Facts Check: CCM Vs CHADEMA (Tulinganishe Sera, Itikadi, Uadilifu, Uwajibikaji)

Facts Check: CCM Vs CHADEMA (Tulinganishe Sera, Itikadi, Uadilifu, Uwajibikaji)

CCM ni wazuri kwa kudumisha amani na utulivu huku wakivumilia matusi na maneno ya dhihaki toka kwa viongozi wa CDM
Funguka zaidi Mkuu kuhusiana na sera za CCM kwenye Kilimo, afya, Uwekezaji na mengineyo...
 
Hapo penye RED CDM wanatupeleka pabaya hawana utashi wa kudumisha amani, wanapendelea nchi isitawalike.
Na. 21: SERA za MAMBO YA NJE: CDM wamefungamana na chama cha kidini Christian Democratic Party na chama kinachounga mkono USHOGA
Mkuu hapa uko kwenye facts check siyo porojo, Mwaga data hapa ni kwa jinsi gani CHADEMA wanasababisha nchi isitawalike, Chama cha CDP na Conservative vinatofauti gani na Vyama vya Republican na Labour kinacho iunga mkono CCM?... Mwaga facts mkuu...
 

CHADEMA ni chama cha itikadi ya MRENGO WAKATI (center party)kinachojenga na kuimarisha uchumi wa soko huru, biasharahuru na sekta ya watu binafsi bila kupoka mamlaka ya umma katika maeneo nyetihususani pale penye hitilafu ya soko au penye maeneo nyeti ya kiuchumi. wakatiCCM ni chama kinacho jenga ujamaa na Kujitegemea.



Wewe acha kutumia fikra zako Chadema wenyewe wanasema Chadema ni chama cha kibepari.

Cha kushangaza wanasema wao ni chama cha kibepari wakati huo huo kina urafiki na vyama vya kihafidhina huko Ulaya na Marekani.

Hayo uliyoandika ni kwa maslahi ya nani.
 
Funguka zaidi Mkuu kuhusiana na sera za CCM kwenye Kilimo, afya, Uwekezaji na mengineyo...

Kilimo: Kilimo Kwanza ni mkombozi wa mkulima mdogo kwa vile kinamsogezea zana za kilimo na pembejeo karibu na mkulima, masoko ya mazao ya kilimo yameboreshwa.

Afya: Zahanati na vituo vya afya zimeongezeka na maboresho yameonekana; vyandarua vimetolewa nchi nzima, hospital za rufaa kila mkoa. Idadi ya watumishi wa Afya imeongezeka.

Uwekezaji: Idadi ya wawekezaji wa ndani na nje wameongezeka kutokana na kuwepo kwa mazingira yanayovutia uwekezaji katika madini na gesi
 
Kungekuwa na makabrasha(sera) kwanza tukapima kama makabrsha(sera) yana mashiko, then tukawapima kila mmoja against makabrasha yake.

Ccm tumeshaona utendaji wao, cdm tutawapimaje utendaji wakati hawajawahi kuongoza? Au tunapima uongozi ndani ya chama si kiserikali?

Tutapimaje facts bila kuwa na facts zenyewe? Au tunapima tu vile twajisikia?
 
Mleta mada umekosea; SI BUSARA KULINGANISHA mlima na kichuguu; mara nyingine jaribu kulinganisha CDM na TLP vipo katika kundi moja;-
1. Vyama vya Upinzani
2. Wenyeviti wanatoka mkoa mmoja
 

CHADEMA ni chama cha itikadi ya MRENGO WAKATI (center party)kinachojenga na kuimarisha uchumi wa soko huru, biasharahuru na sekta ya watu binafsi bila kupoka mamlaka ya umma katika maeneo nyetihususani pale penye hitilafu ya soko au penye maeneo nyeti ya kiuchumi. wakatiCCM ni chama kinacho jenga ujamaa na Kujitegemea.



mkuu, mbona unaongea kinyumenyume?
 
Chadema siyo chama cha siasa ni kikundi cha watu fulani ambacho kinatumia mwamvuli wa siasa kufanyia mambo yake.[/QUOTE

Wakati fulani unatakiwa kuwa serious na kutumia akili yako vizuri ili upate thawabu kwa mujibu wa imani yako!!

Thawabu zinapatikana kwa kuisifia Chadema,

Huwezi kulinganisha mlima kilimanjaro na mlima tegeta.

Chadema rika lake kina CUF. NCCR Mageuzi. TADEA.
 
Mleta mada umekosea; SI BUSARA KULINGANISHA mlima na kichuguu; mara nyingine jaribu kulinganisha CDM na TLP vipo katika kundi moja;-
1. Vyama vya Upinzani
2. Wenyeviti wanatoka mkoa mmoja

sure mkuu, pia wenyeviti wa vyama wote ni wachaga. hata ukichukua NCCR MAGEUZI pia hufanana na chadema maana wenyeviti pia ni wachaga
 
Kilimo: Kilimo Kwanza ni mkombozi wa mkulima mdogo kwa vile kinamsogezea zana za kilimo na pembejeo karibu na mkulima, masoko ya mazao ya kilimo yameboreshwa.

Afya: Zahanati na vituo vya afya zimeongezeka na maboresho yameonekana; vyandarua vimetolewa nchi nzima, hospital za rufaa kila mkoa. Idadi ya watumishi wa Afya imeongezeka.


Uwekezaji: Idadi ya wawekezaji wa ndani na nje wameongezeka kutokana na kuwepo kwa mazingira yanayovutia uwekezaji katika madini na gesi

Mkuu hii nchi yenye mambo yote hayo kwenye red ipo wapi na mimi nikaishimo
 
Wewe acha kutumia fikra zako Chadema wenyewe wanasema Chadema ni chama cha kibepari.

Cha kushangaza wanasema wao ni chama cha kibepari wakati huo huo kina urafiki na vyama vya kihafidhina huko Ulaya na Marekani.

Hayo uliyoandika ni kwa maslahi ya nani.
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
(CHADEMA)
​

KATIBA​

3.B. Itikadi ya CHADEMA
3.1.1CHADEMA ni chama cha itikadi ya MRENGO WA KATI (center party).

3.1.2CHADEMA ni chama kinachoamini kukuza na kuimarisha uchumi wa nchi kwa kutumia
raslimali zanchi yetu bila kuathiri uhuru wa Taifa, na kuhakikisha kuwa umma kwa
ujumlaunanufaika na raslimali zao.

3.1.3CHADEMA inaamini katika kujenga na kuimarisha uchumi wa soko huru,
utakaoheshimuna kulinda haki na mali za watu, biashara huru na sekta ya watu binafsi
bila kupokamamlaka ya umma katika maeneo nyeti hususani pale penye hitilafu ya soko
au penyemaeneo nyeti ya kiuchumi. Tunaamini katika soko huru sio soko holela.

3.1.4CHADEMA inaamini kuhakikisha matumizi bora ya raslimali asilia za nchi ilizichangie
kikamilifukatika pato la taifa na hasa kuboresha huduma za kiuchumi zinazotumiwa na
wananchiwote.

3.1.5CHADEMA inaamini katika uzalendo na kuthamini mila na desturi zetu zilizonzuri.

3.1.6CHADEMA inaamini katika uhuru chini ya sheria zilizo za haki.

3.1.7CHADEMA inaamini katika siasa ambazo ziko juu ya vyama zenye kusimamia zaidi
maslahi yaTaifa.

3.1.8CHADEMA inaweka umuhimu wa pekee katika familia kama moja ya taasisi muhimu
ya kijamii.

3.1.9CHADEMA inaamini katika umuhimu wa uhuru wa kuamini katika kujenga maadili ya
mwanajamiimmoja mmoja bila kuifanya dini kuwa sehemu ya dola.

3.1.10CHADEMA inaamini taifa linaundwa na watu, hivyo uhai wake unawategemea watu, na
mabadilikoyake yanatokana na watu.

3.1.11CHADEMA inaamini katika kujenga uwezo wa wazawa katika kumiliki na kuendesha
uchumi.

Umeelewa? au bado kuna vitu vinakuchanganya!Kwa sababu wanadamu tunatofautiana mno.
 
Chadema siyo chama cha siasa ni kikundi cha watu fulani ambacho kinatumia mwamvuli wa siasa kufanyia mambo yake.
mambo yapi hayo ya kukutea wewe usinyonywe na majangiri
 
Wewe acha kutumia fikra zako Chadema wenyewe wanasema Chadema ni chama cha kibepari.

Cha kushangaza wanasema wao ni chama cha kibepari wakati huo huo kina urafiki na vyama vya kihafidhina huko Ulaya na Marekani.

Hayo uliyoandika ni kwa maslahi ya nani.

sure mkuu, ili upendwe chadema sharti ukumbatie ubepari
 
Sera za ccm ni kudhofisha elimu, kuwapa wazungu madini, kuuza maliasili zote, ardhi, meno ya tembo, viongozi kutibiwa nj
 
Hapo penye RED CDM wanatupeleka pabaya hawana utashi wa kudumisha amani, wanapendelea nchi isitawalike.
Na. 21: SERA za MAMBO YA NJE: CDM wamefungamana na chama cha kidini Christian Democratic Party na chama kinachounga mkono USHOGA
Mwenzetu uko kwenye porojo.

Hivi hii picha hapa inahusika na kudumisha Amani ya Tanzania?

attachment.php


Msiwadharau watanzania kiasi hiki.
 
Kilimo: Kilimo Kwanza ni mkombozi wa mkulima mdogo kwa vile kinamsogezea zana za kilimo na pembejeo karibu na mkulima, masoko ya mazao ya kilimo yameboreshwa.

Afya: Zahanati na vituo vya afya zimeongezeka na maboresho yameonekana; vyandarua vimetolewa nchi nzima, hospital za rufaa kila mkoa. Idadi ya watumishi wa Afya imeongezeka.

Uwekezaji: Idadi ya wawekezaji wa ndani na nje wameongezeka kutokana na kuwepo kwa mazingira yanayovutia uwekezaji katika madini na gesi

Mkuu tunahitaji something tangible! Kilimo kimekuza uchumi kwa % ngapi toka sera ya kilimo kwanza iasisiwe, Wakulima hawakopwi tena? mbona huko kusini wanaandamana? Mbona wakulima wa Pamba wanalalamika? Tuambie contribution ya kilimo kwenye pato la Taifa...
Afya za wananchi zimeboreka? Madaktari wanapata vitendea kazi? wanalipwa stahili zao? vifo vya akina mama na watoto vimepungua kwa % ngapi? Madawa yanapatikana kwa walengwa? Wangapi wana access kwenye hizo hospital? Wananchi wangapi wako covered kwenye mpango wa medicare?...
Uwekezaji umeongeza GDP kwa % Ngapi? Tupe mchanganue wa Michango ya:- Dhahabu, Tanzanite, Uranium, Nickel, Gypsum, Coal, Chuma, Almasi, Gesi, Uwindaji, Viwanda, kilimo, Uvuvi, Ufugaji na mitandao ya simu...
Facts tu ndo tunazozihitaji mkuu....CHADEMA watuambie watatufanyia nini kwenye hayo maeneo endapo watapewa nchi kuongoza...Projections zinawezekana kabisa...sisi tuko hapa kuangalia viability...
 
Mwenzetu uko kwenye porojo.

Hivi hii picha hapa inahusika na kudumisha Amani ya Tanzania?

attachment.php


Msiwadharau watanzania kiasi hiki.
Safi sana... Facts tu ndo tunaziangalia hapa. Kwa matakwa ya uzi huu, mkuu tuwekee sera ya CDM kuhusiana na Ulinzi na Usalama ili Tulinganishe na ya CCM...
 
Mleta mada umekosea; SI BUSARA KULINGANISHA mlima na kichuguu; mara nyingine jaribu kulinganisha CDM na TLP vipo katika kundi moja;-
1. Vyama vya Upinzani
2. Wenyeviti wanatoka mkoa mmoja


 
Sera za ccm ni kudhofisha elimu, kuwapa wazungu madini, kuuza maliasili zote, ardhi, meno ya tembo, viongozi kutibiwa nj

Mkuu Swaswa, yawezekana kabisa una point, ebu tufafanulie so far Wamedhoofisha Elimu kivipi kwa kiasi gani? natambua kuwa ni kweli 60% wamefeli, Mishahara ya walimu Ikoje? Inakidhi mahitaji yao muhimu?
Wazungu ni kweli wanachukua more than 98% ya madini yetu! So far wameshasafirisha Dhahabu kiasi gani? yenye thamani gani? figure ni muhimu Mkuu...
Maliasili zilizouzwa ni zipi? kwa kiasi gani? Ardhi kiasi gani imekwapuliwa so far? nani wamechukua hiyo ardhi? wapi? So far Tani ngapi za meno ya Tembo zimekamatwa? Viongozi wangapi wanatibiwa nje ya nchi? kwanini wasitibiwe hapa kwetu?.. CHADEMA wanasemaje sera zao kuhusiana na Madini, maliasili, Ardhi?....
 
Back
Top Bottom