Faida tutagawana nusu kwa nusu: Mtego ni kuwa hata hasara tutalazimika kugawana nusu kwa nusu!

Nani kasema faida tutagawana 50/50 ?
Magu kasema hivyo ila mzungu yule amesema wamekubaliana in future wataunda partnership ya 50/50
Hio maan yake ni hasara na faida na kuchangia mtaji...
 
hawajawah kupata hasara barrick sema faida ilikuwa inaliwa na wachach hqkuna aliyeweza kusema zaid ya kuwatetea lkn sasa kuanzia management tutakuwepo tutaona kila kitu nampongeza rais wetu jwa kweli hakuna mfano africa.

Mkuu haya mavitu kama hujui ni bora uwe msomaji tu, mwaka 2015 hawa jamaa walitangaza hasara ya US$ 197.1 Milion.....kwa MoU iliyofikiwa jana, GoT ingechagia kwenye hasara hiyo kwa 50%.
 
Siku faida ikiandikwa hivi $-600 Milion nazo tutagawana tu.
Kiufasaha zaidi kihasibu huwa inaandikwa hivi USD (600). Sitashangaa magamba yakachekelea yakiona hiyo figure kwenye mabano yakadhani ni "fungu" lao.
 
Mkuu haya mavitu kama hujui ni bora uwe msomaji tu, mwaka 2015 hawa jamaa walitangaza hasara ya US$ 197.1 Milion.....kwa MoU iliyofikiwa jana, GoT ingechagia kwenye hasara hiyo kwa 50%.
Duh! Naona dalili za kuingizwa mkenge wa kutisha.
 
Acha uzuzu, usalama wa taifa watakuwemo kwenye uhasibu mpaka board. Yaani kwa ufupi Mungu alishaamua kuikomboa Tz, ukimpinga Dkt Magufuli unampinga Mungu.
Usalama wa Taifa wapi?wale wanaotongoza mabinti kwa kutumia ID za TISS au wale waliojaribu kumuua LISU mchana kweupe wakamkosa au wale ambao walimtolea NAPE bastola mbele ya waandishi wa habari au unaongelea watu gani maana nyie vijana wa Lumumba mtakuwa mmebanwa na Haja ya mabadiliko
 
Angalizo: Iwepo sentensi kabisa inayosema " tutagawana faida tu lakini hasara ni mzigo wa mwekezaji". Huo mtego tukiutegua mapema nina uhakika watakataa na majadiliano yataanza upya!

Unajua hawa wajanja multi national companies wanapiga mahesabu na ku negotiate wakiwa na view ya mbali sana. Je hiyo migodi bado ina dhahabu kiasi gani? Je wanaweza kuuza shares zao bado na hata kubadili kampuni? Je uendeshaji utakuwa monitored na managed vzr ili wasihujumu migodi au uzalishaji? Nk nk
 
mzungu mjanja sana, naomba kuuliza ni mgodi gani ambao bado unachmbwa dhahabu hapa tanzania na barick? pili zile trilioni 300 kama sikosei ndio hatupati tena? tutamiliki 50% of shares je shughuri za uendeshaji tutashirikishwa au kazi yetu itakua kupewa tu financial statements zinazoonyesha tumepata hasara?
Umeambiwa hadi kwenye bodi watakuwepo wabongo na watalaam wengi wakibongo kwahiyo kila kinachoendelea kutokea day 1 tutajua.
 
Kiufasaha zaidi kihasibu huwa inaandikwa hivi USD (600). Sitashangaa magamba yakachekelea yakiona hiyo figure kwenye mabano yakadhani ni "fungu" lao.
Asante mkuu, leo nimenyaka maandishi ya kiuhasibu. Siku nikiona USD (600) najua jiti hilo.
 
Nianze kwa kutoa pongezi ya dhati maana kulipwa asilimia 0.156 ya tulichokuwa tunadai si haba! Lakini LA maana zaidi ni yale maboresho mbele ya safari!

Lakini kuna mtego mbaya kwenye haya makubaliano! Sijui kama hilo limewekwa sawa. Unaposema mtagawana faida nusu kwa nusu maana yake ni kuwa hata hasara mtagawana nusu kwa nusu! Vinginevyo iwekwe wazi kuwa faida tutagawana sawa ila hasara itabebwa na mwekezaji, kitu ambacho mwekezaji si rahisi kukikubali maana hakiendani na logic!

Ikumbukwe kuwa wameahidi kugawana faida ambayo mpaka sasa kwa mujibu wa CAG hawajawahi kuipata ndio maana hawajawahi kulipa kodi itokanayo na faida! Ila miaka yote "vitabu" vyao huonyesha wamepata "hasara" kubwa tu! Kwa hiyo kama haya makubaliano yakawa "back-dated" tangu walipoanza kuchimba dhahabu, hakuna hata senti moja ya faida ambayo tutagawana, ila kuna mamilioni ya dola ya hasara ya kugawana pia!

Labda waanze kuzalisha faida kuanzia Leo, vinginevyo tutegemee kugawana hasara badala ya faida!

Kitakachotokea tusipoliweka hili sawa ni kuwa tutajikuta tumepelekana mahakamani tutakapogoma kugawana hasara wakati tulikubali kugawana faida! Mahakama itatafsiri kwa logic tu kuwa kama faida tunafaidi nusu kwa nusu maana yake ni kuwa na hasara tufaidi nusu kwa nusu! Hapo ndipo ile sh. bilioni 700 itakapotutokea puani maana hasara "itatengenezwa" kubwa kuliko hiyo!

Angalizo: Iwepo sentensi kabisa inayosema " tutagawana faida tu lakini hasara ni mzigo wa mwekezaji". Huo mtego tukiutegua mapema nina uhakika watakataa na majadiliano yataanza upya!

Sisi ni shareholder by 16% na hiyo ndiyo itakuwa hasara yetu just in case!
Lakini mimi naweza kukuhakikishia kuwa hicho kitu hakipo kwa sababu wataalamu wanasema kuwa mpaka muda huu ni 10% tu ya resources zetu kwenye madini imeshachimbwa, na inasemekana kuwa kwa upande wa gemstones, hata pale chini kwenye majengo yaliyopo Mwadui, chini yake ni mali tupu, wanaita nadnani Kimberlite kwa jina la kitaalamu, na imetandaa kwenda mbali. Kwa ufupi tu ni kwamba madini tulionayo Tanzania ukiamua uyachimbe yote, huwezi kuyamaliza isipokuwa inabidi ukubali kuwa nyumba na mashamba yasiwepo, labda uwepo utaalamu wa kuhamia baharini tukajenge huko halafu nchi kavu tuache kwa ajili ya uchimbaji tu, upo hapo? Waone wataalamu wa madini watakupa LIVE!
 
Acha uzuzu, usalama wa taifa watakuwemo kwenye uhasibu mpaka board. Yaani kwa ufupi Mungu alishaamua kuikomboa Tz, ukimpinga Dkt Magufuli unampinga Mungu.
Wakati tunaibiwa miaka 19 mfululuzo taifa halikuwa na usalama wake? Kwa nini mnapenda kutoa majibu mepesi kwa hoja nzito?
 
Acha uzuzu, usalama wa taifa watakuwemo kwenye uhasibu mpaka board. Yaani kwa ufupi Mungu alishaamua kuikomboa Tz, ukimpinga Dkt Magufuli unampinga Mungu.
Sema mungu na sio Mungu. Acha kumshirikisha Mungu na hii serikali ambayo inapata madaraka kupitia ushirikina, kisha sehemu kama hizi ndo Mungu aingilie kati.

Mungu hachangamani na uovu, hakuna mapatano ya giza na nuru.
 
kumbe hii mambo bado mbichi, tusianze kusherekea wakati bado tupo gizani , tumetanguliza strust kwa each side na trasparence pia ila hawa jamaa hawajawahi kuwa na urafiki na mtu. What their after ni max profit , Tusiwaamini sana, kama ni kweli tunacho gawana ni faida na ambayo hawajawahi ipita , hili jambo waliweke sawa nikibidi lijadaliwe bungeni .. Tusije badaye tuka anza rushiana lawama.
Siku hizi haturushiani lawama, ni mwendo wa lisasi tu Mkuu
 
Ulitegemea upewe faida ipi ktk hasara.

Jua maana ya win win situation. Lazima wote m feel. Kama kuna faida mna enjoy wote vivo ivo ktk hasara mnasilizia wote.
 
Back
Top Bottom