Naona Ndoa za Mkataba zitakuja Tanzania, yapi maoni yako?

Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
26,117
34,077
Habarini Wadau,

Kwa namna maisha ya Mahusiano na zaidi ya Ndoa yalivyo kwetu sisi Watu weusi, ninaona kabisa baada ya miaka kadhaa kutakuja kuwepo "Ndoa za Mikataba" yaani watu wanasainishana muda ambao wanataka ndoa zao zisurvive

Ndoa za sasahivi za kidini, yaani za Kikristo na Kiislam na hata za kimila zina changamoto nyingi. Usaliti umekuwa mkubwa na Wanandoa wengi wanaishi na watoto wasio wa Mume au Mke husika katika ndoa

Itafikia ile hali ya makubaliano kuwa tunaoana kwa miaka mitatu tu na nahitaji tuzae watoto wawili then tunaachana kabla ya kugombana au kuuana

Inawezekana pia hii ikaleta ahueni kwa wanawake wengi mitaani wenye umri wa kuolewa na hawana Waume kwani wanajua wanaweza kupata Mume hata atakayeachana na Mkewe

Je Ndoa za Mkataba hazitakuwa ndoa bora kwetu Watanzania?
 
Kwamba tutakaa miaka miwili ,kama hatujapata mtoto basi tunaachana
Kama target ilikuwa ni mtoto, ila pia mnaweza kukubaliana kuishi wawili na kula bata hata msipopata mtoto...then baada ya hapo utamuoa au kuolewa na mwingine wa kuzaa nae
 
Ndoa ni makubaliano ya wawili, kama wakikubaliana waishi hata mwaka mmoja ni wao na makubaliano yao.

Binafsi sipendelei hivyo, mahusiano mazuri ni yenye uhakika wa kuwa pamoja hadi utengano wa ulazima utokee, sio kwa wenzi kuamua.

Japo faida ipo, kila mmoja atakuwa makini kuwezesha ‘kurenew’ mkataba, na pia ambao wataona vigumu kuendelea watapata nafasi ya kuendelea na maisha mengine.
 
Umalaya tu .... Unafikria hata ukiweka miaka 6 hao watoto wataishije ?

Kulelea watoto kwa upande mmoja ni changamoto hata uwe na pesa na ujiandae kwa mambo ya hovyo.
 
Wakati ambapo wote tunakubaliana kifungu cha 'mpaka kifo kitutenganishe' kirekebishwe kuna mitizamo kadhaa.
A. Kuna wanaowaza (kama mleta mada) muda umezidi hivyo upunguzwe, iwe miaka mitatu, mitano nk lakini kikubwa upungue.

B. Na wapo kina sie sasa tunaowaza kwamba muda huo hautoshi hivyo uongezwe. Yaani iwe hadi baada ya kifo🤔. Kama kuna maisha baada ya hapa tuishi tena milele tukimtumikia Mungu pamoja.

Yaani kama mbinguni hakuna kuujaza ulimwengu watoto (so no sex). Hatuhitaji tena kushirikiana atoe yai nitoe mbegu tulete bonge la mtoto.

Hata mbinguni kuna assignment zipo. Mfano kujifunza, kuimba, kuabudu nk. Basi tushirikiane kuijaza mbingu nyimbo na mapambio. Yaani akiandika verse, mi ntafanya mixing ya biti, hivyo vinanda na vinubi tutoe singo kali malaika na wanambingu ni kuserebuka tu. Hit song kwerikweri 😱😆😆😆
 
B. Na wapo kina sie sasa tunaowaza kwamba muda huo hautoshi hivyo uongezwe. Yaani iwe hadi baada ya kifo. Kama kuna maisha baada ya hapa tuishi tena milele tukimtumikia Mungu pamoja.

Yaani kama mbinguni hakuna kuujaza ulimwengu watoto (so no sex). Hatuhitaji tena kushirikiana atoe yai nitoe mbegu tulete bonge la mtoto.

Hata mbinguni kuna assignment zipo. Mfano kujifunza, kuimba, kuabudu nk. Basi tushirikiane kuijaza mbingu nyimbo na mapambio. Yaani akiandika verse, mi ntafanya mixing ya biti, hivyo vinanda na vinubi tutoe singo kali malaika na wanambingu ni kuserebuka tu. Hit song kwerikweri
Kwa wanaowaza hivyo basi hongera kwao
 
Habarini Wadau,

Kwa namna maisha ya Mahusiano na zaidi ya Ndoa yalivyo kwetu sisi Watu weusi, ninaona kabisa baada ya miaka kadhaa kutakuja kuwepo "Ndoa za Mikataba" yaani watu wanasainishana muda ambao wanataka ndoa zao zisurvive

Ndoa za sasahivi za kidini, yaani za Kikristo na Kiislam na hata za kimila zina changamoto nyingi. Usaliti umekuwa mkubwa na Wanandoa wengi wanaishi na watoto wasio wa Mume au Mke husika katika ndoa

Itafikia ile hali ya makubaliano kuwa tunaoana kwa miaka mitatu tu na nahitaji tuzae watoto wawili then tunaachana kabla ya kugombana au kuuana

Inawezekana pia hii ikaleta ahueni kwa wanawake wengi mitaani wenye umri wa kuolewa na hawana Waume kwani wanajua wanaweza kupata Mume hata atakayeachana na Mkewe

Je Ndoa za Mkataba hazitakuwa ndoa bora kwetu Watanzania?
naunga mkono hoja hii, ndoa za mikataba ni nzuri na zitasadia kuondoa sintofahamu baina ya wanandoa.
mmi naanza, wewe je?
 
Wakati ambapo wote tunakubaliana kifungu cha 'mpaka kifo kitutenganishe' kirekebishwe kuna mitizamo kadhaa.
A. Kuna wanaowaza (kama mleta mada) muda umezidi hivyo upunguzwe, iwe miaka mitatu, mitano nk lakini kikubwa upungue.

B. Na wapo kina sie sasa tunaowaza kwamba muda huo hautoshi hivyo uongezwe. Yaani iwe hadi baada ya kifo🤔. Kama kuna maisha baada ya hapa tuishi tena milele tukimtumikia Mungu pamoja.

Yaani kama mbinguni hakuna kuujaza ulimwengu watoto (so no sex). Hatuhitaji tena kushirikiana atoe yai nitoe mbegu tulete bonge la mtoto.

Hata mbinguni kuna assignment zipo. Mfano kujifunza, kuimba, kuabudu nk. Basi tushirikiane kuijaza mbingu nyimbo na mapambio. Yaani akiandika verse, mi ntafanya mixing ya biti, hivyo vinanda na vinubi tutoe singo kali malaika na wanambingu ni kuserebuka tu. Hit song kwerikweri 😱😆😆😆
Mimi pia ni hao akina sie, naungana na wewe.

Milele ndio mpango, kuishi nikijua tunaachana baada ya muda fulani ina maana gani kuishi pamoja?
Bora kila mtu aishi kivyake iwe ni kukutana tu kila mtu arudi kwake.
 
Ndoa ni makubaliano ya wawili, kama wakikubaliana waishi hata mwaka mmoja ni wao na makubaliano yao.

Binafsi sipendelei hivyo, mahusiano mazuri ni yenye uhakika wa kuwa pamoja hadi utengano wa ulazima utokee, sio kwa wenzi kuamua.

Japo faida ipo, kila mmoja atakuwa makini kuwezesha ‘kurenew’ mkataba, na pia ambao wataona vigumu kuendelea watapata nafasi ya kuendelea na maisha mengine.
Ndoa za mkataba wengi hufilisika hasa wanaume

Sababu mwanamke anamchuna to.the maximum na wakiachana lazima ampe kiinua mgohgo
 
Inategemea na Sheria za ndoa katika nchi husika

Kwa mfano kwa Waislam sidhani kama kuna kitu kama hicho, japo ikifungwa haitakuwa ya kidini tena
 
Back
Top Bottom