Uchaguzi 2020 EXCLUSIVE: Maswali kwa Mgombea Urais wa JMT, Tundu Lissu kutoka kwa Watanzania watumiao mitandao ya kijamii

Status
Not open for further replies.
Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu wa haki aliekutetea pale Dodoma walipotaka kukunyang'anya uhai wako lakini wakashindwa! Asante Mwenyezi Mungu kwa zawadi ya uzima wa Rais wetu.

Swali 1:
Mh. Kuna baadhi ya watanzania ambao hawakusoma lakini Wana ujuzi, Kuna wale wameishia njiani hawakumaliza formfour, hawana vyeti vya shule lakini wanajua kusoma na kuandika vizuri lakini hawawezi kuajiriwa na serikali, mfano madereva, mafundi na watu kama hao, je ukiwa Rais wetu utaliweka vipi hili?

Swali 2: kunawatanzania wana mashamba/viwanja wananyimwa mikopo mpaka uwe na nyumba, je utaliangalia hili ili watu wa aina hiyo wakopesheke?

Swali 3: elimu bure yetu imekuwa bure kweli, je utabadirisha/ kuboresha elimu bure kuwa elimu ya kujiari badala kutegemea ajira? La mwisho, chama tawala kimetugawa, kimepandikiza chuki, unatakiwa kuisifia CCM tu, ukisema tofauti na matakwa yao wewe unakuwa mchochezi, unatumika kibaraka wa mabeberu, siyo mzalendo na maneo ya aina hiyo, je utakomesha tabia hizo za uonevu? Asante
 
Ndg mhemishiwa, pole kwa kampeni.

Suala la ajira kwa vijana tunaomba ufafanuzi. Mtaani vyuma vimekaza.
 
Elimu yetu kwa Sasa iko katika matabaka makubwa Sana kwenye upande was ubora. Pesa ya mtu ndiyo huamua hatima ya ubora wa elimu atakayopata mtoto wake, utalishughulikia vipi Hilo?

Pili elimu ya sekondari kwa Sasa karibu Kila mwanafunzi anakwenda, hata wasiokuwa na uwezo kumudu masomo ya sekondari Kuna utaratibu kwa watoto Aina hiyo?
 
Mh Tundu A. Lissu,

Kama mgombea wa kiti cha uraisi wa JMT, umekuwa ukisikika kutoa kauli za kutisha pale kutakapokuwa uvunjwaji wa haki kwa uchaguzi kwa kusema ICC itawahusu.

Sasa, itakuwaje pale utakapo kuwa umeshindwa kura? Utajuaje kuwa umeshindwa kihalali kweli, maana umekuwa ukitahazarisha sana NEC isije imajaribu kupindisha ukweli?
 
Mhe. Lissu,

Kwanza pole sana kwa kazi ngumu ya kampeni unayoendelea kuifanya.

Nimesikiliza na kutizama kampeni zako zote nchi nzima kupitia Youtube, bila kukosa hata siku moja na nimefurahishwa sana na uwezo wako mkubwa wa kujenga hoja, kueleza sera na ilani ya chama chako kwa ufasaha sana. Naomba nikuulize swali moja tu:

Umeahidi kupitia Ilani ya Chama kufuta makato ya 15% ya bodi ya mikopo, na kua 3% -- tunashukuru sana. Lakini vipi kuhusu retention fees ya 6% kwa mwaka?

-- Deni langu lilikua 16m baada ya kumaliza chuo. Kutokana na kuchelewa kupata kazi, deni likakua hadi kufikia 29m na kilichokuza ni retention fees na ilikua inaendelea kuongezeka kwa kasi, ikabidi kukopa bank 21m kulipunguza.

OMBI:
Iwapi utafuta retention fees, tunaomba serikali yako irejeshe fedha ilizokata kwa wanufaika wa mikopo kupitia kanuni ya retention fees ya 6% maana wengi wetu wakati tunaomba mikopo, hii kanuni haikuwepo, ni haramu na imetutia umasikini.
 
Lissu brother
naomba kutambua fine za barabara kwa kiwango cha 30,000 kwa wiki na naomba kuwakilisha wamiliki wote wa magari hasa ya biashara na fine hii ya 30,000.

Hizi fine zinaweza zidi hata malipo kwa TRA BIMA SUMATRA kwa mwaka .

Naweza sema mwaka jana tu nimelipa fine zaidi ya 900,000 ....

Naomba kutambua mpango wako madhubuti kuhusi fine hizi.

Sent from my SM-A605FN using JamiiForums mobile app
 
Hongera kwa kampeni nzuri zenye kutufungua macho na kuyajua mengi mabovu katika awamu hii.

Swali langu ni kuhusu elimu

Je mtatumia mbinu gani kubadiri mfumo wa elimu ili uwe ni mfumo unaoendana na maisha ya sasa?

Mimi na famikia yangu tutakupigia kura wewe

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Muheshimiwa tundu lissu swali langu kwa unavyoona upendeleo wa wazi wa nec na polisi kuendelea chama tawala utafanya aje kwenye mazingira kama aya kulinda ushindi wako
 
1. Je analichukuliaje kuhusu bei na gharama za vifurushi vya mitandao ya simu kama vifurushi vya dakika na intaneti? Kwani mitandao simu zinabei kubwa na watanzania wengi ni masikini.

2. Amejiandaaje kukabiliana na ujuma za uchaguzi kutoka kwa chama tawala... maana wakati wa kampeni zinaoneka wazi hata kabla ya uchaguzi?
 
1. BwanaTundu Lissu,wewe ni Celebrated Lawyer hapa Tanzania, Mwanasheria Msomi,nguli uliyepata kuwa Rais wa Wanasheria Tanzania TLS, Kwa nini umeamua kumtumia Mwanasheria Mzungu Bwana Robert Amsterdam awe Mwanasheria wako?

2. Je, Wanasheria wa Tanzania ni mambumbumbu!?

Jibu swali Bwana Tundu Lissu.
 
Mheshimiwa Tundu Lissu, Watanzania ni wapenzi wa michezo hasa mpira wa miguu, lakini viwanja vya michezo vingi hasa vya mikoani ni vibovu na hasa baada ya Chama Cha Mapinduzi kujimilikisha viwanja vilivyokuwa vinamikikiwa na Manispaa na vilivyojengwa kwa nguvu za wananchi.

Je, huoni ni wakati muafaka viwanja hivyo vikarejeshwa na kumilikiwa na halmashauri ili viweze kuhudumiwa, kufanyiwa uwekezaji na mapato yake kukaguliwa na CAG?
 
Katika Ilani ya CHADEMA hakuna hata sehemu moja inayoeleza namna Serikali itakavyokusanya mapato kwa maana ya vyanzo vyake?

Je, Serikali ya CHADEMA itatoa wapi fedha ikizingatiwa Ilani imeeleza kufuta na kupunguza kodi nyingi sana?

Je, fedha za kuendesha Serikali zitatoka wapi ikizingatiwa kwasasa Serikali iliyoko madarakani ina struggle
 
Swali: Serikali yako itaiangalia vipi suala la direct income tax?

PAYE, Je itafuta chanzo kingine cha mapato ili kuiondoa kabisa?
 
Swali. 1. Anazungumziaje kuhusu uchimbaji wa gesi uliokuwa umeanza huko Mtwara na sasa umepotea na makampuni ya uchimbaji hayapo.

Swali. 2. Nini msimamo wako binafsi na serikali ya chadema juu mikataba yote ya uchimbaji wa madini? Vipi hasa huu Barrick na GoT?
 
Utakapokuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, utalishughulikia vipi suala la uraia pacha?
 
Mheshimiwa Tundu Lissu, Watanzania ni wapenzi wa michezo hasa mpira wa miguu, lakini viwanja vya michezo vingi hasa vya mikoani ni vibovu na hasa baada ya Chama Cha Mapinduzi kujimilikisha viwanja vilivyokuwa vinamilikiwa na Manispaa na vilivyojengwa kwa nguvu za wananchi.

Je, huoni ni wakati muafaka viwanja hivyo vikarejeshwa na kumilikiwa na halmashauri ili viweze kuhudumiwa, kufanyiwa uwekezaji na mapato yake kukaguliwa na CAG?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom