekezaji si rahisi kukikubali maana hakiendani na logic!

Ikumbukwe kuwa wameahidi kugawana faida ambayo mpaka sasa kwa mujibu wa CAG hawajawahi kuipata ndio maana hawajawahi kulipa kodi itokanayo na faida! Ila miaka yote "vitabu" vyao huonyesha wamepata "hasara" kubwa tu! Kwa hiyo kama haya makubaliano yakawa "back-dated" tangu walipoanza kuchimba dhahabu, hakuna hata senti moja ya faida ambayo tutagawana, ila kuna mamilioni ya dola ya hasara ya kugawana pia!

Labda waanze kuzalisha faida kuanzia Leo, vinginevyo tutegemee kugawana hasara badala ya faida!

Kitakachotokea tusipoliweka hili sawa ni kuwa tutajikuta tumepelekana mahakamani tutakapogoma kugawana hasara wakati tulikubali kugawana faida! Mahakama itatafsiri kwa logic tu kuwa kama faida tunafaidi nusu kwa nusu maana yake ni kuwa na hasara tufaidi nusu kwa nusu! Hapo ndipo ile sh. bilioni 700 itakapotutokea puani maana hasara "itatengenezwa" kubwa kuliko hiyo!

Angalizo: Iwepo sentensi kabisa inayosema " tutagawana faida tu lakini hasara ni mzigo wa mwekezaji". Huo mtego tukiutegua mapema nina uhakika watakataa na majadiliano yataanza upya!

Barrick wakituona tunavyochekelea naamini wao wanacheka zaidi hadi mbavu zinawauma
 
Acha uzuzu, usalama wa taifa watakuwemo kwenye uhasibu mpaka board. Yaani kwa ufupi Mungu alishaamua kuikomboa Tz, ukimpinga Dkt Magufuli unampinga Mungu.
Hahaha...usalama wa taifa ... Yaani watanzania sijui huwa mnawaza nini....hivi usalama wa taifa wakiwepo ndio hatupigwi... Kwani miaka yote hiyo hatukuwa na usalama wa taifa??? Unadhani jpm atatawala milele??? Unajua atakayefata baada ya jpm atakuwa na sera gani....!!!?? Kwa akili zako unafikiri biashara ya uchimbaji na uuzwaji wa madini ni kama kuuza karanga...??
 
Sisi tumekubaliana kugawana faida nusu kwa nusu na si hasara, hiyo ni tafsiri yako.
Unajua maana ya profit??? Kwa taarifa yako kuna faida (-ve) ambayo baada ya kutoa production cost unapata....

Ngoja nikupe ka mfano kadogo pamoja na elimu yangu ya la nne B.
Unaponunua kitu mfano mayai kwa jumla ya sh. 1000. Akayachemsha na kuanza kuyazungusha mtaani na baadae ukauza na kupata 1800. Kwenye hiyo 1800 toa capital ambayo ni buku...itabaki 800 hiyo toa gharama zote ikiwa ni pamoja na chumvi..gharama za kupika na muda wako wa kuuza mtaani...kama hizo gharama zitazidi 800 lets say zikawa 1200 ndipo tutasema tumepata faida ya -400!! Sasa hiyo -400 kama ulikuwa mnashirikiana na mwenzako lazima mgawane ili kila mmoja achukue faida ya -200
 
Itakuja hoja kuwa Barrick haipati faida, kwa swala la msamaha wa kodi litajitokeza.....
 
Ficha upumbavu wako mkuu, tangu lini na wapi ukasikia hasara inakua offset na capital? Kama nyie ni sehemu ya uwekezaji lazima mtaumizwa tu na hasara (endapo itatokea) ingawa inakua na limitations (limited liability).

Mkuu ujinga ni mzigo sana na Magufuli ana kazi sana katika hili...

Nikuuilize swali moja kama wewe sio mjinga na mpumbavu utalijibu..

Hivi ukiwa na biashara yako umewekeza mtaji wa shilingi 100,000. Mwaka mzima umefanya biashara, mwisho wa mwaka ukaja piga hesabu ukakuta umepata faida ya shilingi 20,000 baada ya kuondoa matumizi yote. Ina maana utakuwa na 100,000 + 20,000 = 120,000 wakati wa kuanza mwaka mpya wa fedha. Hii 20,000 unaweza kuiondoa ukafanyia mambo yako mengine (dividend) au ukaiongezea kukuza mtaji (Capitalization of profit)

Chukulia kinyume chake. Ukiwa na biashara yako umewekeza mtaji wa shilingi 100,000. Mwaka mzima umefanya biashara, mwisho wa mwaka ukaja piga hesabu ukakuta umepata hasara ya shilingi 20,000 baada ya kuondoa matumizi yote. Ina maana utakuwa na 100,000 - 20,000 = 80,000 kwa maana ya kwamba umetumia kingi zaidi ya kile ulichozalisha na ziada ya matumizi yako imetokana na pesa ya mtaji. Wakati wa kuanza mwaka mpya wa fedha utakuwa na shilingi 80,000 ya mtaji kwa maana ya kwamba matumizi yako yamekuwa makubwa hadi umetumia pesa za mtaji.

Hivi huwa unaelewa nini unaposikia watu wakisema amekula mtaji, amefilisika!!!

Mkiitwa Vilaza mnakasirika pumbavuu kabisa.
 
bavicha hawana uelewa kuhusiana na lolote lakini wanajaza forum kwa mambo yasiyokua na maana kabisa
 
Back
Top Bottom