Fahamu upande wa pili wa Dangote

Fahamu upande wa pili wa Dangote

Daah! sisi tunajua nchi yetu ina itikadi za kisekula kumbe kuna serikari kama serikari ya awamu ya nne iliwapeleka watu kuhiji Mecca, kama hili swala ni kweli basi naanza kupata wasiwasi na uliokuwa uongozi wa awamu ya nne.



Mnaona sasa kumbe walitanguliza imani kipindi muwekezaji anakuja ndiomana leo anavyopata misukosuko wanaleta mambo ya imani tena kwa kusema kuwa anahujumiwa kisa yeye ni Muislamu.
Hii kesi ni sawa na ile ya mababu zetu kupewa gololi na mzungu na wao kuchukuwa almasi na dhahabu . ...EHH RHABUKA NAKUOMBA USIKIE KILIO CHETU.....
 
Enough is enough . .jamani dah!
 
Kuna utafiti nafanya kuhusu dangote....!! Kuna vitu vimeniuma sana..ntaandika thread kuhusu dangote
 
Haya ngoja tupate uhakika kumhusu huyu investor toka Nigeria dunia kijiji tuone yaliyojificha
 
False flag
Katumwa huyuu jamaaa tena hafai muongo sana, dangote ana utapeli gani Wakati kila kitu kiko clearly wewe vp lakin?
 
Hahaha naona umeamua kutafuta kiki kwa kupitia aliko dangote
Umelopoka mengi mno ila je unajua gharama ya kwenda kuhiji kwa mtu mmoja?

Jitahidi kupunguza kujipendekeza ukapitiliza yaka kukuta ya wateuliwa.
 
issue cement ipo very complicated kwasababu bei ya cement inapangwa juu ya meza badala kuwa determined na supply and demand...tulitapeliwa kiwanda cha twiga hapa kilikuwa kinapata profit more than 100% na kuajiri watanzania zaidi ya 4000 msuya na genge lake la wizi wakikomalia mpaka wakakibinafsisha bila sababu za msingi waliopinga kisiuzwe wakina nicas mahinda wakapelekwa kaburini kwa nguvu... kiukweli cement hapa Tanzania haipaswi kuuzwa zaidi ya 5000/= kwa mfuko coz kila kitu kinapatikana hapa hapa Tanzania but ujanjaunja wa viwanda vya cement wanauza bei ya ajabu kabisaa...I don't care about dangote ila kama ametuahidi atatuzia cement bei ya chini tumpe nafasi coz tunaumia ni sisi wananchi wa kawaida si wanasiasa.
 
Jamani mikataba si ipo tena kwa mujibu wa sheria za kazi na uhamiaji. Mwenye kopi ya huo mkataba atupie hapa tuudadavue. Usije kuta mkataba ulikuwa na provisions ambazo leo zinafanya Dangote aonekane tapeli. Ila bandiko hili kinaonekana lina kaukweli. Hata hivyo ili kuwa balanced kamkataba katupiwe hapo au wanaojua watuambie kama Dangote amekiuka vipengele fulani vya mkataba ili kustahili madongo yote haya!
 
Walioingia naye mikataba ni ccm ....

Wanaovunja mkataba ni Ccm.....

Waliompokea ni Ccm......

Wanaotaka aondoke ni Ccm.....

Tafakari chukua hatua.........
Huyoo chizi alioandika huu ujinga,akatafute kick nyengine ila sio hii duuuu nafasi huyuu,dangote kaweka almost 1 billion $ ktk ya poli pale alafu anadiliki kumuita ati tapeli [emoji40] [emoji40] [emoji40]
 
Haahaah tunasema mazungumzo baaada ya HABARI. Mbona mwanzo hukusema.
 
Dangote labda abadilike ndio tutaweza kufaidi uwepo wake hapa Tanzania, ila kwa jinsi alivyo na ninavyomfahamu..kwa sasa kuondoka kwake ni nafuu kwa Watanzania na Taifa.

Yule bwana hawezi kufanya biashara bila utapeli hata mfanyakazi wake wa chini kabisa anajua. Jamaa anaingia mahali kwa lugha tamu sana na ahadi kibao, lakini si mtu yule.

Wapo wanaosema kuhusu ajira za watanzania walioko pale, ni hivi wafanyakazi wataalamu walioko pale ni wale waliokuwa kwenye viwanda vingine vya cement vilivyokuwa vinawalipa vizuri ila baada ya kusikia tishio la ujio wa likiwanda kubwa ambalo lingepewa gas, exemption ya kodi n.k likapunguza bei ya cement viwanda hivyo vingekufa kwa kushindwa kujiendesha,

Hatua mojawapo zilizochukuliwa na viwanda bora kama vile Twiga na vingine ni kupunguza wafanyakazi kwa kiasi kikubwa ambao wengi walienda Dangote kulipwa ujira mdogo sana maana yeye Dangote anatumia management ya Wahindi.

Kule Nigeria alianza biashara zake kwa style ya kuwahonga viongozi wakuu na wakampa excemption ya kodi, matumizi ya barabara hovyo na vitu vingine akashusha bei ya Cement, viwanda vingine vikafa akabaki yeye mwenyewe akishikilia kama 90% ya soko la cement na Lafarge kama chini ya 10% vingine vilikufa baada ya kuhakikisha kwamba ameviua akapandisha bei ikarudi kama zamani.

Hivyo ndivyo alitaka kufanya Tanzania, JK alimpa maeneo makubwa sana, mpaka na eneo la kujenga bandari yake binafsi, jambo ambalo kwa maoni yangu naona ilikuwa hatari hata kwa usalama wa nchi.

Eneo lililojengwa kiwanda na mining lilikuwa la vijiji vitano, ni eneo kubwa ambalo lilikuwa mali ya wananchi, Dangote kwa kushirikiana na viongozi wa serikali ya awamu ya nne waliwatapeli wale wazee kwa kuwapa vitu vidogo vidogo na ziara ya kwenda kuhiji kwa wazee wachache pamoja na laki tano tano na ahadi kibao wakabariki kuiacha ile ardhi na wale wazee wakatumika kuwashawishi wengine wakaingia kingi.

Mara kadhaa nilikuwa nikiwaona hawa wazee wanaojiita wenyeviti wa vijiji vile wakiambaa ambaa pale nje ya kiwanda cha Dangote wakitapeli watu kwa ahadi ya kuwaunganishia vibarua kiwandani wakati hata wao hawana ruhusa ya kuingia ndani ya kiwanda, wazee wamepigika wanajuta tu kimoyo moyo.

Niliwahi kujaribu kuongea na mmoja wao ambaye alikuwa mwenyekiti wa wenyeviti wakati huo nikiwa kiongozi wa chama cha wafanyakazi hapo Kiwandani, nilipomuuliza sababu ya wao wazee kugawa ardhi bure kwa Dangote aliniambia kwamba wao waliamini Dangote si mfanyabiashara ni Alhaji kwa hiyo walitoa ardhi kwa Alhaji ili ajenge kiwanda kiwasaidie watu..

Nilishangaa sana, lakini kilichonifurahisha ni kwamba wanajuta maana zaidi ya laki tano na ziara ya Mecca hawajafaidika tena kwa namna walivyotarajia.
Mtindo wa ufanyaji kazi wa Dangote ni wa kitapeli tapeli tu, anatapeliwa kuanzia mfanyakazi wake wa chini mpaka Rais na mawaziri wakiingia kingi wanatapeliwa.

Kule Nigeria, ana kiwanda kikubwa Four kiln lines kwenye state ya Obajana na kingine Ibese, wafanyakazi zaidi ya 60% ni wahindi, wanaishi vizuri kila kitu wanachotumia ni tofauti na weusi, magari, nyumba za kuishi n.k ni tofauti kabisa.

Wahindi wanaletwa wakiwa hawajui kitu kabisa wanafundishwa na weusi (wanigeria) halafu wakishajua wanawasimamia weusi, wanawanyanyasa sana waafrika, pale ndipo nilipojua kwamba Tanzania ni nchi nzuri sana na siku zote nawambia ukitaka kujua uzuri wa nchi yetu Tanzania nenda Nigeria. Hususanu kufanye kazi kwa Dangote.

Wakati Dangote anafungua kiwanda Tanzania, alikuwa anaahidi kuajiri watanzania lakini ukweli ni kwamba alikuwa ameandaa makontena ya wahindi kuja Tanzania kama ilivyo Nigeria, thanks to God Magufuli akaingia Madarakani.

Wale wahindi wachache waliokuwepo walichukia sana wakaanza hata kukuza mambo au kutunga uongo wakiilaumu Serikali ati kwa kuweka vikwazo vingi, wakati mwingine wanamdanganya Dangote kuhusu Serikali yetu na Watanzania ili wao wapate faida. Ninao ushahidi wa mambo baadhi ambayo kwa makusudi kabisa management ya kihindi ilikuwa ikimdanganya Dangote kwa faida yao.

Mojawapo ilikuwa ni ubora wa makaa ya Mawe ya Tanzania, tulikuwa na vijana wetu maabara pale, hata mimi niliposikia kwamba makaa yetu ya mawe yana quality ya chini niliumia sana niliwauliza wahandisi wetu waliokuwa maabara wakasema ni uongo.

Hiyo ilikuwa mbinu ya wahindi kufanya biashara na makampuni ya South Afrika kwa faida yao huku wakichafua bidhaa zetu.

Lingekuwa jambo la ajabu sana kama serikali ingekubali uhuni huo, nawapongeza sana Mawaziri hawa wa awamu ya tano kwa kutumia elimu yao vizuri kuchunguza hilo kwa sababu hata enzi zile tulikuwa tuwaeleza serikali kila tunapopata nafasi lakini enzi ya awamu ya nne ilikuwa enzi ya aina yake. tulionekana wapuuzi au maskini wanoko.

Watanzania tunapopinga au kutetea ni vema tukatafuta ukweli kwanza, Dangote industries ukiisikia kwenye vyombo vya habari utaona ni mkombozi kwa watanzania, lakini kwa namna ilivyo na inavyotaka ifanyiwe ni hatari sana kwa taifa.

Tumshukuru sana Rais na serikali kwa msimamo wake. Dangote hana tofauti na akina Carl peters wa zamani labda abadilike.........

Itaendelea wiki ijayo
Kama kweli ni mtu hatari sana
 
Kuja kwa viwanda vya wageni Tanzania ni neema pia kwa bidhaa za ndani na ajira kwa ujumla, nitashangaa sana kama dangote ataajiri zaidi ya watu 50 wahindi akaacha watanzania na serikali ipo, pia nitashangaa sana kama baadhi ya materials kama makaa ya mawe nayo yaagizwe kutoka nje ya nchi nawakati yanapatikana Tz, kuhusu gesi anunue sio kwa kupewa bure, maana in returns sisi tutanunua bidhaa zake iweje tumbembeleze wakati huo kiwanda kimeshajengwa nchini? hataki basi afunge, mfanyabiashara yeyote anae fanya kazi kwa karibu na wahindi unatakiwa kumuangalia very close,maana wahindi ni corrupted people in the world, hivyo dangote pia lazima tukae nae chonjo tukizubaa atashangaza.
 
kuna mtu namfahamu alifanya interview nafasi nahiifadhi alishundanishwa na mtu toka south Afrika na akashinda ila lilipokuja swala la malipo yakawa chini nafikiri ilikuwa njama wamlete mtu toka south afrika.Huu mtindo wa kuanzisha viwanda na kuuza bidhaa kwa bei ya chini upo sana kwani baada ya muda viwanda vingine vinakufa baadae anapobaki mmoja anapandisha bei na hakuna wa kumpinga.Kwanini vivutio apewe dangote peke yake wakati tuna vingi vya cement kwanini awe yeye peke yake.Kuna wafanyakazi wengi wa nje waliondolewa na serikali ya awamu hii baada ya kubainika hawana vibali.Wakati tunahitaji wawekezaji ni vema wawekezaji waheshimu sheria za nchi na pia wasiwekeze kwa watu binafsi kama viongozi wanaokuwa madarakani muda huo
 
Tatizo watanzania tumezoea na tunataka mzungu aje mikono mitupu,tumpe ardhi aende bank akope,atunyonye kisha asepe zake ndiyo tutamuita muwekezaji.Kumbuka Dngote ana surplus ya pesa na viwanda nchi mbali mbali afrika hivyo hana hasara kama udhaniavyo.Wewe ndiye utapata hasara Kwa kuuziwa cement sh 15000
Mondoros
 
Back
Top Bottom