EXCLUSIVE Interview with Zitto Zuberi Kabwe at Jamii Forums [Coming Soon]

EXCLUSIVE Interview with Zitto Zuberi Kabwe at Jamii Forums [Coming Soon]

Status
Not open for further replies.
1: Kwanini umependekeza mwaka wa mgombea wa uraisi uanzie miaka 35 na sio 20 au 30?.
2: ulisema sasa ni zamu ya vijana, je sisi wenye miaka 20, au ulijiangalia mwenyewe?.
3: watu wanaokujua tangu masomoni wanasema wewe ni mbinafsi, unajitetea vipi kuhusu suala hili?
 
Swali: 1. Katika mpango wako, lini utawasaidia majimbo ya uchaguzi yanayopakana na Kigoma kupambana nba CCM?
2. Kuna fununu kuwa wewe unatumwa na Mheshimiwa Rais kuvuruga CHADEMA na hii imeonekana katika maeneo mengi ikiwa ni pamoja na kuwa na mikutano naye ya faragha, kutangaza kugombea urais kabla ya muda wa kuchukua fomu n.k. wewe binafsi unasemaje kuhusu hili?
3. Kwa maoni yako, nani ataweza kuivusha CDM 2015 katika nafasi ya Urais wa Tanzania kama wewe usipogombea?
 
Da Ashadii maswali yangu kwa Zitto ni machache.
Mosi, iliwahi kuripotiwa na gazeti la Mwanahalisi kuwa Zitto alimpa rafiki yake Kafulila magari ya kupigia kampeni. Idadi ya magari tajwa ilikuwa kubwa kulinganisha na kipato cha Zitto. Je Zitto anaweza kutoa ufafanuzi juu ya hili maana alionekana bonge la mkwasi.
Pili Zitto kwanini haoi na kama kweli anataka kugombea urais tutampimaje rais mhuni ambaye usela wake unaweza kuhatarisha usalama wa taifa?
Tatu,kuna uvumi kuwa Zitto ametumia nafasi yake ya wenyekiti wa kamati ya Bunge kujingenezea utajiri. Je analisemeaje hili?
Tano na mwisho, Zitto aliwahi kusema kuwa asingegombea ubunge kwa muhula wa pili lakini baadaye akagombea. Je huu si ushahidi kuwa Zitto ni muongo wa kawaida anayeweza kusema hili kesho akafanya tofauti?
Naomba kuwasilisha.
 
Maswali bado bado yanapokelewa? (Naamini jibu ni ndio ili nasi ambao tulipitwa mwanzoni tupate fursa)
Maswali yangu ni
1. Je, Zitto anaiona CDM ina strengths zipi kwa sasa, ambazo anaamini zitaiwezesha kushinda uchaguzi wa 2015?
2. Je, Zitto anaiona CDM ina weakness zipi, ambazo zisipofanyiwa kazi, kushinda 2015 itakuwa ngumu?
3. Je, Zitto anatushauri tufanye nini sisi wanachama wa kawaida huku chini, katika kuhakikisha chama chetu kinaimarika zaidi na hata kushinda 2015?
4. Kuna watu wananiaminisha eti CDM kuna mpasuko na makundi, hasa baina ya viongozi wa juu. Zitto ana nini cha kuniambia huku vijijini niliko?
 
swali
1. kama katibu mkuu wa CDM, moja ya mpango wa kiutawala wa CDM ni Majimbo, Je anaweza elezea jinsi ambavyo uongozi wa kimajimbo utakavyo kuwa? yaani, resource distribution, administrations in judicial,legislative and province. faifa , changamoto n hasara zake
2. Je kwa nini uongozi wa CDM chini haupo imara? na lini watafika kila kata na serikali ya mtaa kwa nchi nzima? nini kikwazo?
3. kama sera ya majimbo ipo je kwanini uongozi wa CDM ki chama haupo ki majimbo? hawaoni ni dalili ya kutudanganya? kama chama hakipo hivyo hiyo serikali itaweza (5yrs)? kama unashinda term moja
4. Kwanini CDM haija ajiri watendaji wa mikoani, wilayani na ngazi za chini?
nitarudi kwa sehemu ya pili
Wakatabahu
 
AshaDii,

..nilikushauri usimuulize kuhusu nia yake ya kugombea Uraisi mwaka 2015. kwa mtizamo wangu hakuna jipya litakalopatikana kutoka ktk majibu yake.

..binafsi ningependa maswali yako yajikite ktk masuala yanayohusu CDM, sera zao, na utayari wao wa kushika madaraka ya nchi.

1. Zitto na Mbowe wamesikika kumsifia Raisi Kikwete kwa kutatua kero za wananchi. Kitendo hicho ni sawa na ku-endorse rekodi ya CCM na serikali yake. Je, ktk mazingira hayo CDM wana sababu gani za kuwashawishi wananchi wawatoe CCM madarakani na kuikabidhi nchi kwa CDM?

2. Elimu yetu imeporomoka kwa kiwango kikubwa sana. Wahitimu wa vyuo vyetu wanafanya vibaya wanaposhindanishwa na wahitimu wa nchi jirani. Je, anafikiri CCM imekosea wapi? Pia CDM ina mikakati gani ya muda mfupi na mrefu kutatua tatizo hilo ktk ngazi za elimu ya msingi, sekondari, vyuo vya ualimu, na vyuo vikuu, ikiwa itapewa madaraka? Je, mikakati hiyo inatekelezwa ktk jimbo lolote lile ambalo limeshikwa na wabunge wa CDM??

3.Tukiwa bado kwenye elimu; CDM walitoa ahadi kwamba elimu ya msingi na sekondari itakuwa bure. Je, CDM ikipewa madaraka utekelezaji wa ahadi hiyo utachukua muda gani? Pia serikali kuchukua mzigo wa kugharimia elimu ya msingi na sekondari 100% haoni kwamba utaikosesha serikali mapato ambayo yangetumika kuboresha viwango vya elimu??

4. Sera ya ubinafsishaji na soko huria imeshindwa kutatua tatizo la ajira kwa vijana. Je, CDM watarekebisha vipi tatizo hilo?

5.Uzalishaji ktk sekta za kilimo na ufugaji umeendelea kushuka nchini. Tunaomba atueleze sera na mkakati wa CDM kuinua kilimo nchini. Nini maoni yake kuhusu mpango wa CCM wa kilimo kwanza.

6.Sera ya mambo ya nje na mahusiano ya kimataifa ya CDM. Nini tofauti kati ya CCM na CDM ktk eneo hilo. Je, CDM ina msimamo gani kuhusu Tanzania kujiunga na OIC? CDM ina msimamo gani kuhusu ushiriki wetu ktk jumuiya za SADC na EAC? Je, ni nini hasara na faida za msimamo wa Tanzania kuhusu ARDHI ktk jumuiya ya EAC? Je, ni nini faida na hasara msimamo wa Tanzania kuhusu mkataba wa ulinzi wa EAC?

7.Uwekezaji wa serikali ktk miradi mikubwa. Nini faida na hasara za serikali kuwaachia wawekezaji jukumu la kujenga bandari, viwanja vya ndege, na miradi ya umeme? Ikiwa CDM watapewa madaraka serikali yao itawekeza ktk miradi ipi mikubwa?? Fedha za miradi hiyo zitatoka ktk vyanzo vipi??

8.Suala la michezo. Kwanini Tanzania tumeshindwa kufanya vizuri ktk mashindano ya kimataifa pamoja na kwamba mapesa mengi sana yametumika ktk vilabu vya mpira wa miguu?? Nini maoni yake kuhusu mtizamo kwamba Tanzania iachane na mpira wa miguu na badala yake ielekeze rasilimali na nguvu zake ktk riadha ambayo tuliwahi kuwa na rekodi nzuri??
 
Last edited by a moderator:
Anawezaje kuomba kupepelusha bendera ya cdm na huku alisha waaminisha waislam kuwa cdm ni chama cha wakristo? Na anachukiwa cdm kwa sababu ya dini yake? 2. Kwanini aanze mchakato wa kuutaka urais mapema kiasi hiki?
 
Swali kwa zitto. 1. Kuna mbunge kijana wa cdm jimbo la arumeru amewahi kutamka wazi kwamba kaskazini ijitenge iwe taifa huru, wewe kama kiongozi wa chama na mbunge kijana na mtanzania pia unalizungumziaje hili? 2.jimbo lako la kigoma kaskazini lina madiwani wengi wa ccm kuliko wa cdm, umeshindwa kuhamasisha halmashauri yako iwe chini ya cdm kama tunavoona moshi mjini,na maeneo mengine? 3.chadema kinanasibishwa na ukanisa na uchaga na pengine ukaskazini.nini maoni na msimamo wako katika hili
 
AshaDii,

maswali yangu nayaelekeza kwako, why zito and not me ? kwa nini umeomba ruksa kwa founder wa jf kwani unategemea kupata any financial token from this interview? hii interview ina tija gani kwako, kwa zitto na jf members ?
 
Last edited by a moderator:
mi ningependa kujua kama kuna ukweli wewe wa zitto kutumiwa na kambi ya lowasa kudhoofisha cdm kabla ya 2015. kwa kutanga nia ya kugombea urahisi ilikuleta mgawanyiko katika chamacha cdm na kuyoa mwanya kwa ccm na lowasa kuingia magogoni kirahisi. pili nigependa kujua zitto anauhusiano gani wa karibu na usalama wa taifa kama ni kweli jee yeye ni mtu wa usalama na anatumiwa na usalama kutekeleza anayoyafanya?
 
Narudi,
1. Kama CDM wanapata hatamu , Je mikataba gani ambayo itakuwa ya kwanza kushughulikiwa?, ikiwemo kuvunja, kujadiliwa na kubadilishwa?
2. Kitu gani ambacho hili litaifa linahitaji ili kuweza kufanya vizuri kiuchumi, kijamii na kisiasa?
3. kama katiba haitakuwa tayari 2014, uchaguzi wa serikali za mitaa CDM watashiriki kwa kataiba ya zamani?
4. Endapo umri wa kugombea uraisi hautabadilishwa na zitto akashindwa, je hato gombe ugunge tena? nini sababu, ana acha siasa?
5.kama atakuwa Waziri wa fedha wa JMT nini vipaumbele vya budget yake ndani ya miaka 5 ya kwanza.
6. Je cdm wana mfumo gani wa ubinafisishaji?
nitarudi
Wakatabahu
 
Zitto

what do you consider to be the number one issue affecting our country??

What will you do to address it??
 
Last edited by a moderator:
AshaDii,

..nilikushauri usimuulize kuhusu nia yake ya kugombea Uraisi mwaka 2015. kwa mtizamo wangu hakuna jipya litakalopatikana kutoka ktk majibu yake.

Mkuu Jokakuu nishukuru kwa list ya maswali yaliyo shiba... Na maeneo yote ambayo unaona ni msingi aulizwe pia tumeweka. Tumejitahidi saana kuyaandaa kwa ku cover maeneo yale ambayo wengi wana kiu nayo; hivo usitie shaka mkuu.

Nimekupata kuhusu sababu yako ya kuto kumuuliza mambo ya Uraisi 2015, ila unakuta kuna vitu ambavyo haviwezi kuulizwa bila kupelekea majibu kuenda huko, for instance his stance katika kupunguzwa kwa umri wa urais, uamuzi wake wa kutogombea ubunge 2015, na the like. But like I said nimekupaa mkuu na nashukuru.
 
Asha Dii
Tuletee mh. Zitto aingie kwenye mtandao ajibu direct kutoka kwa wahusika

Chama
Gongo la mboto DSM
 
ASHIDII unawapatia sana wanaouliza maswali ya ovyoovyo...napenda majibu yako.Yaani unawapa makavu yenye ukweli ndani yake.
 
Leka dutigite

ishaka maneke,tunayofurahaa kwa wazawa kigoma....aridhi yenye rutuba ya kuzalisha chelewa....
Mkuu uliza swali sio LEKA DUTIGITE hapa,Uliza swali Zitto amewasaidiaje wasanii kuondokana na wizi wa kazi zao kupitia ring tone(callertune) za kwenye simu.
 
AshaDii,

maswali yangu nayaelekeza kwako, why zito and not me ? kwa nini umeomba ruksa kwa founder wa jf kwani unategemea kupata any financial token from this interview? hii interview ina tija gani kwako, kwa zitto na jf members ?

Notorious stop being notorious bana! Why you basi na not Zitto? Lol.

On a serious note,

Kwa nini Zitto not you?

Namfaham kuwa ni mmoja wa mwanasiasa ambaye kuna baadhi ya wadau wengi wangependa majibu toka kwake directly. Nikaoa nianze na huyo. Nimeanza kumtafuta kitambo sio issue ya kusema kuwa I just called and he said yes! Hata hivo wewe pia ukitaka tuhojiane kwa interview sio mbaya mradi naomba u-verify user name yako.

Kwa nini nimeomba ruhusa kwa Jf founder?

Kuwezesha hili zoezi nahitaji msaada mkubwa sana toka kwa moderators, mimi kama mimi siwezi kitu hapa. Hiyo ndio ilinifanya niombe ruhusa kwa Melo, ili wakikubali wajue kuwa wana kazi ya kuni assist hadi zoezi zima liishe.

Kwa upande wangu napata mengi kwenye hii interview... Kwanza nakuwa na bahati (I consider it that) ya kuwasiliana na Mkuu Zitto Kabwe na kumuuliza maswali yoote ambayo huwa najiuliza juu yake huku pia nikipata bahati ya kuwawakilisha wana Jf kuwakilisha maswali yao. Sitegemei kupata pesa yoyote; nitapata vipi na hali mimi ndio nilitaka na nika-initiate...

Ila hivi you have brought it up nitashukuru ukiweza nikatia chochote kile ndani ya uwezo wako maana kwa kweli nimechacha ingawa ilitakiwa isiwe hivo kwani zumbemkuu alini ahidi asilimia 50% ya mapato yake jizi kati kwa ushahidi wa engmtolera anae nidai %1 ya hilo pato. :becky:
 
ASHIDII unawapatia sana wanaouliza maswali ya ovyoovyo...napenda majibu yako.Yaani unawapa makavu yenye ukweli ndani yake.
.

Wewe naye kilaza kweli kweli,kwani kazi ya kujibu maswali ni Ashadii au Zitto Zuberi Kabwe?Kituko cha karne!
 
........................................................

Ila hivi you have brought it up nitashukuru ukiweza nikatia chochote kile ndani ya uwezo wako maana kwa kweli nimechacha ingawa ilitakiwa isiwe hivo kwani zumbemkuu alini ahidi asilimia 50% ya mapato yake jizi kati kwa ushahidi wa engmtolera anae nidai %1 ya hilo pato. :becky:
halafu siku ile nilipata hela ya madafu laki 2 ya bwerere kweli......
nilikutafuta simu zako zote hupatikani, itabidi unipe namba nyingine sio zile za makontena.
leo tena najua ntapata mijihela....loh. ile ya siku ile naweka deni. (samahani kwa kuchakachua thread yako leo....teh teh teh)
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom