Uchaguzi 2020 EXCLUSIVE: Maswali kwa Mgombea Urais wa JMT, Tundu Lissu kutoka kwa Watanzania watumiao mitandao ya kijamii

Status
Not open for further replies.

JamiiForums

Official JF Response
Nov 9, 2006
6,099
2,000
Salaam,

Ndg. Tundu Lissu ni mwanachama wa JamiiForums tangu 2010 akitumia jina halisi.

Kwa sasa, Lissu ni mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA; hivyo akiwa kama mwanachama mkongwe wa JamiiForums na mtumiaji mkubwa mitandao mingine ya kijamii, ameamua kutenga muda wa saa 2 kujibu maswali mbalimbali ya wadau kupitia hapa jukwaani.

Mada hii ni maalum kwa ajili ya kuweka maswali ambayo atayajibu kesho tarehe 15 Oktoba, 2020 kuanzia saa 2 hadi 4 asubuhi. Ameahidi pia kupokea ushauri wa wadau.

Tunakaribisha maswali yenye kulenga kujenga Tanzania yetu bila kumkashifu wala kumvunjia heshima yeyote (be objective). Maswali yanaweza kujikita katika nafasi yake kama mgombea urais au safari yake ya kisiasa kwa ujumla.

NOTE: Wagombea Urais wengine pia wako huru kutumia jukwaa hili kuufikia umma wa Watanzania na jitihada zinafanywa ili wafikiwe wote ikiwezekana.

ILANI: Maswali yamekusanywa ya kutosha, mgombea ametumiwa maswali hayo na atayajibu kadiri muda utakavyoruhusu.

Mjadala huu umefungwa
 

MWANAWAVITTO

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
246
250
Mheshimiwa,

(a) Je, Serikali yako ipo tayari kuanzisha uchunguzi wa vifo tatanishi, utekwaji nyara na kupotea kwa watu mfano wa Ben Saanane, Azory Gwanda na wengineo?

(b) Je, serikali yako ipo tayari kuwachukulia hatua watendaji wote wanaohusika na kuwabambikia watu kesi?
 

inchaji

JF-Expert Member
Jul 5, 2019
1,494
2,000
Swali: Pay As You Earn (PAYE), mimi kama mtumishi wa sekta binafsi naiona kama ni kubwa mno na Serikali ya CCM inaona lakini haijali wala kufanya chochote.

Tarehe 28 Oktoba nitampigia kura.

Je, akiingia madarakani atapunguza kidogo asilimia za PAYE ili kutupunguzia mzigo sisi wafanyakazi wa Jamhuri?
 

Papaa_Mobimba

JF-Expert Member
Mar 3, 2019
212
500
Mheshimiwa Lissu utafanyaje Mawakala wako nchi nzima wasipoingia vituoni? Masanduku ya kura yakitolewa vituoni kiholela na nakala za matokeo kukosekana?

Je, unafikiri Watanzania wana Utayari wa kuingia barabarani?

Baada ya mvurugano wa kimatokeo pamoja na kikatiba ? Je utakuwa tayari kukaa meza moja kumaliza tofauti zako za kiitikadi na kisiasa pamoja na Rais Magufuli?

Je, utakubali kuunda serikali ya Nusu mkate pamoja na Rais Magufuli,iwapo ikatokea kuwa serikali ya nusu mkate ndio muafaka wa kurudisha umoja wa kitaifa?
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,360
2,000
Mheshimiwa, mna mpango gani wa kuwakutanisha Wagombea Ubunge wote kwa pamoja kuwa na mkakati maamuzi pale mawakala wao watakapogundua kuwa kumekuwa na wizi au mchezo mchafu wa kura vituoni kwao?

Maana haya mambo ya kusubiri rufaa hayana matokeo chanya tumeona katika uenguaji wagombea.
 

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
10,108
2,000
Nataka kujua tumejipanga vipi kuzuia mawakala wetu kuuza kura zetu kwa CCM?

Maana Kuna hujuma kwenye uchaguzi huu na kete iliyobaki ni kuwanunua mawakala wa chadema.

Pia je chadema itaweka mawakala nchi nzima ili kuepusha wizi wa kura maeneo hasa ya vijijini?

Je wanachi tukipiga kura tubaki vituoni kuanzia asubuhi mpaka jioni ili kutoa presha kwa tume kutoa matokea halali kwa haraka?

Je simu na form za matokeo zikizuiwa na tume kupewa mawakala chama kinachukua hatua gani maana ndio njia ya kupata ushahidi wa matokeo mapema vituoni.
 

kikoozi

JF-Expert Member
Jun 24, 2015
1,173
2,000
Habari my mgombea urais, pole na kampeni.

Swali langu ni:
Je, mfumo uliopo wa kuomba ajira Serikalini (namaanisha kupitia Utumishi-Ajira Potal) utauondoa au utaendelea kuwepo hivi hivi, na kama utauondoa, mfumo utakaokuja nao utakuwa ni wa aina gani?
 

August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
6,429
2,000
Je USA raia wao waliulizwa kuhusu muungano wao au UK? Na kwanini hawafanyi hivyo?

Na zaidi ya hapo mbona hufikiri kuvunja nchi ya Tanganyika/ Tanzania Bara kwani miundo wetu ulifanywa na wakoloni, hatukuulizwa kama Kilimanjaro iwe Kenya au Tanganyika n.k n.k
 

respect wa boda

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
4,537
2,000
Swali langu ni kuhusu Biashara:

Wafanyabiashara wanalipishwa faini kubwa zisizoendana na uhalisia ktk biashara. Mfano, mteja anaweza kununua kiatu cha shilingi 15000 dukani, muuzaji akisahau kumpa risit mnunuzi anatakiwa kulipa faini ya kiasi kisichopungua sh 3,000,000.

Ukiwa Rais, uko tayari kuifanyia marekebisho Sheria hii ya kinyonyaji na isiyolipika kwa Wafanyabiashara?

BACK TANGANYIKA
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom