Facebook nayo yaitimua Huawei kwenye huduma zake

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Kampuni ya Facebook, Marekani China, simu za Huawei,

Kampuni ya Facebook imeingia rasmi katika vita vya kiuchumi baina ya Marekani na China ikizuia huduma wezeshi (APP) zake kutumika katika simu za Huawei.

Zuio hilo linalenga huduma mama ya Facebook na nyingine kutoka kwa kampuni washirika ambazo ni WhatsApp na Instagram.

Hatua hiyo inafuatia uamuzi wa Marekani mwezi Mei kuzuia kampuni za Marekani kutumia huduma za Huawei kutoka China, ikieleza ni “sababu za kiusalama”.

Hata hivyo, watu ambao tayari wamenunua simu za Huawei na wanapata huduma husika wataendelea kuzitumia isipokuwa wale wapya.

Facebook imesema pia itaendelea kusambaza huduma za kuweka mambo mapya (updates) kwa wamiliki wa sasa wa simu za Huawei.

Kampuni ya Huawei haijatoa taarifa yoyote kuhusu uamuzi huo wa Facebook.

Uamuzi huo unawahusu wateja ambao tayari walikuwa wanatumia huduma hizo na si wale wanaotaka kupakua pale wanapotaka kuanza kutumia simu mpya za Huawei.
 
Unapotosha. Katazo hili linasema apps za FB, Whatsapp na IG hazitakuwa zimeingizwa kwenye simu mpya za Huawei, lkn ukishanunua simu mpya ya Huawei unaweza kwenda Playstore uka download FB, Whatsapp na IG bila matatizo na zikafanya kazi. Kwahiyo, kama ukinunua simu mpya za Huawei unaweza ku download FB, Whatsapp na IG mwenyewe aka manual downloading.
 
Playstore ipi na Google walikuwa wa kwanza kucomply na Ban ya serikali?
 
Simu za Huawei zilizo sokoni kwa sasa haziguswi na ban ya Google services kama Playstore. Hiyo Google ban ni kwa models mpya za simu za Huawei ambazo watakuja nazo in the future.
 
Unapotosha. Katazo hili linasema apps za FB, Whatsapp na IG hazitakuwa zimeingizwa kwenye simu mpya za Huawei, lkn ukishanunua simu mpya ya Huawei unaweza kwenda Playstore uka download FB, Whatsapp na IG bila matatizo na zikafanya kazi. Kwahiyo, kama ukinunua simu mpya za Huawei unaweza ku download FB, Whatsapp na IG mwenyewe aka manual downloading.
We ndo hujaelewa sasa....unajua playstore ni mali ya google?...unajua kwamba google ndo wakwanza kutii agizo la serikali ya marekani kuvunja uhusiano na huawei?

Usinunue tena simu za huawei kama huna m'badala wa kufanya la sivyo hutatumia app yeyote inayopatikana google playstore.
 
Back
Top Bottom