Facts Check: CCM Vs CHADEMA (Tulinganishe Sera, Itikadi, Uadilifu, Uwajibikaji)

Facts Check: CCM Vs CHADEMA (Tulinganishe Sera, Itikadi, Uadilifu, Uwajibikaji)

CHADEMA ni genge la wateule waliodhamiria kuigawa nchi vipande vipande kupitia kivuli cha siasa. CCM ni mkusanyiko wa watanzania kutoka makundi mbalimbali pande zote za nchi

kwenye RED kusanyiko lililona na makusudi yafuatayo:-

1. Kuhakikisha hifidhi zetu za wanyama zibaki bila wanyama.
2. Maeneno yote yenye madini yabaki mashimo yasiyo na madini.
3. Madaktari na waandishi wetu wa habari wabaki bila kucha, meno n.k
4.Na mengineyo mengi.............. hayo makundi yaliyokusanywa na hiyo kitu kwenye blue ni hatari yafaa tushirikiane kuitokomeza.
 
Chadema siyo chama cha siasa ni kikundi cha watu fulani ambacho kinatumia mwamvuli wa siasa kufanyia mambo yake.

Kwa uelewa wangu CCM ni genge la wahuni majambazi mafisadi wauaji na watekaji wasiojali maisha na utu wa watanzania zaidi ya maslahi yao Wakati CDM niwatetezi wa watanzania wenye kujali maisha ya watanzania.CDM ndo ukombozi wa taifa hili.
 
Ndugu zangu tujikite kuzichambua Sera za CCM na CHADEMA kwenye Madini, ardhi, Elimu, Afya, kilimo, michezo, Uvuvi, Ufugaji, Uadilifu, uwajibikaji, ulinzi na Usalama, Uwekezaji nk... Haya maeneo yatatusaidia sana kujua pumba na mchele coming 2015...
 
Hapa nimetoka "kapa"...!

Mlinganyo unafanyika vipi wakati ccm wana dola na chadema wanataka kukamata dola?
 
Hapa nimetoka "kapa"...!

Mlinganyo unafanyika vipi wakati ccm wana dola na chadema wanataka kukamata dola?

kweli kabisa sisi tunataka utekelezaji sio sera ....ccm wanatakiwa watekeleze sera kitu ambacho wameshindwa mpaka sasa ushahidi fuatilia bunge .....ilani yao ya uchaguzi ni zero...hata budget tu wanayo panga huwa haifiki hata 20% lakini inayofuata wanapanga tena madudu yaleyale ndio maana mpaka leo kila mbunge anazungumzia maji hakuna
 
Siasa za Tanzania kwa sasa zimekumbwa na upotoshwaji mwingi ndani yake. Ni nadra sana kuwakuta wenye dhamana wakinadi sera za vyama vyao, wengi wao wamejikita zaidi kwenye vijembe na wakati mwingine huwa wanaporomosha matusi mazito ya nguoni!

Sisi wananchi wa kawaida hatuhitaji matusi na mifarakano bali tunahitaji sera nzuri ya kutuletea maendelea yanayoshabihiana na Rasilimali ambazo Mwenyeezi Mungu ametujaalia...Tuna hitaji Itikadi itakayotuunganisha badala ya kutugawa Watanzania. Tunahitaji viongozi Waadilifu. Tunahitaji Serikali itakayowajibika kwa wananchi na si kwa wanyonyaji wachache wenye kutumia mgongo wa uwekezaji.

Uzi huu unajikita katika kulinganisha Sera, Itikadi, Uwajibikaji na Uadilifu wa Vyama Vikuu Shindani CCM na CHADEMA ktk kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa 2015 CCM na CHADEMA... Naomba tujikite zaidi kwenye mada. Matusi na jazba zisizo na msingi tujaribu kuepukana nazo.

karibuni GTs tufanye Facts Checkup bila ya kujali ushabiki wa kisiasa kwa manufaa ya nchi yetu na watu wetu ..Only facts ndizo zinazohitajika kwenye maeneo yafuatayo:-

1.Sera ya Muungano
2.Mfumo wa uendeshaji wa serikali Serikali (uliopo vs Majimbo)
3. Sera ya Uwekezaji na Uwazi kwenye mikataba inayoingiwa
4. Uadilifu
5. Uwajibikaji
6. Sera ya kilimo
7. Sera ya Madini
8. Mali asili na Utalii
9. Sera ya Elimu
10. Sera ya Afya
11. Sera ya Ufugaji
12. Sera ya uvuvi
13. Sera ya Michezo
14. Mishahara ya Wafanyakazi
15. Ukusanyaji wa Kodi
16. sera ya ardhi
17. Sera ya Nyumba na Makazi
18. Uwezeshwaji wa wananchi
19. Sera ya Rasilimali watu
20. Ulinzi na usalama

ANGALIZO MUHIMU: Hapa ni CCM Vs CHADEMA pekee...

Mkuu Ilboru,

Nakubaliana sana nawe katika kuleta uzi huu hapa JF,lakini wakati unauleta uzi huu ungefanya kwanza utafiti ili uweze kujua kama kuna waraka ama tamko lolote mbali na alilotoa aliyekuwa katibu mkuu mh. mzee Makamba la kupiga marufuku wana CCM kukaa kwenye panel au mdahalo kunadi sera za chama chao.

Nijikite kwenye mada husika moja kwa moja,CDM wanaamini ili kuwa na muungano ulio imara ni bora kuirudisha serikali ya Tanganyika ambayo itaungana na serikali ya mapinduzi Zanzibar kuunda JMT,seikali ya JMT itahusika na mambo ya muungano tu na hizi serikali mbili zitahusika na mambo ya ndani ya nchi zao japokuwa kuna mambo ambayo watakuwa wamekubaliana katika muungano watayasimamia kwa pamoja,hali inakubalika kwa pande zote za JMT.

CCM ni waumini wa muungano wa serikali mbili ambao wao wanaamini ndiyo njia pekee ya kudumisha mustakabali wa amani ya nchi hii ilihali dalili na mawingu ya uvunjivu wa amani yametanda kwa wingu jeusi.Lakini pia muundo huu wa serikali mbili wao wanauona una tija cha msingi ni kuziba mpasuko ulioko,hali inayopingwa na kila upande wa JMT

Sera ya uwendeshaji serikali ya majimbo ni mfumo ambao serikali ya CCM unaupinga kwa kigezo ambacho kinatumika kuwagawa wananchi na kuonyesha hawana sababu za msingi ambazo wanaweza kusimamia,lakini kwa upande wa CDM wanaamini mfumo huu ni mzuri kiuendeshaji serikali kutokana na kuwa serikali hii ya mfumo wa majimbo unarudisha madaraka kwa wananchi kuanzia ngazi ya chini,lakini si kurudisha madaraka tu bali kulinda na kusimamia rasiliamali za taifa kwa manufaa ya Watanzania na ndiyo dawa yenye tija kwa kudhibiti ufisadi wa amali ya umma.

CCM wanaamini katika usiri wa mikataba na wawekezaji,hali inayopeleka ufisadi kuibuka kwa kishindo na kuibua pengo la wenye nacho na wasi nacho kuongezeka siku hadi siku.CDM wanaamini uwazi wa mikataba ndiyo suluhisho pekee kwa mustakabali wa rasiliamli za taifa na watu wake lakini pia ndiyo njia pekee ambayo inaweza kusaidia kuto kukuwa kwa deni la taifa kutokana na mikataba mingi kutokuwa na tija kwa taifa na yenye kujaa wingi wa usiri unaopelekea watu wachache kujimilikisha rasilimali za taifa na kuzifanya mali za familia.
 
nyie mko tanzania ipi kampuni zinasajiliwa pale jengo la ushirika mnazi mmoja kwa ......................nimesahau jina hapo nikikumbuka nitawatajia
Kampuni siku hizi zinasajiliwa kwa msajili wa vyama vya siasa? mtake radhi Mzee Tendwa tafadhali..
 
Mafilili,
Naona usipomtaja Slaa siku yako haiingii. Kama nilivyotamka kwenye thread nyingine, wewe ni mwongo, mzushi na mchonganishi. Ni mvivu wa utafiti au unayoyasema unafanya hivyo kwa malengo machafu. Chadema hakuna uamuzi hata mmoja, anaufanya Mbowe, au Slaa ambao haukupitishwa na vikao vya Kikatiba, ikiwa ni pamoja na Mshahara wa Dr Slaa. Niliku challenge, hapo juu kuwa, weka hadharani mshahara wa Wabunge, posho zao, na kisha weka hadharani wa Dr Slaa ili watanzania walinganishe Kama inafanana. Wrong major or Minor wrong conclusion, sijui tatizo lako ni kisomo au bangi? Hujafanya utafiti huna haki ya kuzungumza au kuchangia. Upotoshwaji hautavumiliwabtena Chadema, tutaujibu hapo hapo ili walio wanyofu wasije kupotoshwa.



Mkuu hata wewe? Woga wa nini? Utake usitake CHADEMA imesajiliwa na inawabunge wakutosha kuongoza upinzani Bungeni...
Tujikite kwenye mada! Vipi sera ya CCM Kuhusu hayo niliyoyaorodhesha hapo Juu?...Nape pia anakaribishwa humu kwa ufafanuzi zaidi...

Mbowe pasipo kushirikisha vikao vya maamuzi; AMEPITISHA DR. SLAA ALIPWE MSHAHARA NA MARUPURUPU SAWA NA WABUNGE kupitia fedha za ruzuku
 
Mafilili,
Naona usipomtaja Slaa siku yako haiingii. Kama nilivyotamka kwenye thread nyingine, wewe ni mwongo, mzushi na mchonganishi. Ni mvivu wa utafiti au unayoyasema unafanya hivyo kwa malengo machafu. Chadema hakuna uamuzi hata mmoja, anaufanya Mbowe, au Slaa ambao haukupitishwa na vikao vya Kikatiba, ikiwa ni pamoja na Mshahara wa Dr Slaa. Niliku challenge, hapo juu kuwa, weka hadharani mshahara wa Wabunge, posho zao, na kisha weka hadharani wa Dr Slaa ili watanzania walinganishe Kama inafanana. Wrong major or Minor wrong conclusion, sijui tatizo lako ni kisomo au bangi? Hujafanya utafiti huna haki ya kuzungumza au kuchangia. Upotoshwaji hautavumiliwabtena Chadema, tutaujibu hapo hapo ili walio wanyofu wasije kupotoshwa.

Hahahahahahaha hii imenichekesha sana. Dah, Josephine kashatuharibia kiongozi kwa tamaa zake za kuwa first lady!!!
 
Maamuzi makubwa hufanywa na watu wachache mfano Mbowe katangaza rasmi kuwa Dr. Slaa ni mgombea wa URAIS kupitia CDM mwaka 2015
CCM wanafanya maamuzi makubwa yepi ndugu, hayo maamuzi ya wengi CCM uhalalishwa kwa Rushwa bila matakwa halisi ya wapiga Kura, kumbuka Kikwete alifanya nini wakati anataka kuwa mgombea akina Rostam, Lowasa mwanzo walizunguka nchi nzima kumnadi kikwete na pia hao hao walitumia fedha nyingi kuwarubuni wajumbe pale Dodoma kwa maana hiyo nafuu ya tamko la mbowe kuliko kuwaadaa wananchi kuwa mnafuata Demokrasia wakati ni Rushwa tu inayotembea, na je kwa nini Mangula alitamka kuwa wale Viongozi wote waliochaguliwa kwa Rushwa atawashughulikia kwa miezi sita lakini hadi sasa kimya.
 
We mwehu Mafilili inamana hapo ndio upeo wako wa kufikiria umefika mwisho au ni hzo buku7 zinakuzuzua.Mwangalie kiongozi mwenzako Mwingulu kapiga kelele kuona watanzania hawamsapoti kawa kimya.
 
ccm kwa sasa ndio wameshika dola,zaidi ya nusu karne sasa,chadema ni wapinzani rasmi na bado wachanga but challenging, kuhusu ulinganifu wa policy na philosophy na utekelezaji wake, naweza kugeneralize kwamba mpaka sasa ccm ni failures,maana hata falsafa ya chama haijulikani ni ipi,achilia mbali sera zisizotekelezeka,,kwa trend hii wanakwenda kufa,,chadema wakipunguza kuitilafiana wakajenga chama from the grassroots,wanaweza kutuletea kesho iliyo bora zaidi
 
Chadema siyo chama cha siasa ni kikundi cha watu fulani ambacho kinatumia mwamvuli wa siasa kufanyia mambo yake.

Hicho kikundi kimesajiliwa na ofisi ya vyama vya siasa au ni ofisi ya makamu wa rais?
 
Watu wa Tunduma walifurahi sana kusikia sera hizi. Dr. Slaa kama kawaida yake akawachangisha hela halafu akaingia mitini. Slaa hana tofauti na Diamond maana wote wakitoka jukwaani mifuko yao inatuna.

Hivi under Diamond nako watanzania walipitishiwa ndoo na wakachangia!!! tena kwa hiyari yao? Duh kama ni hivyo nawashangaa wanaoshindwa kuweka ripoti wazi.
 
Mafilili,
Naona usipomtaja Slaa siku yako haiingii. Kama nilivyotamka kwenye thread nyingine, wewe ni mwongo, mzushi na mchonganishi. Ni mvivu wa utafiti au unayoyasema unafanya hivyo kwa malengo machafu. Chadema hakuna uamuzi hata mmoja, anaufanya Mbowe, au Slaa ambao haukupitishwa na vikao vya Kikatiba, ikiwa ni pamoja na Mshahara wa Dr Slaa. Niliku challenge, hapo juu kuwa, weka hadharani mshahara wa Wabunge, posho zao, na kisha weka hadharani wa Dr Slaa ili watanzania walinganishe Kama inafanana. Wrong major or Minor wrong conclusion, sijui tatizo lako ni kisomo au bangi? Hujafanya utafiti huna haki ya kuzungumza au kuchangia. Upotoshwaji hautavumiliwabtena Chadema, tutaujibu hapo hapo ili walio wanyofu wasije kupotoshwa.

Dr Slaa karibu sana Mkuu, MAFILILI humu ndani wanamjua sana wala haina haja ya kubishana nae...Nashauri Mpotezee tu kwani malengo yao yanajulikana...
Back kwenye mada...Mkuu kwa nafasi yako tutashukuru sana tukipata sera za CHADEMA, itikadi na mikakati mbalimbali mliyowaandalia wananchi pindi mkipewa ridhaa ya kuongoza nchi...Lengo letu hapa ni kushindanisha sera na mikakati ya utekelezaji wa wake kwenye Madini, Kilimo, Elimu, Utalii, Ulinzi na Usalama, Afya, nk...
 
Hivi wabunge wa Chadema pale bungeni wapo wangapi vile? Mwenye data anipe na wa CCM pia. Nadhan watakuwa nusu kwa nusu kwa mchakamchaka huu!!!?
 
Zinatekelezeka ama hazitekelezeki?...

Hiyo muulize aliyezitoa kwa sababu yeye ndio anajua mahesabu aliyopiga ya kufuta kodi na kuongeza matumizi. Huwezi kujua labda ameoteshwa muujiza wa kikombe kujaza pipa.
 
Back
Top Bottom