Fahamu hili, kabla hujasaini mkataba wa ndoa na mwenzi wako

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,701
Siku Ile unasaini Ile karatasi ya mkataba wa ndoa ni siku Muhimu Sana Wenda kuliko siku zote katika maisha yako yote.

Siku hiyo unasaini mkataba wa Mafanikio yako katika awamu mpya ya maisha au mkataba wa kufeli kabisa katika maisha.

Kabla ya kufikiri ni gauni gani utavaa, fikiri Huyu ninayeolewa Naye atasababisha maisha yangu kupanda au kushuka kabisa.

Kabla hujafikiria ukubwa wa harusi yako na suti gani uvae, jiulize Huyu dada ninayeingia Naye huu mkataba atakuwa ndio chanzo Cha anguko langu au kuinuka kwangu.

Lazima ujiulize maswali magumu kabla hujaingia katika ndoa.


Hivyo dondoo hizo zikusaidie

1: Maumivu ya kuvunja ndoa ni makubwa na makali kuliko kuvunja uchumba.

2: Kama ulikuwa husali, angalau Anza kusali Mungu akupe hekima ya kuchagua nani anayekufaa.
Kama ulikuwa unasali mara Moja ongeza angalau mara tatu.

3:Ukivunja ndoa ya kwanza, ndoa au mahusiano ya pili utafiti unaonyesha Huwa ni machungu Zaidi ya Ile ya kwanza.

3: Watu wengi hawana Raha ya ndoa, wanavumiliana tu Kwa sababu ya watoto. Wengi hawakujua ukubwa wa mkataba wanaoingia.

4: Ndoa ni kitu kizuri Sana. Mungu anapenda Sana watu waoe na kuolewa. Shetani anapinga Sana ndoa. Hivyo ndoa yako ikianza na kumtanguliza Mungu, huna hofu za kuogopwa, maisha yatakuwa Raha, na changamoto zitakazojitikeza ni zile zitakazowasogeza karibu Zaidi na kuwaimarisha na sio kuwasambaza.

Muebrania
Mitale na Midimu
 
Back
Top Bottom