Poa sister nimekuelewa na naandaa maswali ya kumuuliza na kwa kuwa yeye anatka kuwa kiongozi wetu kwa siku zijazo asiogope kuulizwa maswali hata kama yatakuwa yanauzi lakini atakuwa amepata nafasi hadimu yakujua mawazo ya watu anaotaka kuwatawala!Nikiri kuwa mimi pia nina maswali ya kumuuliza na hata nikipata nafasi ya kukaa naye face to face tukizungumza tu yaliyo msingi na ndani ya maswali ambayo ninayo inaweza chukua sio chini ya masaa mawili ama zaidi. Naamini ningefanya jitihada zaidi hiyo nafasi ningepata...
Kwa muktadha huo Sijajihami Mkuu... Nimeona ni kheri nitoe tahadhari mapema sababu ni mpitaji mzuri tu hapa JLS, najua ni namna gani watu wanakuwa na sumu kali wakiona jina la Zitto ama lolote lihusulo yeye. Najua kuwa bila tahadhari basi tunaweza kuwa na pages za kejeli na tusipate yaliyo msingi. Nakuhakikishia kuwa maswali yote nitawakilisha na ndiyo maana nikaona nisiwe mchoyo wa hiyo nafasi nihusishe na members pia. Hivo Tukutuku kama una swali uliza na litafikishwa...
Karibu sana.
Mkuu mimi nafanya kazi na mwajiri wangu anajua mshahara wangu kwa kuwa yeye ndiye aliyeniajiri na ndiye anayeniandalia huo mshahara.Sisi kama wananchi ni kweli kabisa ni waajiri wa rais,lakini kuna utofauti kidogo kwa sababu there is no direct involvement in the supervision of our employee (Rais).Hata hivyo naamini ukienda ofisi ya rais utumishi unaweza kupata hizi taarifa bila shaka.
Nashukuru for the tag,mwaswali yapo lakini sidhani kama yatajibiwa.I'm pessimistic on this one.
Hakuna "direct involvement in the supervision of our employee" kivipi? No wonder tupo kwenye hali tuliyonayo!!!!
Na haya mambo ya "naamini ukienda ofisi ya rais utumishi unaweza kupata hizi taarifa bila shaka" ndiyo siyataki mimi. Kwanza unasema "unaamini", halafu unasema "unaweza", halafu katika sentensi hiyo hiyo unasema "bila shaka"!!
Good grief...wewe unajua au hujui?
Ashadii - "maisha binafsi" ndiyo "msingi" wa "maisha ya kiongozi mwadilifu"...! Binadamu awaye yote anapojaribu "kuficha masiha yake binafsi" fahamu fika kuwa huyo binadamu anayo mapungufu makubwa sana "ki-uongozi"...!
Nashukuru for the tag,mwaswali yapo lakini sidhani kama yatajibiwa.I'm pessimistic on this one.
Kuna uwezekano mkubwa nikawa msomaji tu.
Mkuu mimi sijui lakini siwezi kulaumu kwa kuwa binafsi sijawahi kufanya jitihada za kutafuta hizi taarifa.Kwa kifupi bila kumumunya maneno mimi nakuhakikishia hizi taarifa zinapatika ofisi ya rais utumishi.
Labda niulize kuwa unapo sema binafsi una maana gani? Kuna maswali binafsi... 'unapenda kula nini', 'siku gani huwezi sahau katika maisha yako?' 'unapenda maisha ya namna gani?' na the like...
Nimetoa hiyo tahadhari sababu watu hawachelewi kuleta maswali kama 'umewahi lala na wanawake wangapi?', 'girlfriend wako ni nani?' 'unafanya mapenzi mara ngapi kwa mwezi?' 'umewahi lala na AshaDii?'
Hivi umenipata maana yangu?
Naamini kabisa kuwa maisha ya Zitto binafsi ni open book, wengi wanamfahamu kwa mbali ama kwa kutokea anako tokea. Sasa kwa mtindo na maswali hayo sioni kuwa tukipata majibu yake kama lina faida yoyote kwa jamii.. Labda kama nakosea; but hivo ndio naamini.
Mwanangu Ashadii umeniudhi leo kwa mara ya kwanza. Inaonekana kama huyo Zitto wako ana matatizo mengi kiasi cha kuogopa baadhi ya mambo yasiguswe.
If indeed he is but a public figure hiyo protectionism ya nini? Hii maana yake ni kwamba unataka aulizwe anachotaka kuulizwa. Kwa mfano, kama ataulizwa ataoa lini au kwanini haoi na umri unakwenda kama kiongozi wa umma kuna ubaya gani? Maana wengi wanashangaa ni vipi ataweza kuongoza taifa iwapo hana hata uwezo wa kuwa na foundational unit yaani familia.
Pili kulikuwa na tetesi kuwa naye ameficha mafweza Uswisi. Hii inaweza kulenga kumchafua ili awagwaye waliofanya hivyo, je huoni kuwa hii ni nafasi adimu ya kuondoa shaka? Pia kama yeye ni mwanasiasa mahiri kwanini akingiwe kifua kama kichanga.
You seem to be a bundle of contradictions!
Unasema wewe hujui halafu hapo hapo "bila kumumunya maneno" unanihakikishia kuwa hizo "taarifa zinapatikana ofisi ya rais utumishi".
Hivi huoni unavyojikanganya?
Kujua taarifa zinapopatikana na kujua taarifa zenyewe ni vitu viwili tofauti.Sijui kwa nini unashindwa kunielewa.Sijui mshahara wa rais kwa sababu sikuwahi kilipa umuhimu jambo hili,kwa kazi ninayoifanya nafahamu hizi taarifa zilipo ndiyo maana nimekuhakikishia mkuu!
Nimejua kupitia kazi ninayoifanya,viongozi wote wa kitaifa wagebill yao ipo ofisi ya rais utumishi!Umejuaje kuwa huko utumishi ndipo zinapopatikana hizo taarifa?