Uchaguzi 2020 EXCLUSIVE: Maswali kwa Mgombea Urais wa JMT, Tundu Lissu kutoka kwa Watanzania watumiao mitandao ya kijamii

Status
Not open for further replies.
Mheshimiwa Tundu Lissu maswali yangu ni haya:

1. Umekua ukitoa ahadi nyingi sana majukwaami ambayo inaonesha zitahitaji kutumia pesa nyingi sana mfano kupandisha mishahara, kulipa fidia kwa waliobomolewa maeneo mbalimbali nchini na hata kulipa walioondolewa kwa vyeti feki. Na wakati huo huo ukisema utapunguza kodi hadi kubaki kodi moja tu kwa mwananchi. Je, umejipangaje kuyafanikisha hayo na pesa una mpango zitoke sehemu gani?

2. Vijana wengi tuko mtaani bila ajira. Je, umejipanga kuweka vipaumbele katika sekta ipi na utaanza na sekta ipi katika kuajiri, au tutegemee vijana wote tusio na ajira kupatiwa ajira?
 
Kwa kauli yako Mh, naomba ugusie Sera yako kwenye zao la Tumbaku ambalo limeharibiwa soko lake kwa miaka hii mitano.

Pili, naomba uelekeo wako kwa diplomasia yetu ya kiuchumi na kijeshi ukanda wetu wa Afrika Mashariki, Kati na Duniani

Tatu, Sera yako ya Uchumi imeelekeza zaidi kwenye kuiachia sekta binafsi kuwa mzalishaji huku Serikali ikijihusisha kidogo. Ni nguvu kiasi gani utaelekeza kwenye uzalishaji wa public goods?

Nne, naomba uelekeo wako katika sera ya maendeleo ya sayansi na teknolojia ili kuendana na maendeleo ya dunia

Tano, naomba uelekeo wako kuhusu nishati kama nyenzo muhimu ya uzalishaji.

Sita, nchi za wenzetu wana muda mwingi zaidi wa kufanya kazi (uchina na Korea Kusini), una mpango gani kwenye hili ili nasi tuongeze muda wa kazi?

Angalau maeneo haya yanatosha kwa sasa
 
Mh Tundu Lissu, sikuwa na mpango wa kukupigia kura lakini kwa manyanyaso upinzani mnayoyapata, nitakupigia kura.

Hata hivyo naomba unijibu yafuatayo:-

1. Nini msimamo wako wa kuhamishia Serikali Dodoma?

2. Nini msimamo wako kwa miradi ya serikali inayoendelea kama:-

A) SGR kuifikisha Kigoma, Mwanza na Rusumo
B) Mradi wa umeme (Nyerere hydro power)
C) Daraja la Busisi-Kigongo Ferry
D) KM 180 kuiunganisha kigoma na lami?

Aksante
 
1. Takribani 80% ya Watanzania ni Wakulima. Je, utawasaidiaje kunufaika na jasho leo? Mfano:- Wakulima wa korosho msimu 2018/2019 hawajlipwa pesa zao, wakulima wa ufuta msimu 2020 hawajalipwa pesa zao (Mtwara na Lindi) na TMX ingawa wafanyabiashara walishalipa pesa tangu zamani?

2. Ajira kwa Vijana ni tatizo sugu kwa sasa tangu 2016-2020. Je, utalitatua vipi tatizo hili?

3. Fao la kujitoa ni mwiba kwa watumishi. Je, utalishughulikiaje ili watumishi wachukue pesa zao muda wowote?
 
Asanteni sana uongozi kwa kutupa nafasi hii adhimu. Nina maswali kadhaa

1. Ni sekta gani za kiuchumi ambazo zitakuwa kipaumbele kwako ambazo kwa hizo ukuaji wake utachochea ukuaji wa uchumi, utachochea mzunguko wa fedha na kusaidia ukuaji wa ajira?

2. Sekta binafsi ni sekta muhimu sana kwa uchumi na hutajwa kuwa injini ya uchumi wa nchi yoyote, sekta hii kwa muda hapa nchini imekuwa ikifanya kazi chini ya kiwango, je pindi utakapoingia madarakani wewe na serikali yako mna mikakati gani wa kuiboresha sekta hii ili isaidie ukuaji wa uchumi na kuongeza idadi ya ajira?

Kwa sasa nianze na hayo asante
 
Pole sana na kazi nzuri ya ukombozi tuliyokutuma watanzania.

Maswali yangu ni kama ifuatavyo:-

1. Ni hatua gani serikali ya CHADEMA itachukua dhidi ya wahusika wa manunuzi ya ndege na uwanja wa ndege. Je, Katiba iliyopo haiwezi kuwa kikwazo cha kumwajibisha mshukiwa namba moja?

2. Hatua gani zitachukuliwa kwa wahusika wa mauaji yaliyotokea awamu hii ikiwemo Ben Saanane, Mawazo, Azori nk.
 
1. Je, Ukiingia madarakani utabatilisha sheria Inayozuia Rais kutokushitakiwa kwa makosa aliyoyatenda akiwa madarakani au utaiacha iendelee?

2. Je, Tanzania Corona ipo au Haipo, Kama ipo kwanini hufuati ushauri wa wataalam? Kama haipo kwanini usiutangazie ulimwengu ujue Tanzania hakuna Corona?

3. Msimamo wako kuhusu swala la mapenzi ya jinsia moja ukoje? Na ukìingia Madarakani Serikali itabaki Dodoma au Dar-es-Salaam?

4. Mambo gani makubwa matatu (3) unayompongeza Rais Magufuli aliyoyafanya kwa muda wa miaka 5 aliyokaa Madarakani?
 
Safi sana, nina maswali mawili kwake:

- Je, endapo atashinda na kuukwaa urais atashughulika vipi na mikataba ya kinyonyaji ambayo imekuwa mwiba kwa taifa letu mpaka kufikia kuzua mijadala mbalimbali nchini?

- La pili je, ni jitihada zipi atazifanya kuhakikisha anapanua wigo kwa sisi vijana ili tuweze kutatua changamoto zetu za kiuchumi?

La nyongeza: Ana kipi cha kutuhakikishia vijana haswa wanaotegemea teknolojia ktk kuingiza kipato halali? Je, atatumia misingi ipi kuendeleza hilo ikiwa ni pamoja kuwapa Uhuru zaidi ili waweze kuingiza kipato na kujitegemea. Akiwa kama kiongozi atafanya nini juu ya hilo?
 
Naomba utufafanulie suala hili, baada ya kumiminiwa risasi miaka zaidi ya 3 hivi sasa na kukimbizwa kwenda kutibiwa nje ya nchi, Polisi walijitokeza na kutueleza wananchi kuwa ushahidi wa suala hilo, umekwama kwa kuwa wewe na dereva wako hampo nchini.

Swali langu, je baada ya kurejea nchini, tunaomba utufafanulie kama Polisi weshakuja kwako na kuchukua maelezo ya ushahidi wako kama walivyoahidi, ili kukamilisha upelelezi wao?
 
Umekuwa ukipinga ujenzi wa miundombinu mfano barabara/madaraja/vivuko, ukisema wazi hayo sio maendeleo ya watu, na leo ulipokuwa Ukerewe umesema utajenga daraja. Je, unakula matapishi yako kwa kupinga na kuahidi jambo hilohilo?
 
Kwanza, hongera kwa kampeni zako ambazo kweli zinamwitikio mkubwa kuliko mgombea yeyote.

Pili, pole ni mbinu chafu zinazofanywa na dola kukukwamisha katika kampeni zako, lakini hata hivyo naamini ukisimama kupiga kampeni leo, bado utapata kura za tufani kwa kuwa watanzania wameikataa CCM kwa nguvu kwa mateso ya kila aina tupitiayo.

Maswali yangu kwako ni haya:-

1. Je, kama utakuwa umeshinda, alafu usitangazwe, utachukua hatua gani? Je, hutatuacha solemba kama Lowassa aliyeshindwa kutetea haki yetu ya kupigania ushindi?

2. Tume ya Uchaguzi imekataza Mawakala kuingia na simu vituoni. Je, hii haitaathiri ushahidi wa matokeo?

3. Tumesikia fununu kuwa timu ileile ya Masaki iliyochakachua matokeo 2015 kabla ya kuwasilishwa Tume kwamba ipo Dodoma. Je, kama chama mmefuatilia hili?

Nakutakia kila la heri, tuko nyuma yako.
 
Mh. TL,

Vipi kuhusu Muhimili wa mahakama katika kesi zinazowahusu masheikh wa UAMSHO,

Je, namna gani utalishughulikia hilo suala la viongozi wa UAMSHO wanaoozea Jela pasipo kesi zao kusikilizwa?
 
Ahsanteni sana JamiiForums kwa fursa hii. Maswali yangu ni:

1. Kuhusiana na sera ya majimbo: naomba ufafanuzi kutoka kwako TL juu ya namna hii sera ya majimbo itakavyokua structured na itakavyofanya kazi iwapo CHADEMA itashinda. Je, mgawanyo wa mapato utakuwaje kati ya jimbo na jimbo (ukizingatia kwamba haya majimbo yatakua na utofauti wa uwezo wa kuzalisha). Je, movement ya watu katika ajira itakuaje kati ya haya majimbo? Kutakua na restrictions za ajira au fursa za masomo kati ya majimbo? Uhusiano kati ya majimbo na serikali kuu utakuaje? Je, sera hii haitaleta utengano katika taifa letu?

2. Umesikika ukisema kwamba utaruhusu wananchi wachunge hadi kwenye hifadhi za taifa. Ningependa kupata ufafanuzi kuhusu hili.

3. Serikali yako iwapo itapewa ridhaa, itachukua approach gani kuhusiana na Muungano kati ya Tanzania bara na Zanzibar? Je, itauvunja muungano huu?

4. Chama cha CHADEMA kimejipanga vipi ili kisiibiwe kura au kuhujumiwa katika mazingira ya uchaguzi huu? Chama kimejipangaje kuwa na mawakala nchi nzima (chama kina uwezo huo?), Chama kimejipangaje ili hao mawakala wasinunuliwe? Chama kimejipangaje kwa janja janja za wizi wa kura?

Ni hayo tu. Ahsante.
 
Mh Tundu Lissu, kuelekea katika kupiga kura hivi karibuni mna wahakikishia vipi Wananchi wa Tanzania juu ya Kura zao kuwa na maana na sio kupoteza wakati?

Nimeuliza hivi kwa sababu ya rafu ninazoona zinaendelea dhidi ya Upinzani.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom