Fahamu undani wa mnyama simba

Ni kweli mkuu na ikitokea kwa bahati mbaya akaua mtu huyo lazima auwawe kwa sababu wanasema nyama ya binadamu inakuwa na chumvichumvi na ni tamu kwa hiyo simba akionja nyama ya binadamu atasahau nyama pori na ataanza kuwinda binadamu ndo maana huwa anauwawa
hapo sasa nimeamini unatambua ulicho kiandika baada ya kumjibu huyu mtu.hakika uko vzr.
juu ya elimu yako.hongera sana.
 
Ni kweli mkuu hawa white lion wana undugu na hawa simba wa kawaida isipokuwa wao wanakuwa weupe kutokana na huzaliwa na gene nyingi sinazosababisha albinism na hawa white lion hawana uwezo wa kuishi porini kama hawa simba wa kawaida wao huhifadhiwa kwenye vigala vya kuhifadhia wanyama pori (zoo ) na hasa hasa wanapatikana kwenye zoo katika nchi za Africa kusini, Austria na nchini Serbia kwa hiyo ukibahatika kutembelea moja kati ya hizi nchi hao White lion utawaona. Picha ninazo ila bado sijafahamu namna ya kuziweka kwenye sehemu comment
Hata hivo uzi uliotuletea ni mzuri sana wacha tukusaidie.
White-Lion-Full-Hd-Wallpaper-680x425.jpg
 
144a5ba57b5c133cuc3f7abd6ec632e45.jpg
Simba kwa kiingereza anafahamika kama lion na jina lake la kisayansi (scientific name) anafahamika kama panthera leo na koo(Genus) yake ni panthera, hii koo panthera inajumuisha na wanyama wengine ikiwemo tiger wa bara la asia, chui, American jaguar, na mnyama anaefahamika kama puma au mountain lion.

Simba yupo kwenye order ya wanyama walaji wa nyama almaarufu carnivore na familly yake inaitwa felidae, hii familly ya felidae inajumuisha paka wote wanaopatikana duniani ikiwemo wanaofugwa manyumbani, paka pori, simba, chui, tiger, jaguar na wengineo jamii ya paka ikiwemo cheetah(Duma).

Simba ndiye paka mkubwa Africa na anashika namba mbili duniani baada ya tiger ambaye anapatikana barani Asia pekee dunia nzima na simba pekee ambaye huishi katika makundi miongoni mwa wanyama jamii ya paka na kundi lao linaitwa(pride) pia simba ni wanyama wanaopendelea kuishi maeneo wazi yenye nyasi(Open area) kama ngorongoro crater na Serengeti national park.

Simba pia anafikia hadi uzito wa kg 220-250 kwa dume na upande wa jike ni kg 100-120 na katika familia ya simba ni majikee pekee wanaofanya shughuli ya uwindaji (hunting ) na madume wao hubaki na watoto na majike wakishaua mnyama simba dume ndo huanza kula kisha watoto na baadaye jike ilihali wao ndo wawindaji.

Pia simba ndo wanyama wanaoongoza kwenda fungate (Honeymoon ) na huenda kwa takribani wiki mbili, iko hv kwa kuwa hawa wanaishi katika makundi dume na majike ikitokea katika ile familia kama kuna jike ambaye yuko heat hua anamchukua dume wanaenda mbali kidogo na ile familia kwa ajili ya kufanya mating kwa huo muda wa wiki mbili na kabla ya kwenda fungate kwa kawaida yule jike anayehitaji kwenda fungate na dume huwa anamuwindia dume chakula kizuri chenye mafuta ambacho kitamshibisha yule dume na wakiwa fungate huwa hawali kitu chochote wanakunywa maji tu kwa huo mda wa wiki mbili na huwa wanajamiana kila baada ya dakika saba (sasa ebu fikiria siku ina dakika saba ngapi na kwa huo mda wa wiki mbili dume atampanda jike mara ngapi).

Simba pia hupendelea kuwinda wanyama kama mbogo, pundamlia, nyumbu na baadhi ya swala na kwa kawaida simba dume ana uwezo wa kula hadi Kilo 15 za nyama na akishakula hizo kilo 15 huwa anauwezo wa kukaa siku tatu mpaka wiki moja bila kula halafu ndo anakuja kuwinda tena.

Katika kuwinda kwao wanatumia staili kuu tatu ya kwanza ni sporting ( wanaangalia mnyama wa kumuwinda), ya pili ni stalking ( wananyemelea ) na ya mwisho ni ambush ( kuvamia) na wakishakamata mnyama huwa wanakimbilia kuuma shingoni ili kumbana pumzi(suffocate) na sio kunyonya damu kama wengi wanavyodhani na kwa kawaida simba jike hubeba ukauzito kwa mda wa miezi 3 na anazaa kuanzia watoto 2-4.

Sasa unaweza ukajiuliza kama jike la simba hubeba ujauzito kwa huo mda na kujifungua watoto wengi mbona simba ni wachache? Iko hv hawa wanaishi kwenye makundi dume akimiliki majike wake na huwa hawa madume wenye familia wanachallengiwa na madume ambao hawana familly kwa ajili ya kimiliki zile familly na ikumbukwe sio madume wote wa simba wanamiliki familia sasa ikitokea kwa bahati mbaya huyu simba mwenye family akapigwa na dume mwenzake ambaye hana family huyu dume ambaye hana family atachukua ile family ya yule dume aliyempiga na kuitawala yeye na kwenye ile family akikuta kuna watoto wa yule dume aliyempiga atakachofanya huyu dume atawaua wale watoto wote kwa sababu hawezilea damu isiyoyake na anafanya vile ili jike mwenye wale watoto apatwe na uchungu aingie kwenye heat ili ambebeshe mimba yake na kama kwenye ile familia kuna jike mwenye ujauzito atakachofanya huyu dume atamchukua yule jike atamtoa nje ya family na ataforce kumpanda hadi ile mimba itoke then anampachika mimba yake.

Vile vile hawa simba dunia nzima wanapatikana Africa na Asia na katika bara la asia wanapatikana pale india pekee katika msitu unaoitwa geyforest. Vilevile hawa simba ndo wanyama wanaoongoza kulala kwa siku hulala masaa 16 na kufanya kazi masaa 8 na kawaida wanawinda usiku na wakati mwingine mchana pale hali inaporuhusu na hawa ni wachangamfu mchana na usiku (diurnal and nocturnal ) yaani wao huona usiku na mchana. Huyo ndo bwana simba (king of jungle ) kama wengi wanavyopenda kumwita.
Maisha ya simba kwa wastani ni miaka mingapi?
 
Mkuu huna hadithi inasema simba dume akizeeka simba jike na wanaye humwua , sababu hawataki utegemezi. Je kuna ukweli wowote?
Si kweli!! Kwa kawaida simba dume anayemiliki familia akishazeeka hunyang'anywa ile family na madume pinzani ambao hawana family na yeye atafukuzwa kwenye familia na kwenda kuishi maisha ya kivyake (solitary )
 
Nimeipenda hiyo honeymoon yao tu....halafu kumbe hao madume wana wivu namna hiyo...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom