Uchaguzi 2020 EXCLUSIVE: Maswali kwa Mgombea Urais wa JMT, Tundu Lissu kutoka kwa Watanzania watumiao mitandao ya kijamii

Status
Not open for further replies.
Swali: Je, unaamini kwamba Tume ya Uchaguzi ni huru? Kama sio huru, kwanini unaingia kwenye Uchaguzi ikiwa huna imani na Taasisi iliyopewa mamlaka hayo kikatiba?
 
Ahsante kwa fursa hii. Swali langu ni hili:

Naomba uelezee namna utakavyoweza kuboresha mfumo wetu wa Elimu nchini ambapo kila mwanafunzi anapomaliza ngazi yeyote ya elimu, awe na uwezo na ujuzi wa kuweza kujitegemea.

Kuliko mfumo wa Sasa unao malizia muda mwingi wa wanafunzi madarasani. Lakini akirudi mtaani hajui nini afanye kutatua changamoto zake.
 
Mh. Tundu Lissu

1. Watanzania walio wengi tunaamini huu uchaguzi sio wa huru na haki. Je utatushawishi vipi tukupe Kura kama tulivyo wapa wakina mh. Lowassa 2015 na mh.Dr Slaa 2010 na hawakutangazwa kama wameshinda.

2. Ukishinda urais je utaendeleza hii miradi mikubwa ya mh.John.

3. Utafanya nini kuhusu muungano wa Tanganyika na Zanzibar pindi ukiwa Rais.

4. Mikakati ipi utaiweka kwenye elimu ili kuondoa sintofahamu kwenye mfumo huu WA elimu Tanzania.

5. Utafanyanini kwenye idara ya uhamiaji ili kuondoa usumbufu kwa wahitaji.
 
Nauliza:-

Mwaka 2015 mlikuwa na kituo kimoja cha kupokea matokeo - bahati mbaya siku kadhaa kabla ya uchaguzi inasemekana vifaa vyenu viliibiwa, sasa:-

(i). Mwaka 2020 mmeandaa vituo vingapi kwa malengo hayo na viko wapi?

(ii). Kisheria tume ya uchaguzi ndiyo yenye jukumu la kupokea na kutangaza matokeo - sasa iwapo takwimu mlizopokea zikitofautiana na zile za tume mtafanya nini?

(iii). Ukiachilia mbali takwimu za kiitikadi watafiti wenu wanaonesha generally unakubalika kwa asilimia ngapi?

Msakila M Kabende
Mwanaccm kindakindaki
Kigoma - Tanzania
 
Mhe, Lissu mimi kabla sijafika kuuliza swali naomba kujua kama kuna mkakati wowote wakufanya kikao cha wagombea wote wa Ubunge na udiwani pamoja na mawakala ili kupeana mikakati.

Nasema hivi sababu ulipokuwa na kikao kule Kibaha usiku mambo uliyowaambia wanachama wako yalionekana kama mageni kwao
 
Mheshimiwa mimi ni technician Kuna vitu nimevigundua na serikalini Kuna kitengo cha kutusaidia sisi vijana lakin Kuna mizengwe husaidiwi hasa wakigundia wewe si mwana ccm, je utatusaidiaje sisi vijana?
 
Nina imani Tundu Lissu atashinda uchaguzi mkuu mwaka huu. Je amejiandaaje kibudget/ kifedha kuendesha nchi kwa siku 100 za mwanzo ambazo anatambua akiingia ikulu atakuta hazina haina kitu zaidi ya madeni likuki.
 
Mheshimiwa Lissu, kwa sasa tunaona kwa uwazi kabisa Ma-RC, ma-DC, mahakama, Bunge, Polisi na hata taasisi za kidini zikiwa kama Jumuiya za Chama kilichopo madarakani.

Serikali ya Chadema itakayoingia madarakani, itafanya nini katika kuhakikisha kuwa taasisi hizo hazitumikii siasa na hazitumiki kisiasa kwa maslahi ya Chama kilichopo madarakani?
 
Ndugu, mgombea, swali langu no kuhusu Sheria mpya za hivi karibuni, nyingine zimeanzishwa kwa miswaada ya hati za dharura, mfano ili ya takwimu, Sheria ya vyombo vya habari,ile ya mitandai na nyinginezo zenye lengo la kuzuia Uhuru na kulinda maslahi ya kundi la wachache,serekali utakayoiunda itarekebisha vipi mapungufu yaliyopo.?
 
Mheshimiwa Lissu nini msimamo wako kuhusu mpango wa sasa wa serikali kutaka kuanza kuzichaji pesa taasisi binafsi (kama benki na mitandao ya simu za mikononi) kila watakapotumia taarifa za vitambulisho vya taifa(NIDA) wakati wa kutoa huduma kwa wateja wao.

Note:
Vitambulisho vya taifa ni haki ya kila mtanzania, vililenga kumwezesha kila mtanzania kutambulika rasmi, vimegharamiwa kwa kodi za watanzania, na kitendo cha serikali kupanga kuanza kuwachaji pesa watoa huduma (kama mabenki, makampuni ya simu) kutapelekea taasisi husika kufidia hizo gharama kwa kuwachaji wateja wao, jambo ambalo litapunguza ufanisi wa matumizi ya vitambulisho hivyo na kurudisha mzigo kwa mlipa kodi.
 
Mimi ushauri wangu kwa mheshimiwa Lissu ni kwamba hata hasiposhinda kiti cha urais kutokana na sababu mbalimbali hasa hii ya uminyaji wa demokrasia, aanzishe movements kwenye umoja wa mataifa na jumuia za Ulaya kianzishwe chombo cha kijeshi Afrika ambacho kitakuwa kinachukua hatua za papo kwa papo kwa kiongozi na serikali wa taifa lolote Afrika anayevunja haki za binadamu, utumiaji mbaya wa madaraka uminyaji wa demokrasia n.k.

Tumeshuhudia sana madhira yanayowatokea wagombea wa vya upinzani nchi nyingi za kiafrika lakini jumuia za kimataifa zinaishia kutoa matamko tu ya kulaani bila kuchukua hatua na hivyo raia kuendelea kuteseka,kufa na kukumbana na maafa mengi. Uhuru wa watu kuchagua umekuwa ukirudi nyuma badala ya kusonga mbele baada ya viongozi waliopo madarakani kujiona hawawezi kufanywa lolote.
 
Pole sana mheshimiwa,

Serikali ya awamu iliopita ulijitahidi sana kufufua Michezo na Wanamichezo na mtunda yake yakaonekana baadae kama timu yetu ya Taifa kushiriki mashindano makubwa. Watanzania wenzetu kuonekana katika ligi kubwa kubwa duniani. Kupata tena mabingwa wa Dunia katika ndondi.

Kwa muda wa miaka mitano hii serikali imefunika na kubeza Michezo kabisa mpaka tunafungwa na nchi kama Burundi....

Sasa,
1) Je, Serikali utakaeiunda inazungumzia nini michezo in term of an employment than entertainments?

2) Kweli Jakaya alijitahidi kwenye michezo Sana lakini hakutilia maanani michezo kama Riadha ambayo watanzania tuna history nzuri tu.. Je, unasemaje kuhusu Riadha?

3) Katika miaka mitano hii tunaona uongozi wa taasisi mbali mBali za kimichezo zipo kisiasa kwa ajili ya chama tawala kuliko uzalendo.. Je utakomesha vipi?

Tupe mikakati
 
Mh. Tundu Lissu Kwanini umechagua kugombea urais wa Tanzania kipi kilikusukuma kugombea nafasi hiyo?

Kwanini kila hotuba zako unamtaja Rais Magufuli kwa ubaya na kashfa ?.

Kipi utatufanyia sisi watanzania tukikuchagua ambacho kwasasa akijafanyika ?

Kwanini ukuwasamehe waliokutendea mabaya pindi uliporejea Tanzania ,Kama alivyofanya Nelson Mandela alipowasamehe makaburu walipomfunga miaka 27.

ASANTE.
 
Mheshimiwa Lissu, nakupongeza sana kwa ushindi wako wa kishindo, tunakuomba ukumbuke kutekeleza serq zako, Mungu akusaidie.

Naomba siku ya kuapishwa kwako uwaalike wasanii wa bongo fleva waimbe zile nyimbo zao wanazoimba sasa au ikishindikana utumie ule wimbo wa Zuchu kama background kwa sherehe nzima na ikiwezekana umuagize Dj aucheze kabisa kumpa hasira kali ndugu stone, maana lazima awepo kushuhudia unavyoapa.
 
MH LISSU NAOMBA KUULIZA KAMA IFUATAVYO:

Kuna umuhimu gani wa kuwasilisha malalamiko yetu kwa nchi za nje wakati wenyewe tunao uwezo wa kuyamaliza? Huo siyo kuifanya nchi yetu idharauliwe hasa kwakuwa inamchango mkubwa katika ukombozi wa nchi nyingine?
 
Lissu unajinasibu kuwa wewe ni mpinga rushwa, swali ilikuweje wewe na team yako mwaka 2015 mkamkaribisha fisadi papa tuliyeaminishwa kwa miaka zaidi ya minane bwana lowassa kugombea kiti cha urais kupitia chadema bila ata chembe ya aibu?
 
Nawashukuru Jamiiforum.com kwa kutoa furusa hii ya kuuliza maswali. Nina imani mlengwa atayatendea haki maswali yetu kwa kuyajibu kwa ufasaha na kwa staha.

Maswali yangu ni haya kwa kuanzia.
1. Miaka kadhaa iliyopitia, Mtanzania mwenzetu ndugu Lissu, ukiwa bado mbunge ulinukuliwa ukiitakia mabaya Tanzania na watanzania wote hasa wale wenye uwezo mdogo kiuchumi. Ndugu Lissu ulinukuliwa ukisema kuwaunaitaka dunia/ ulimwengu iifungie/ iwekee vikwazo vya kiuchumi, kidiplomasia, kisiasa, kijamii na mengine kama hayo, yaani dunia itemee mate Tanzania. Kwa uhalisia vikwazo hivi vilipotumika kwenye nchi nyingine mfano Zimbabwe, Iran, hata Venezuela uathiri wananchi wenye vipato vya chini na kati, ambao kwa hapa Tanzania ndio walio walio wengi.

Je, Katika mazingira kama haya Watanzania hawa, sisi, tulio wengi tutapa sababu gani za kukuamini kuwa unaweza kuwa kiongozi wa nchi yetu na kujali maslahi ya nchi hii na watu wake wakati kwa vikwazo ulivyotuombea sisi vitupate vina lenga kukuimarisha wewe binafsi mbele ya wale ambao hawatutakii mema sisi watanzania na nchi yetu kwa ujumla wake!?

2. Siku kadhaa zilizopita ukiwa Mkoani Kilimanjaro, ulinukuliwa kupitia vyombo vya habari ikiwemo televisheni ya ITV ukisema kuwa utarudisha madaraka kwa wananchi kama ilivyokuwa wakati wa Ukoloni. Tulio wengi tunajua wakati wa ukoloni watanzani/wananchi walifanywa manamba na wengine kuuzwa nje kama watumwa.

Je, Kwa kauli hii sisi watanzania tutaachaje kuamini kuwa kipindi tu Ndugu Yetu Lissu utakapopata madaraka ya nchi hii utatuuza watanzania kwa mafungu kama bidhaa sawa na kipindi cha Ukoloni na hivyo ni halali tukunyime kura!?

3. Vyombo kadhaa vya kimataifa na baadhi vya humu nchini vimeandika habari kuwa unasimamiwa na mwansheria wa kimataifa ambaye si mtanzania. Pia wakati wamchakato wako wakupat nafasi ya kugombea inasemwa ulishawishi wajumbe wa mkutano kuvuruga wimbo wa Taifa kwa kuongeza maneno ambayo hayapo. Je, Kwa mambo yote mawili yaliyotajwa sisi watanzania tunakosaje haki ya kukunyima kura kwa kuonyesha unatudharau watanzania na pia unadharau mambo yanayotambulisha utanzania wetu!?

Karibu kwa majibu.
 
Msheshimiwa!

Nataka kujua mambo gani yaliyokusukuma kutoa kauli ambazo zilikuwa zinawatetea Barrick Gold Company pindi serikali ilipokuwa inafanya mchakato wa kutaka kulipwa fidia na kampeni kutokana na kusafirisha makinikia nje ya nchi ambayo yalikuwa na madini ndani yake.

Ambapo Tanzania imefanikiwa kulipwa fidia kuhusiana na suala hilo.
 
Swali langu kwako Mh. Tundu Lissu. Je, mmejipangaje kuhakikisha kila kituo kinakuwa na wakala wa CHADEMA ili kusiwe na udanganyifu kwenye vituo vya kura, maana tumeanza kuona baadhi ya matukio yanayoonesha kuwa baadhi ya mawakala wanaweza kushindwa kuingia kwenye vituo.
 
Status
Not open for further replies.
124 Reactions
Reply
Back
Top Bottom