Facebook wamefeli kuhusu tukio la Ufaransa

Facebook wamefeli kuhusu tukio la Ufaransa

mossad007

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
1,165
Reaction score
852
Mtandao wa Facebook una users karibuni billion moja na million 400 na kati ya hao Users toka Africa ni wengi kiasi cha robo nzima.

Hivi jana yametokea mashambulizi ya kigaidi nchini Ufaransa na katika kuonyesha solidarity Facebook wameweka special icon ya mtu kuweka bendera ya Ufaransa (transparent) plus picha yako ili iwe profile picture.

Utaratibu huu ni mzuri ukizingatia unaonyesha solidarity katika janga lililowakumba ndugu zetu. Lakin April 2 2015 lilitokea shambulizi lilichukua maisha ya watu wengi zaid kuliko hata hili huko Garissa Kenya kana kwamba ni tukio la kawaida hakukuwa na bendera ya Kenya wala special privilledge kwa watu wa Kenya.

Hapa nadiriki kusema Facebook wanaonyesha kulemewa na itikadi za ukanda, ubaguzi, kutokua na usawa ilhali Wakenya ni moja ya mataifa makubwa yenye watumiaji wengi Facebook Africa baada ya South Africa na Nigeria of which ni wachangiaji wakubwa wa pato la Facebook.

Hii ndio picture halisi ya hali ilivyo kati ya mataifa ya Ulaya na Africa ingawa wanajitahidi sana kupaint ionekane wako concerned na kuna concern kubwa lakin Genocide za Rwanda na Burundi, vita za Wenyewe kwa wenyewe na vifo vya wapigania Uhuru kama Lumumba na Nkurhuma ni ushahidi tosha kuwa mikono na fikra zao hazina huruma wala concern dhidi ya waafrika.
 
ni mali yao na watafanya chochote watakachotaka huwezi kuwazuia

Africa tufungue ya kwetu na sisi ya kutu connect waafrica
 
Kwahiyo unatakaje, wao wamekaa darasani na kubuni facebook, kwenu Tanzania mmebuni nini cha maana
 
tatizo la waafrica ni viongozi wabovu tuna watu wanaweza kuanzisha mitandao ya kuunganisha waafrica lakini serekali za africa watazifunga kama zinasema maovu yao, sijaona kiongozi wa africa mwenye ndoto za kuwajenga wanachi wake ili waweze kupambana ktk ulimwengu, wala hawana ndoto za kujenga mataifa yao yawe makubwa kiuchumi,kisiasa na kijamii, wao ni kuiba na wanafurahi kuona watu wao wakiwa maskini, ili waendelee kuiba na kuwafanya watumwa
 
Huu utamaduni wa kupenda kulalamika kuwa hufanyiwi hivi au vile na watu wengine ndio umetulemaza sana waafrika. ni muda wa kubadilika sasa.
 
Nakumbuka miaka ya tisini wakati kuna mgogoro mkubwa wa wakimbizi toka Rwanda na Burundi, wakati huo huo kulikuwa na tifu la wakimbizi huko Balkan state(Sarajevo, Bosinia nk) Unafiki wa wazungu sasa, wale wakimbizi wa ulaya mashariki walikuwa wanapewa mkata, siagi, nyama, maji ya chupa na vyote vizuri. Hawa waafrika ilikuwa ni makande na maji ya bomba, duh kipindu pindu sasa.
 
Akifa mzungu mmoja sawa na waAfrica 100" mitandao yao kila kitu chao cc niwatumiaji tu kwaio tuvunge hatuna chetu
 
Back
Top Bottom