Fahamu undani wa mnyama simba

Fahamu undani wa mnyama simba

Simba jike aliyekomaa kuzaa anaishi katika familia yao kumbuka madume yanakuja nakuondoka ila majike daima wanabaki na koo yao daima wao wanaishi kama mabibi.mama.shangazi.mabinamu katika kaya yao pia kukumbusha tena ikitokea mwezao mmoja anakaribia kufa wanajua kuwa mwezao haponi na wale Wa umri wake wanamsindikiza safari yake ya mwisho na wanamuacha wanaondoka zao

Ahsante Mkuu (noted with concern).
 
Kingine ni kwamba simba hua hapendi dharau za kuchekewa chekewa kutaniwa

anakula kilo 15 baada ya hapo anapumzika kuwinda lakini hii haimaanishi kwamba nyumbu wanaweza kupita mbele yake akawaacha.
Sijapendezwa na kitendo chao cha kula kilo 15 tu na kushiba wakati wanaangusha mnyama wenye kilo 200 hadi 300 kwa mfano wale nyumbu au mbogo. Ni waharibifu tu hao.
 
Je wajua ni kwanini simba jike anajitenga pale anapokaribia kuzaa na kwenda mafichoni kipindi cha miezi mitatu na anaporudi lazima awatambulishe watoto kwa mzee Wa familia na kinakuwa kipindi kigumu kwa familia zima kwani mzee akiwakataa watoto anawauwa.sababu kubwa ni hii.na ndio msingi mkubwa sana wasimba jike kwenda mafichoni.simba jike anakuwa na chuchu za matiti nne tuu.sasa kama unakumbuka simba wananyonyesha watoto Wa simba yoyote jike Wa ile familia yao sasa kama akijifungulia pale kwenye familia basi watoto wake watakufa kwa njaa maana hawana uwezo mkubwa wakunyonya maziwa ya mama yao kwakuwa wale wengine wameshakuwa wakubwa kuliko wao na watanyonya wakubwa tuu.hapo mama analazimika kuondoka tuu ilikulinda afya za watoto wake.sababu ndogo ndogo ni kwa kuogopa wasiumie kwenye familia.magonjwa ya milipuko.
 
Hawa simba dume ,vijana baada ya kufikisha miaka miwili wanatimuliwa kwenye familia zao ,swali je hakuna uwezekano baadae wakakutana na mama na dada zake ? Au anawajua dada na mama zake hivyo hatoweza kuwaingilia kimwili ?
 
Awa wote ni jamii yapaka na wanatofautiana kwa mazingira yao
Tiger ndio paka wakubwa kuliko wote asa Wa siberian Tiger.wao wanamadoa makubwa makubwa sana kuliko Wa chui na cheeter.ndio wananguvu kubwa za mwili mzima kuliko paka wote.pia anauwezo mkubwa sana wakuogelea tofauti na paka wengine angalau jaguar nae anauwezo sio mkubwa kama Wa Tiger wakuogelea.Tiger wanawinda kwa ambush kali sana kama radi linavyopiga wanalingana na chui katika uindaji Wa ambush.Tiger ni mnyama anayeishi pekee kama chui juguar puma

Chui.aina yapaka yeye anamadoa doa madogo kama yacheeter ila wanatofautiana na cheeter kwa kuwa chui sio mrefu na mwembamba kama Cheeter na hiyo ndio tofauti yao kubwa sana.piachui anaishi mwenye ila kama anamtoto atamlea Bila ya baba tofauti na simba wao wanalea watoto wao kwa ukoo.chui ndio mnyama anayewinda kwa utulivu mkubwa kuliko wote mfano anaweza akawa anawinda mahali simba walipolala na akafanikiwa windo lake Bila ya kelele yoyote na simba wakajajua kama chui amaefanya yake baadaya ya windo kupandishwa juu ya mti na ile harufu ya damu ndio uwafanya simba kujua.chui ndio mnyama paka mwenye kubwa sana nguvu za miguu ya mbele kuliko wote kwani anauwezo wakupandisha Mara mbili juu ya mti uzito Wa windo lake.pia chui uwinda kama solo hunter kama tiger puma
Cheeter naongezea nilishamgusia juu.ndio paka mwenye speed kuliko paka wote na wanyama wote Wa nchi kavu cheteer ndie paka dhaifu kuliko wote.anapokuwa anakimbiza windo lake analikimbiza kwa muda maalumu kwani asipofanya hivyo anapata madhara yafuatayo 1.moyo kupasuka.2.calories zake kila anapofanya windo na kulikosa windo zinapongua sasa akizimaliza ndio mwisho Wa maisha yake.cheeter ndie mnyama ambaye anapofanikiwa kulipata windo anakula haraka ndani ya dakika 20 ili anapovamiwa na fisi.simba awe amekula angalau kumbuka fisi mmoja anauwezo mkubwa wakpambana na kumfukuza cheeter au chui kwenye mawindo yao.

Juguar ni chui Mweusi Wa amerika ya kusini sifa zake kama za chui wakawaida sema yeye anauwezo wakuogelea.

Puma ni simba Wa amerika ya kusini anayepatikana katika milima ya Andes sifa zake tofauti na simba Wa Afrika kwani ni solo hunter yeye.pia mdogo kiumbo kwa kuwa anapatikana kwenye baridi na anakaa milimani tuu.pia kuonekana kwake ni nadra sana sana inaweza kukuchukua muda mrefu kumuona na ndio maana wataalamu wanategesha kamare tuuu ili kujua kama yupo.
Mkuu nakushukuru sana kwa masomo yako murua. Ubarikiwe sana. Huwa napenda kuangalia video za wanyama na nilishangazwa na kitendo cha simba kuwa dhaifu kwa chatu tofauti na chui ambao wana uwezo wa kuua chatu. Unaweza kunifafanulia kidogo kuhusu hilo suala?
 
Je wajua ni kwanini simba jike anajitenga pale anapokaribia kuzaa na kwenda mafichoni kipindi cha miezi mitatu na anaporudi lazima awatambulishe watoto kwa mzee Wa familia na kinakuwa kipindi kigumu kwa familia zima kwani mzee akiwakataa watoto anawauwa.sababu kubwa ni hii.na ndio msingi mkubwa sana wasimba jike kwenda mafichoni.simba jike anakuwa na chuchu za matiti nne tuu.sasa kama unakumbuka simba wananyonyesha watoto Wa simba yoyote jike Wa ile familia yao sasa kama akijifungulia pale kwenye familia basi watoto wake watakufa kwa njaa maana hawana uwezo mkubwa wakunyonya maziwa ya mama yao kwakuwa wale wengine wameshakuwa wakubwa kuliko wao na watanyonya wakubwa tuu.hapo mama analazimika kuondoka tuu ilikulinda afya za watoto wake.sababu ndogo ndogo ni kwa kuogopa wasiumie kwenye familia.magonjwa ya milipuko.
Duuuh! Naona simba wana akili sana kuzidi wanyama wote isipokuwa binadamu
 
Sijapendezwa na kitendo chao cha kula kilo 15 tu na kushiba wakati wanaangusha mnyama wenye kilo 200 hadi 300 kwa mfano wale nyumbu au mbogo. Ni waharibifu tu hao.
Aahh.. Mkuu piga mahesabh vzur, simba hali mmoja, wanakuwa kadhaa hapo kila mmoja na kilo 15 zake tumboni.. Hizo kilo 200za myumbu bado hujatoa mifupa, kichwa, utumbo n.k.. Kwa hyo kuangusha hao wanyama ni sawa tu
 
Je wajua kuwa simba dume mmoja akiwa anavamia na wenzake madume mfano matatu kabla ya kukutana nakupigana wanapeana vitisho vya mngurumo na endapo yule mmoja anayevamia akatoa mkali zaidi ya wale wanaokuja watatu wale watatu wanaghairi kuja wanajua mwezao ni mkali na ananguvu kubwa kuliko wao.pia simba dume anapovamia na wenzake na mfano wawili na kuendelea simba jike wale Wa yule anayevamia wanaweza kuamua kumsaidia dume au kutomsaidia.kwanini wanamsaidia kupigana.kama kuna watoto wadogo ambao wameshakua na wanajua akishindwa dume basi watoto wao watauliwa pia wanamsaidia kama yule dume ameishi kwa upendo mkubwa na wale wanaweke na kwanini simba majike yanpoamua kutomsaidia mwanaume pindi wanapovamia kwasababu dume limezeeka kwao kuna kuwa hakuna ulinzi wakuaminika kwa ajili ya watoto wao na mji wao pia simba jike wanapenda kupandwa na simba mwenye uwezo bora na nguvu ili kutoa watoto bora.pia je mnajua kuwa kila simba wanakaya zao ambazo daima zinatengenishwa na kwa kuweka alama ya mikojo ya simba dume ambao ndio walinzi wakuu wafamilia.je wajua kuwa ikitokea kwa simba majike yakavuka mpaka Wa kwenda kuwinda na watoto zao na wakakumbana na masimba jike wakaya nyingine ambao ndio eneo lao wale waliovamia atakama wako wengi wanakimbiasana na ikitokea walikwenda na watoto wao wanawaacha nyuma na wale waliowafumania kama wale watoto wakiwa wadogo sana hawahui na watawaacha mpaka mama yao atakapowaita kwa mlio maalumu.

AISEEE mnajuaje na hali hamjui lugha yao
 
Awa wote ni jamii yapaka na wanatofautiana kwa mazingira yao
Tiger ndio paka wakubwa kuliko wote asa Wa siberian Tiger.wao wanamadoa makubwa makubwa sana kuliko Wa chui na cheeter.ndio wananguvu kubwa za mwili mzima kuliko paka wote.pia anauwezo mkubwa sana wakuogelea tofauti na paka wengine angalau jaguar nae anauwezo sio mkubwa kama Wa Tiger wakuogelea.Tiger wanawinda kwa ambush kali sana kama radi linavyopiga wanalingana na chui katika uindaji Wa ambush.Tiger ni mnyama anayeishi pekee kama chui juguar puma

Chui.aina yapaka yeye anamadoa doa madogo kama yacheeter ila wanatofautiana na cheeter kwa kuwa chui sio mrefu na mwembamba kama Cheeter na hiyo ndio tofauti yao kubwa sana.piachui anaishi mwenye ila kama anamtoto atamlea Bila ya baba tofauti na simba wao wanalea watoto wao kwa ukoo.chui ndio mnyama anayewinda kwa utulivu mkubwa kuliko wote mfano anaweza akawa anawinda mahali simba walipolala na akafanikiwa windo lake Bila ya kelele yoyote na simba wakajajua kama chui amaefanya yake baadaya ya windo kupandishwa juu ya mti na ile harufu ya damu ndio uwafanya simba kujua.chui ndio mnyama paka mwenye kubwa sana nguvu za miguu ya mbele kuliko wote kwani anauwezo wakupandisha Mara mbili juu ya mti uzito Wa windo lake.pia chui uwinda kama solo hunter kama tiger puma
Cheeter naongezea nilishamgusia juu.ndio paka mwenye speed kuliko paka wote na wanyama wote Wa nchi kavu cheteer ndie paka dhaifu kuliko wote.anapokuwa anakimbiza windo lake analikimbiza kwa muda maalumu kwani asipofanya hivyo anapata madhara yafuatayo 1.moyo kupasuka.2.calories zake kila anapofanya windo na kulikosa windo zinapongua sasa akizimaliza ndio mwisho Wa maisha yake.cheeter ndie mnyama ambaye anapofanikiwa kulipata windo anakula haraka ndani ya dakika 20 ili anapovamiwa na fisi.simba awe amekula angalau kumbuka fisi mmoja anauwezo mkubwa wakpambana na kumfukuza cheeter au chui kwenye mawindo yao.

Juguar ni chui Mweusi Wa amerika ya kusini sifa zake kama za chui wakawaida sema yeye anauwezo wakuogelea.

Puma ni simba Wa amerika ya kusini anayepatikana katika milima ya Andes sifa zake tofauti na simba Wa Afrika kwani ni solo hunter yeye.pia mdogo kiumbo kwa kuwa anapatikana kwenye baridi na anakaa milimani tuu.pia kuonekana kwake ni nadra sana sana inaweza kukuchukua muda mrefu kumuona na ndio maana wataalamu wanategesha kamare tuuu ili kujua kama yupo.

INTERESTING.....
 
GJY6QL3NGwd4KSZ23Hu-ofox_UQj0UkGiONUj2nWsvmvB-nKHo9a6I_tazn0_X5UhA=h900

Simba kwa kiingereza anafahamika kama lion na jina lake la kisayansi (scientific name) anafahamika kama panthera leo na koo(Genus) yake ni panthera, hii koo panthera inajumuisha na wanyama wengine ikiwemo tiger wa bara la asia, chui, American jaguar, na mnyama anaefahamika kama puma au mountain lion.

Simba yupo kwenye order ya wanyama walaji wa nyama almaarufu carnivore na familly yake inaitwa felidae, hii familly ya felidae inajumuisha paka wote wanaopatikana duniani ikiwemo wanaofugwa manyumbani, paka pori, simba, chui, tiger, jaguar na wengineo jamii ya paka ikiwemo cheetah(Duma).

Simba ndiye paka mkubwa Africa na anashika namba mbili duniani baada ya tiger ambaye anapatikana barani Asia pekee dunia nzima na simba pekee ambaye huishi katika makundi miongoni mwa wanyama jamii ya paka na kundi lao linaitwa(pride) pia simba ni wanyama wanaopendelea kuishi maeneo wazi yenye nyasi(Open area) kama ngorongoro crater na Serengeti national park.

Simba pia anafikia hadi uzito wa kg 220-250 kwa dume na upande wa jike ni kg 100-120 na katika familia ya simba ni majikee pekee wanaofanya shughuli ya uwindaji (hunting ) na madume wao hubaki na watoto na majike wakishaua mnyama simba dume ndo huanza kula kisha watoto na baadaye jike ilihali wao ndo wawindaji.

Pia simba ndo wanyama wanaoongoza kwenda fungate (Honeymoon ) na huenda kwa takribani wiki mbili, iko hv kwa kuwa hawa wanaishi katika makundi dume na majike ikitokea katika ile familia kama kuna jike ambaye yuko heat hua anamchukua dume wanaenda mbali kidogo na ile familia kwa ajili ya kufanya mating kwa huo muda wa wiki mbili na kabla ya kwenda fungate kwa kawaida yule jike anayehitaji kwenda fungate na dume huwa anamuwindia dume chakula kizuri chenye mafuta ambacho kitamshibisha yule dume na wakiwa fungate huwa hawali kitu chochote wanakunywa maji tu kwa huo mda wa wiki mbili na huwa wanajamiana kila baada ya dakika saba (sasa ebu fikiria siku ina dakika saba ngapi na kwa huo mda wa wiki mbili dume atampanda jike mara ngapi).

Simba pia hupendelea kuwinda wanyama kama mbogo, pundamlia, nyumbu na baadhi ya swala na kwa kawaida simba dume ana uwezo wa kula hadi Kilo 15 za nyama na akishakula hizo kilo 15 huwa anauwezo wa kukaa siku tatu mpaka wiki moja bila kula halafu ndo anakuja kuwinda tena.

Katika kuwinda kwao wanatumia staili kuu tatu ya kwanza ni sporting ( wanaangalia mnyama wa kumuwinda), ya pili ni stalking ( wananyemelea ) na ya mwisho ni ambush ( kuvamia) na wakishakamata mnyama huwa wanakimbilia kuuma shingoni ili kumbana pumzi(suffocate) na sio kunyonya damu kama wengi wanavyodhani na kwa kawaida simba jike hubeba ukauzito kwa mda wa miezi 3 na anazaa kuanzia watoto 2-4.

Sasa unaweza ukajiuliza kama jike la simba hubeba ujauzito kwa huo mda na kujifungua watoto wengi mbona simba ni wachache? Iko hv hawa wanaishi kwenye makundi dume akimiliki majike wake na huwa hawa madume wenye familia wanachallengiwa na madume ambao hawana familly kwa ajili ya kimiliki zile familly na ikumbukwe sio madume wote wa simba wanamiliki familia sasa ikitokea kwa bahati mbaya huyu simba mwenye family akapigwa na dume mwenzake ambaye hana family huyu dume ambaye hana family atachukua ile family ya yule dume aliyempiga na kuitawala yeye na kwenye ile family akikuta kuna watoto wa yule dume aliyempiga atakachofanya huyu dume atawaua wale watoto wote kwa sababu hawezilea damu isiyoyake na anafanya vile ili jike mwenye wale watoto apatwe na uchungu aingie kwenye heat ili ambebeshe mimba yake na kama kwenye ile familia kuna jike mwenye ujauzito atakachofanya huyu dume atamchukua yule jike atamtoa nje ya family na ataforce kumpanda hadi ile mimba itoke then anampachika mimba yake.

Vile vile hawa simba dunia nzima wanapatikana Africa na Asia na katika bara la asia wanapatikana pale india pekee katika msitu unaoitwa geyforest. Vilevile hawa simba ndo wanyama wanaoongoza kulala kwa siku hulala masaa 16 na kufanya kazi masaa 8 na kawaida wanawinda usiku na wakati mwingine mchana pale hali inaporuhusu na hawa ni wachangamfu mchana na usiku (diurnal and nocturnal ) yaani wao huona usiku na mchana. Huyo ndo bwana simba (king of jungle ) kama wengi wanavyopenda kumwita.
Mkuu,
Asante kwa kjishughulisha kutupa elimu hii nzuri ingawaje kuna wapuuzi wanashindwa kuona uthamani wa kupoteza muda wako wa kuweza kutoa elimu kama hii ambayo watu husota nayo pale mweka. Wanaleta topic za ujinga!
Nauliza kwa nini simba has a akifugwa kwenye game Sanctuary hazai?
 
Back
Top Bottom