Uchaguzi 2020 EXCLUSIVE: Maswali kwa Mgombea Urais wa JMT, Tundu Lissu kutoka kwa Watanzania watumiao mitandao ya kijamii

Status
Not open for further replies.
Pole na majukumu muheshimiwa mgombea urais.

Swali:
Nini msimamo wako au serikali yako iwapo utashinda kuhusu mapenzi ya jinsia moja?
 
Mheshimiwa;

Ajira ni moja kati ya swala nyeti katika Uchaguzi huu. Je, ni eneo gani kati ya haya ambayo utashughulikia ili kuhamasisha uzalishaji wa ajira? Utafanya nini katika kila eneo?
  1. Je, ni Kilimo
  2. Je, Viwanda
  3. Je, ni Huduma
  4. Je, ni teknolojia
Je, unafikiri tatizo la ajira ni la kidunia au pia kuna masuala ya ndani ya nchi ambayo yanachangia?
 
Asante sana kwa kutoa fursa hii Jamii Forums - Siasa.

Mimi ninafarijika sana na dhanira ya serikali ya CHADEMA ya kurejesha mchakato wa KATIBA MPYA. Kwa sababu matatizo mengi tunayokabiliana nayo kama taifa ama jamii - hususan ambayo yamejidhihirisha waziwazi katika miaka hii mitano iliyopita - ni ya kimfumo (structural). Kupatikana kwa Katiba Mpya sio tu itakuwa ni sisi kujitendea haki, bali pia tutakuwa tunawatendea haki watoto wetu, wajukuu wetu, na vitukuu wetu!

SWALI 1: Mojawapo ya UFISADI (kleptocracy) mkubwa ulioratibiwa na serikali za CCM ni malipo ya kufuru kwa wabunge. Ndio maana haishangazi viongozi wastaafu wanafanya kila liwezekanalo kuwapenyeza wake na watoto wao Bungeni. Je, serikali ya CHADEMA itakuwa tayari kufutilia mbali UFISADI wa aina hii? Je, unaweza kulidokeza tatizo hili katika kampeni zako za sasa?

SWALI 2: Wapinzani/washindani wako wameanza kupiga propoganda za kupotosha dhana ya 'maendeleo ya watu'. Je, unaweza kujitahidi kuifafanua kwa kutumia mifano kuntu kama ulivyofanya leo (10/14) katika mkutano wako wa Ukerewe kwamba tunaposema maendeleo ya watu haina maana hatupangi maendeleo ya vitu. Tunapanga maendeleoa ya watu kwa vipaumbele. Badala ya kujenfa daraja la Salender au uwanja wa ndege kijijini kwa Rais Lissu, tunajenga daraja la Kisorya au tunaboresha miundombinu ya Jangwani ili kukabiliana na tatizo la mafuriko linalojitokeza kila msimu wa mvua tokea tupate uhuru!

SWALI 3: Mimi ni m-diaspora. Je, serikali ya CHADEMA ina mpango gani kulinda haki za kuzaliwa, za kibinadamu na za kikatiba za waDiaspora?

SWALI 4: M-diaspora akitaka kuchangia mafuta na maji kufanikisha kampeni zako, atume wapi mchango huo?
 
Maswali:

Kwanini unahimiza sana kuwa ukishindwa kwenye huu uchaguzi kwamba utaingiza watu barabarani? Je, unataka tuamini kwamba ili Taifa hili liwe na amani ni lazima ushinde wewe? Na kama ndivyo, kwanini tusiamini kuwa wewe ni kibaraka wa Mataifa ya Ulaya?

Ningependa kujua pia, yule dereva wako yuko wapi? Ili tusiamini kuwa umemficha kwa lengo kukwamisha uchunguzi, kwa lengo la kupata kiki na kura za huruma katika Uchaguzi huu.
 
Kuna wakandarasi wengi wamefilisika kutokana na serikali kutolipa madeni inayodaiwa kwa muda mrefu sana. Je, tutawezaje kupata hela ya kuwalipa ikiwa ni pamoja na riba wanayodai?
 
Mh. Tundu Lissu ninaushauri kwako na serikali yako ikiwa mtapata ridhaa yakutawala: moja ya changamoto kubwa nchini Tanzania tangia uhuru ni tatzo la maji hasa vijijini ambalo linaweza kumalizika kama ifuatavyo;

Tunaweza kushawishi vijana kila kijiji linapoishia bomba la mwisho la maji kuchimba mtaro kwaajili ya kijiji chao baada ya kufika kijiji hicho vijana wa kijiji kinachofuata nao wanachimba kuingiza kijijini mwao hivyo hvyo hadi tunapeleka maji nchi nzma.

Mh. Rais hivi km nchi yetu kila sekunde tunapoteza maji mengi mnno yanayopote baharini kupitia mito mbalimbali inakuaje tunashindwa kusupply maji tu nchi nzima miaka 50+ tangia uhuru hii ni dalili ya low IQ nakutojali wananchi wetu. Mungu akutangulie.
 
Habari Mh. Naomba kuuliza, endapo usiposhindwa uchaguzi huu kihalali kabisa. Je, utakuwa tayari kukubali matokeo na kusaini fomu ya kukubali matokeo?
 
Asante sana mh. Kwa nafasi hii ya pekee, swali langu moja kwa moja ni kuhusu watu wanaokatwa kipindi cha uchaguzi huu kama ukipita na kuwa Raisi Wa jamuhuri ya muungano Wa Tanzania unatuahidi kipi juu ya hatima yao kwasababuahawana makosa zaidi wamebambikiwa tu. Asante sana kila lakheri tupo pamoja ##Lissu 2020--2025
 
Mheshimiwa Lissu,

Pole na harakati za kampeni.

Je ukishinda uraisi, hii miradi iliyoanzishwa na Magufuli ambayo haijakamilika kama SGR je utaendelea nayo kuimalizia au utasitisha zote?
 
Mh Lissu,

Nataka pamoja na mambo mengi ndani ya siku 100 baada ya kuapishwa..Naomba ufafanue namna utakavyo create ajira kwa maelfu ya vijana wa mijini na vijijini kupitia Kilimo, Ufugaji na Uvuvi.

Naamini, hii ndiyo sekta pekee nchini ambayo bado bikira...hii ndiyo muhimili ( backbone) mkubwa wa uchumi wa taifa letu.

Tunaomba maelezo ya kina utaanzaje na mikakati yako itakuwaje... wewe ni shahidi kwamba hawa vijana hawa wa miaka 16 - 25 wanaotuuzia soksi na mabakuli na pasi na jeans za mtumba hawa utawaingizaje kwenye mfumo wa uchumi wa nchi yao ili na wao wawe wadau hasa mwenye hii dhana yako ya maendeleo ya watu badala ya vitu.

Asante sana.
 
Mheshimiwa Tundu Lissu mimi nataka kujua

(1)Mpango wako wa kukabiliana gharama za elimu ya juu(baadhi ya vyuo vikuu vya udaktari ada inafika 6.7M) itafikia kipindi wanaoweza kusoma ni watoto wa matajiri tu na tuliosoma huko tumeziingiza familia kwenye umasikini kwani serikali ina vyuo viwili tu ambavyo havitoshi.

(2)Upi mpango wako kwa vijana wanaokwama kidato cha nne,huoni kuwa ukipata ridhaa uanzishe college za ufundi,biashara na kilimo zenye hadhi inayokubalika (zisizochukuliwa vibaya kaam VETA) vijana wetu wapite huko??

(3)Una mpango upi na vijana tusio na ajira utakapoingia madarakani,je utaweka fungu lolote la kuwakopesha vijana chini ya wizara ya vijana??
(4)Unatuondoa vipi wasiwasi kama tukikupa ridhaa hamtafanya ufisadi??
 
Mh Tundu Lissu mgombea urais, tunaomba useme kuhusu PAYE, kiwango Cha chini Cha mshahara kwa mtumishi wa umma, pamoja na pension na kiinua mgongo,zungumza wewe utafanya Nini juu ya hayo. Ukisha zungumza sisi tutakupa kura zetu na kubadilisha upepo wa siasa ndani ya week ili ushinde
 
Waheshimiwa wagombea

1.Swali langu liko katika swala la ajira
Je mna mkakati gani kulishughulikia swala la ajira kwa vijana?

Na mnaposema vijana wajiajiri je mna uhakika kua vijana wana mafunzo ya kutosha ya ujasiriamli? pamoja na mitaji?

2. Je mna mkakati gani kuipitia upya sera ya ulipaji deni la bodi ya mikopo kwa elimu ya juu?
Maana ni kandamizi kwelikweli
 
Mheshimiwa Tundu lissu je kuna siku unaweza kuunga juhudi ukahamia chama tawala?jibu likiwa hapana je siku ukiunga juhudi sisi wa tz tukufanyaje?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom