Si ATCL AU TGFA hizi zote ni hasara na janga kwa taifa

Lukumba

Member
May 24, 2023
35
91
Wakati Bungea la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania likipitisha makadirio ya Tshs Trilioni 3.5 za wizara ya Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ni vyema Prof.Mbarawa atambue kuwa aidha ATCL au TGFA hasara kwa taifa achague moja kusuka au kunyoa ili kupunguza au kuondoa hasara kwa taifa.

Kwa mfano mwaka 2019/2020 peke yake mkaguzi wa hesabu za serikali Tanzania (CAG) anasema shirika la ndege la Tanzania limepata hasara ya zaidi ya bilioni 60 kwa maana hiyo mpaka hivi sasa shirika la ndege la Tanzania bado linaendeshwa kwa hasara tena hasara kubwa ambayo haijawekwa wazi vya kutosheleza.

Kwa mwaka 2015/2016 shirika lilipata hasara ya bilioni 94.3, mwaka 2016/2017 shirika la ndege Tanzania lilipata hasara ya bilioni 109.3 na mwaka 2017/2018 shirika lilipata hasara ya zaidi ya bilioni 113.8.

Shirika la ndege la Kenya (Kenya Airways) lilitangaza hasara ya dola milioni 83 kwa mwaka 2020. Na kulingana na Mwenyekiti wa shirika hilo la ndege alieleza bayana ya kuwa hakuna ukuaji wa sekta hiyo kwa hivi sasa labda mpaka ifikapo mwaka 2024/2025.

Mfano Mashirika ya ndege ambayo pamoja na corona yameendelea kufanya vizuri kutokana na kujidhatiti kibiashara ni pamoja naShirika la Emirates ambalo pamoja na corona janga la corona kwa mwaka 2020 lilitengeneza faida ya dola milioni 456 ($ 456) . Shirika la ndege la Singapore Airlines likitengeneza faida ya 59.1 bilioni Singapore dola.

Serikali ni vyema ikafahamu kuwa ili kuweza kufanikiwa katika aina hii ya biashara lazima wakubali kujifunza zaidi kutoka kwenye mashirika yanayofanya vizuri kwenye uwanda huu ilikujipatia uzoefu na mbinu za namna za kuendesha mashirika haya kwa faida zaidi. Mfano wa mashirika hayo ni pamoja na Air Canada, Delta Airlines, American Airlines na Singapore Airlines.
Kwa mfano Shirika la ndege Etihad Airline likitengeneza faida ya dola bilioni 1.7 ($ 1.7) kwa kipindi cha mwaka 2020/2021 na kwa mwaka 2021/2022 likitengeneza faida ya dola Bilioni 2.0.

Vinginevyo mashirika haya yataendelea kuwa hasara na mzigo kwa Serikali na wananchi na hivyo kupelekea kurudi nyuma zaidi kimaendeleo kwani fedha nyingi badala ya kupelekwa kwenye maendeleo ya wananchi zitakuwa zikipelekwa kwenye kuokoa mashirika haya kutokana na hasara mashirika haya yanazozipata na kuleta.
 
Pesa na nguvu nyingi sana iliwekezwa kwenye mashirika Kama Emirates ndio maana leo yanafanya vizuri. Huduma zake kuanzia Economy mpaka first class na aina ya chakula na Entertainment zinazotolewa kule hauwezi compare na ATCL.

Infact carrier chache sana duniani Kama vile Qatar, Turkish n.k zinaweza kuwakaribia. Untill yafanyike mapinduzi ya kiuwekezaji kwa ATCL hasara zitaendelea kuwa kubwa.
 
Back
Top Bottom