ZITTO,ZITTO,ZITO........NANI KAMA ZITTO(Wangapi wanaweza kukubali kujitokeza hapa kuhojiwa maswali ya aina yoyote kama zitto)
Thanx ASHDIII kwa jitihada zako,Lakini pia Zitto wewe ni kiongozi wa mfano na kuigwa kwa hili.
SWALI LANGU LA MSINGI KWAKO RAIS WANGU WA KU-MOYO
>KWENYE SAFARI YAKO YA KUGOMBEA URAIS MWAKA 2015 KAMA UTAPITISHWA NA CHAMA NI MGOMBEA GANI WA CCM AKISIMAMISHWA UNADHANI ANAWEZA KIDOGO AKAWA MSUMBUFU.otherwise,najivunia kuwa upande wako siku zote za Maisha yangu.
Mungu akupe afya njema,hata hili la kuhojiwa hapa ni ushindi wa heshima
Anaweza kujibu swali namba 6. Hayo mengine ni mwiba kwake.Mimi nina maswali kadhaa ambayo ningependa Mheshimiwa Zitto ayajibu kwa ufasaha.
[1] Mheshimiwa Zitto umekuwa mpiga debe mzuri wa kupendekeza umri wa kugombea urais ushushwe hadi miaka 35.Je mapendekezo haya ni kwaajili ya vijana wote Tanzania au umesukubwa na nia ya kutaka wewe binafsi kugombea urais kwakuwa mwaka 2015 bado utakuwa haujafikisha umri wa miaka 40.
[2] Mheshimiwa Zitto kampeni za mwaka 2010 ulisikika ukimsifia Rais Kikwete na kumtosa mgombea wa chama chako Dr W Slaa.Baada ya uchaguzi chama chako kilichukua uamuzi wa kususia hotuba ya rais ya ufunguzi wa bunge wewe ukakaidi na kuamua kutoingia bungeni na mwisho ulizungumza na wanahabari kupinga uamuzi wa chama chako kwania ya kuonysha mapenzi yako binafsi kwa rais Kikwete.Baada ya uchaguzi umekuwa ukiandamana na rais mara kwa mara katika ziara zake za nje South Sudan na Ethiopia.Swali kutokana mlolongo wa matukio yote bado unadhani unastahili kugombea urais kupitia CDM ?.
[3] Mheshimiwa Zitto uchaguzi wa mwaka 2010 gazeti la Mwanahalisi lilichapisha mawasiliano ya simu baina yako na naibu mkuu wa usalama wa taifa Jack Zoka.mpaka leo sijasikia ukikanusha,kwakuwa hakuana kanusho toka kwako unaweza kutueleza mazungumzo yenu yalihusu nini ?.
[4] Mheshimiwa Zitto msimamo wako na kauli zako kuhusu muungano wa EA umekuwa mara zote kutoangalia maslahi ya waTanzania.Mfano wewe unaunga mkono free movement of labour,unaunga mkono access ya ardhi kwa wananchi wa wote wa EA wakati unajua wazi wenzetu hawana ardhi ya kuwagawaiya watanzania.Naomba unieleze nini faida za msimamo wako.
[5] Ni kwanini uonekani kwenye mikutano ya M4C ?.
[6] Mheshimiwa Zitto Viongozi/CDM imekuwa mstari wa mbele kufichua ufisadi.Ninazo taarifa za uhakika kuna mwanachama wenu katafuna fedha za M4C ni kwanini mko kimya ?.
Maswali
1. Naomba utaje mali unazo milki
2. Ni kweli unamiliki HAMMER
3. kweli unataka kugombea urais
Swali linamhusu anayedhaniwa na Zitto kuwa mmoja wa maadui zake ndani ya chama.Mkuu Gagnija kwanini unadhani anaweza kujibu swali number sita tu ?.
Labda niulize kuwa unapo sema binafsi una maana gani? Kuna maswali binafsi... 'unapenda kula nini', 'siku gani huwezi sahau katika maisha yako?' 'unapenda maisha ya namna gani?' na the like...
Nimetoa hiyo tahadhari sababu watu hawachelewi kuleta maswali kama 'umewahi lala na wanawake wangapi?', 'girlfriend wako ni nani?' 'unafanya mapenzi mara ngapi kwa mwezi?' 'umewahi lala na AshaDii?'
Hivi umenipata maana yangu?
Naamini kabisa kuwa maisha ya Zitto binafsi ni open book, wengi wanamfahamu kwa mbali ama kwa kutokea anako tokea. Sasa kwa mtindo na maswali hayo sioni kuwa tukipata majibu yake kama lina faida yoyote kwa jamii.. Labda kama nakosea; but hivo ndio naamini.